Unapokuwa na Maswali Muhimu, Unahitaji Majibu Moja kwa Moja Kutoka Kwenye Chanzo.

Hili ndilo tunalofanya katika AskAnAdventistFriend.com.

Tovuti hii inaendeshwa na Waadventista wa Sabato waliojitolea na walio tayari kujibu maswali yako.

Sehemu kubwa ya maudhui yetu inajikita katika maswali ya kawaida kuhusu dhehebu la kikristo la Waadventista wa Sabato na kuhusu imani na misingi yake—pamoja na maswali ya jumla kuhusu imani, mambo ya kiroho, na Biblia. Tunapopokea maswali mengine au maombi ya mada, tunajitahidi kuongeza kwenye ratiba yetu ya uchapishaji kwa wakati.

Kila maudhui yanayochapishwa kwenye AskAnAdventistFriend hupitia mchakato wa kina wa ukaguzi ili tuweze kukupa majibu ya kina, ya moja kwa moja, na yanayotokana na Biblia.

Falsafa yetu

Yesu alipoishi duniani, alikuwa mfano wetu kamili wa maana halisi ya kuwa mtauwa. Alijali mahitaji ya wale walio karibu naye. Alikula na wenye dhambi na aliwapenda waliotengwa.

Badala ya kulazimisha dini au kutoa taarifa ngumu kwa wale walio karibu naye, alijua kuwa njia bora zaidi ya kuwaleta watu kwa Mungu ilikuwa kuwaongoza kwa upendo.

Tunaamini kuwa tumeitwa kufanya hivyo: kuongoza watu kwa Mungu kwa upendo.

Sote tuna maswali ambayo hatutaki kumuuliza tu mtu yeyote. Hilo linapotokea, ni muhimu kuwa na rafiki ambaye unaweza kuzungumza naye kwa uhuru, ambaye yuko tayari kukusaidia kupata majibu hayo.

Maswali yoyote ulionayo, yawezekana sisi pia tuliwahi kuwa nayo! (Hata yale ya aibu au ya kipumbavu.) Na kwa sababu tunaelewa unakotoka, tunataka kusaidia. Pamoja na AskAnAdventistFriend, unaweza kuwa na amani ya moyo kwamba unapata taarifa sahihi zaidi, moja kwa moja kutoka kwenye chanzo.

Waadventista wa Sabato ni nani?

Kanisa la Waadventista wa Sabato ni dhehebu la Kikristo la Kiprotestanti lililoanzishwa nchini Marekani katikati ya karne ya 18. Lilianza kutokana na kundi la Wakristo ambao walisikia dhamira kubwa ya kujifunza Maandiko kwa kina.

Leo, kuna Waadventista wa Sabato milioni 21 duniani kote. Pia zipo hospitali za Kiadventista, mifumo ya shule, shule za tiba na kinywa, huduma za msaada na kuifikia jamii, programu za kimishonari, na mengineyo.

Kila moja ya misingi ya imani ya Waadventista wa Sabato imejengwa katika msingi wa Maandiko. Waadventista wa Sabato hutafuta kuishi maisha kama Kristo alivyoishi, wakisogea karibu na Mungu kila siku.

Ni mapenzi ya Mungu kwamba kila mtu aingie mbinguni (2 Petro 3:9), na kama Waadventista wa Sabato, tunajitahidi kufanya sehemu yetu katika kukamilisha Agizo Kuu la Yesu:

Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
— Mathayo 28:19, 20 ( NKJV).

Kupeleka Habari Njema kwa mataifa yote ndicho kinachowasukuma Waadventista. Kupitia huduma zetu, tunategemea kupanua Ufalme wa Mungu.

Shukrani

AskAnAdventistFriend.com inafanya kazi kusaidia Konferensi Kuu ya Kanisa la Waadventista wa Sabato, na kwa ushirikiano na Taasisi ya Ellen G. White.

Shukrani maalum kwa Konferensi ya Oregon ya Waadventista wa Sabato kwa msaada wake wa ukarimu kwa ajili ya mradi huu.

Vipande kutoka katika filamu, Tell the World, vinatumika kwa ruhusa ya Konferensi Kuu ya Kanisa la Waadventista wa Sabato.