Tunaweza kukuombea?
Maombi yana nguvu. Tunapoomba, tunawasiliana na Mungu, tunasaidiana, tunakaribisha uwepo wa Mungu katika maisha yetu, na tunafungua mioyo yetu kwa uongozi wa Roho Mtakatifu.
Biblia inatuambia “Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.” (Wafilipi 4:6, NKJV).
Biblia pia inatuambia kubebeana mizigo. Kuombeana ni njia bora zaidi ya kufanya hivyo. Hivyo, ikiwa kuna mizigo unayotamani tubebe kwa ajili yako katika maombi, au sifa unazotamani tusherehekee pamoja nawe katika maombi, jaza sanduku la maombi hapa chini.
Iwe unahitaji maombi kwa ajili ya uponyaji, kutiwa moyo, imani, au chochote kingine kilichomo moyoni mwako, rafiki zako Waadventista wataomba kwa dhati kwa ajili yako.
Tushirikishe katika Ombi Lako
Ikiwa unaomba kwa ajili ya uponyaji wako, au wa mpendwa wako:
- “Uniponye, Ee BWANA, nami nitaponyeka; uniokoe, nami nitaokoka; kwa maana wewe ndiwe uliye sifa zangu.” (Yeremia 17:14, NKJV)
- “Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA, Wala usizisahau fadhili zake zote. Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote, Aukomboa uhai wako na kaburi, Akutia taji la fadhili na rehema.” (Zaburi 103:2-4, NKJV).
- “Huwaponya waliopondeka moyo, Na kuziganga jeraha zao.” (Zaburi 147:3, NKJV).
Ikiwa unaomba katika wakati wa huzuni:
- “BWANA yu karibu nao waliovunjika moyo, Na waliopondeka roho huwaokoa.” (Zaburi 34:18, NKJV).
- “Mwili wangu na moyo wangu hupunguka, Bali Mungu ni mwamba wa moyo wangu Na sehemu yangu milele.” (Zaburi 73:26, NKJV).
- “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;” (Mathayo 11: 28-30, NKJV).
Ikiwa unaombea amani kwa ajili ya siku zijazo:
- “Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga” (Yohana 14:27, ESV).
- “Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho. Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza. Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.” (Yeremia 29:11-13, NKJV).
- “Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.” (Warumi 8:38-39, NKJV).
Ikiwa unaomba kwa ajili ya ushindi dhidi ya hofu:
- “usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.” (Isaya 41:10, NKJV)
- “Naam, nijapopita katika bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji” (Zaburi 23:4, NKJV).
- “Iweni hodari na moyo wa ushujaa, msiogope wala msiwahofu; kwa maana BWANA, Mungu wako, yeye ndiye anayekwenda pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha.” (Kumbukumbu la Torati 31:6, NKJV).
Chochote unachokiombea, maombi yako yatashughulikiwa kwa upole, kwa faragha kamili, na bila kuhukumiwa. Tunaamini katika nguvu ya maombi kubadilisha mioyo yetu, kutegemeana, na kumfikia Mungu na kudai ahadi Zake.
