Ellen White na Kitabu cha Pambano Kuu

Pambano Kuu ni moja ya vitabu vya Ellen G. White vinavyo thaminiwa zaidi na Waadventista wa Sabato.

Kati ya maandishi yake yote, hiki ni moja ya vitabu ambavyo alitumia jitihada kubwa za maombi. Kinaunganisha unabii wa Biblia na historia baada ya Biblia na kujadili mambo yatakayo ambatana na matukio ya siku za mwisho.

Katika chapisho hili, utajifunza zaidi kuhusu Ellen White na kitabu chake Pambano Kuu, na kwa nini kina umuhimu mkubwa miongoni mwa Waadventista.

Hapa kuna mambo matatu kuhusu kitabu ambayo tutayajadili:

Tuanze kwa kukupa muhtasari wa kitabu chenyewe.

Kitabu cha Pambano Kuu kinahusu nini?

Kitabu Pambano Kuu kinajadili karibu miaka 2000 ya historia na kuonyesha jinsi ulimwengu umekuwa ukisonga mbele dhidi ya mandhari ya unabii wa Biblia.

Wazo la “Pambano Kuu” linahusu mapambano ya ulimwengu kati ya Mungu na Shetani (wema na uovu), ambayo yamekuwa yakiendelea tangu Lusifa alipotupwa kutoka mbinguni (Ufunuo 12:7-9). Kitabu hiki kinaonyesha jinsi ambavyo mgogoro huu umekuwa ukiendelea tangu mwaka 70 AD, kisha kinazungumzia maendeleo ya historia, ikiwa ni pamoja na kuweka jukwaa la mwisho wa mambo—wakati wa ujio wa Pili wa Yesu na Kuumbwa upya kwa Dunia.

Kinaelezea mapambano yaliyo kuwepo katika kudumisha usafi wa ukweli wa Biblia katika kanisa la Kikristo. Na jinsi mataifa tofauti, harakati, na watu binafsi walivyochukua sehemu yao, kwa njia nzuri na potofu, katika kuendeleza matengenezo.

Pia inaonyesha jinsi Mungu daima alivyosababisha Ukweli wake kushinda licha ya dhuluma kubwa na upinzani dhidi ya Biblia na waamini waaminifu wa Biblia.

  • Kinashughulikia nyakati tofauti kama zama za Giza, na Matengenezo.
  • Kinasisitiza kuhusu uamsho wa kidini kama uamsho mkubwa wa Kwanza na wa Pili na Vuguvugu la ujio wa pili wa Kristo.
  • Kinaeleza visa vya watu waliokuwa waaminifu kwa Mungu ambao mara nyingi walitoa maisha yao kwa ajili ya ukweli na uhuru. Visa vya watu kama Yohane Huss, Martin Luther, Waaldensia, n.k.
  • Inaonyesha jinsi vitendo vya mataifa, hata falme na viongozi wao, vimetimiza unabii wa Biblia.

Na kuhusu ulimwengu wetu wa sasa na mambo yajayo, Pambano Kuu hutoa hekima kuhusu maswali ambayo mara nyingi yanatusumbua:

  • Kwa nini Mungu mwenye upendo aruhusu dhambi na mateso?
  • Nini hutokea tunapokufa?
  • Jinsi muungano wa kidini na kisiasa utakavyo tishia uhuru wetu siku moja.
  • Jinsi tunavyoweza kujiandaa kufanya sehemu yetu katika pambano hili kati ya wema na uovu, na mitego ipi ya kuepuka.
  • Je, mataifa fulani yana jukumu dhahiri katika unabii wa Biblia?
  • “Alama ya mnyama” ni nini?
  • Mpinga Kristo ni nani au ni nini?
  • Uovu utashindwa vipi hatimaye?

Zaidi ya yote, kitabu hiki kinatuongoza kwa tumaini letu kuu, Yesu Kristo.

Kinaonyesha kwamba baada ya yote kusemwa na kufanywa, Yesu atakuja na kufanya mambo yote kuwa mapya. Hatimaye, ni upendo wake, rehema, na haki itakayoshinda vurugu ambayo ulimwengu wetu umekumbwa nayo.

Ndani ya kitabu, Pambano Kuu

Kitabu cha Pambano Kuu kina kurasa 678, kikiwa na sura 42.

Pia kina maelezo ya mwanzo yaliyoandikwa na Ellen White, ambayo hufanywa kama utangulizi. Humo, yeye kwa uangalifu anaelezea jinsi uvuvio wa Roho Mtakatifu ulivyo chanzo cha habari zake.

Hapa kuna muhtasari mfupi wa yaliyomo katika kitabu:

  • Sura ya 1 – Kuharibiwa kwa Yerusalemu
  • Sura ya 2-6 – Mateso dhidi ya Wakristo katika Ufalme wa Kirumi na uasi katika Zama za Giza
  • Sura ya 7-16 – Matengenezo
  • Sura ya 17-22 – Uamsho wa kidini ulimwenguni katika karne ya kumi na tisa.
  • Sura ya 23-38 – Ufafanuzi kuhusu imani muhimu za Waadventista (kama mamlaka ya Maandiko, patakatifu pa mbinguni, hukumu ya upelelezi na hali ya wafu) na umuhimu wake leo.
  • Sura ya 39-42 – Matukio ya siku za mwisho, Kurudi kwa Pili, kukomeshwa kwa dhambi na kuumbwa upya kwa dunia mwisho wa Pambano.

Kwa nini kitabu cha Pambano Kuu ni muhimu?

Waadventista wanakitazama kitabu hiki kama kitabu chenye thamani kubwa kwa sababu kinaonyesha hatua muhimu katika Pambano Kuu na mpango wa wokovu. Kitabu hiki kinatusaidia katika kujifunza Biblia, hasa katika dhana ambazo huchukua muda kuelewa.

Kinaangazia mambo yaliyopita na kuonyesha jinsi matukio ya kihistoria yalivyo timiza unabii wa Biblia. Na jinsi unabii wa Biblia utakavyotimizwa baadaye.

Pia kinatupa mtazamo ambao tunaweza kuona matukio ya ulimwengu wa sasa kwa mwanga wa unabii wa Biblia. Kinaonyesha jinsi pambano linavyoendelea katika siku hizi, na jinsi tunavyoweza kuwa upande wa Mungu.

Na ni muhimu zaidi kwa Waadventista kwa sababu katika siku za mwanzo za dhehebu, kulikuwa na juhudi maalum za kuelewa unabii wa Biblia. Unabii ulikuwa mada ambayo mara chache ilijadiliwa kabla ya wakati huo, angalau kwa mtu wa kawaida ambaye hakuwa mchungaji.

Tangu katika mianzo kabisa, Waadventista kwa ujumla wameendelea kuwa na mtazamo wa kutaka kufahamu matukio ya siku za mwisho. Na daima wamejaribu kuelewa unabii wa Biblia kwa kusoma Biblia kwa makini.

Kwa hivyo tangu mara ya kwanza kilipochapishwa, kitabu hiki kilipokelewa vizuri na Kanisa kwani kilitoa muhtasari wazi wa kutimia kwa unabii wa Biblia uliopita na ujao. Pia, kilitoa mwongozo muhimu sana kwa ajili ya kukabiliana na matatizo ya sasa.

Na juu ya yote, kinaeleza kwa undani mada ya Pambano Kuu, namna ya kujifunza Biblia ifaayo. Unapata kuona jinsi kila aya ya Biblia inavyolingana katika muktadha wa pambano endelevu kati ya wema na uovu. Na mandhari hii imesaidia daima tafsiri sahihi na matumizi ya Maandiko katika maisha ya Kikristo ya kila siku.

Kwa kweli, ufahamu wa Pambano Kuu lenyewe (tukio linalokipatia kitabu jina lake), na jinsi kila utafiti wa kimaandiko na kihistoria unavyolingana katika muktadha wake mkubwa, umewekwa kama moja ya misingi ya imani ya Waadventista wa Sabato. Imefupishwa katika tovuti rasmi ya Waadventista kama imani namba 8, iitwayo, Pambano Kuu.

Hata leo, kitabu cha Pambano Kuu kinaendelea kuwa na manufaa, kuwa muhimu, na kufungua macho. Kinafundisha masomo muhimu ambayo yanaweza kutusaidia kutembea katika wakati wetu wa sasa na kuwa tayari kwa ajili ya siku zijazo, huku tukiepuka majaribu na vikwazo vya Shetani.

Pia unaweza kuona jinsi Mungu alivyyotunza kweli yake katika kipindi kigumu zaidi katika historia. Na jinsi alivyoinua vuguvugu moja baada ya jingine ili kuhifadhi Biblia wakati ilipokuwa imepigwa marufuku. Jinsi watu waaminifu waliopenda ukweli walivyokuwa tayari kusimama kwa ajili ya uhuru na hata kufa badala ya kuacha ukweli walioupenda.

Kila mtu anaweza kuona jinsi Maandiko yanavyoleta mabadiliko safi na ya heshima katika jamii au mtu binafsi. Na ni vigumu kutokiri kwamba Mungu daima anasimama nyuma ya Neno lake kulilinda na kulitimiza, yote kwa faida yetu ya milele.

Na katika kipindi chote cha nyakati tofauti, tamaduni na maendeleo ya jamii, unaweza kuona upendo wa Mungu ukiendelea kufanya kazi kwa bidii kuokoa ulimwengu kutoka katika dhambi na udanganyifu.

Lakini jambo muhimu zaidi, kitabu hiki kinaelekeza kwenye ushindi mkuu wa Mungu juu ya Shetani, wa wema juu ya uovu, na upendo juu ya vitu vyote.

Kinaonyesha kwamba ingawa ulimwengu huu umekuwa uwanja wa vita wa pambano hili, mustakabali mzuri uko mbele kwa sayari yetu, na kwa ulimwengu mzima.

Tunaona kuwa ujio wa pili wa Yesu unaweza kutokea mapema kuliko tunavyoweza kufikiria, na itapelekea mwanzo mpya na mwisho wa dhambi (Ufunuo 21:4). Na yote tunayohitaji kufanya ili tuwe sehemu ya mwisho huu wenye ushindi ni kukubali zawadi ya bure ya wokovu ambayo Yesu anatupatia.

Kuandika na kuchapishwa kwa Pambano Kuu

Kitabu cha Pambano Kuu kilichapishwa kwa mara ya kwanza mnamo 1858 na mume wa Ellen White, James White. Hii ilifuatiwa na upanuzi wa maudhui uliosababisha matoleo mengine mawili mnamo 1844 na 1888. Kisha toleo la mwisho mnamo 1911.

Katika sehemu hii, tutachunguza kwa nini kitabu hicho kiliandikwa, na hatua tofauti za maendeleo ya kitabu hadi kufikia toleo la sasa.

Kwa nini Ellen G. White aliandika kitabu cha Pambano Kuu?

The schoolhouse in Lovett's Grove, Ohio, where Ellen White received the vision about the great controversy

Courtesy of the Ellen G. White Estate, Inc.

Ellen White mwenyewe anajibu swali hili. Anasema alionyeshwa kwamba lazima aandike1 katika maono aliyopokea mwaka 1858.

Lakini safari ya kuandika kitabu hiki ilianza mwaka 1848.

Wakati huo, aliona maono ambayo yalimpa mtazamo mpana sana wa pambano lililokuwepo kwa muda mrefu kati ya Mungu na Shetani. Mgogoro kati ya wema na uovu ulioanza mbinguni kabla ya dunia kuumbwa. Na utakaoisha wakati dhambi itakapokomeshwa milele na dunia kuumbwa upya, kama ilivyoelezwa katika kitabu cha Ufunuo.

Kisha miaka 10 baadaye, akihudhuria mazishi huko Lovett’s Grove, Ohio, mwezi wa Machi 1858, aliona maono mengine kuhusu mada hiyo hiyo.

Maono yalidumu kwa masaa mawili. Alieleza kwamba mengi ya yale aliyoyaona katika maono ya mwaka wa 1848 yalirudiwa. Kisha maelezo zaidi yalitolewa ili awe na ufahamu mpana zaidi wa matukio hayo.

Ndipo alipoagizwa kuandika yale aliyokuwa ameonyeshwa. Pia alionywa kwamba wakati wa kuandika kitabu, Shetani angejaribu kumzuia, lakini bado angepaswa kuendelea kufanya hivyo. Roho Mtakatifu wa Mungu angemwongoza.

Siku inayofuata, Ellen na James walianza kupanga kuchapisha maandishi haya walipokuwa wakisafiri kurudi nyumbani Battle Creek, Michigan.
Waliposimama kumtembelea rafiki wa familia huko Jackson, Michigan, Ellen White alipooza.

Lakini kama jibu la maombi mengi yaliyotolewa kwa ajili yake, alipona sehemu siku iliyofuata na kwenda nyumbani.

Hii ilikuwa shambulio lake la kwanza alipokuwa akifanyia kazi kitabu hiki.

Alipoanza, alikuwa anaweza kuandika ukurasa mmoja tu kwa siku. Kisha angechoka na kulazimika kupumzika kwa siku tatu. Lakini alivyo songa mbele, alipata nafuu. Kufikia wakati alipomaliza kuandika kitabu katikati ya Agosti, alikuwa amerudi katika afya yake ya kawaida.

Na mwezi Septemba, 1858, toleo la kwanza kati ya manne la kitabu lilikuwa tayari kwa usambazaji.2

Matoleo manne ya Pambano Kuu

Baada ya kuchapisha kitabu cha awali kuhusu Pambano kati ya Yesu na Shetani, Ellen White aliendelea kuongeza maelezo kadri miaka ilivyoendelea.

Hatimaye kulikuwa na matoleo manne kufikia wakati alipofariki. Yanayo jumuisha:

Toleo la mwaka 1858

Kitabu kilicho chapishwa kiliitwa: Karama za Roho, Toleo la 1: Pambano Kuu Kati ya Kristo na Malaika Zake, na Shetani na Malaika Zake.

Kilikuwa cha kwanza katika mfululizo wa vitabu vinne vilivyo andikwa kati ya mwaka 1858 na 1864.

Ilikuwa na kurasa 219 zilizozingatia tu sehemu kuu za historia ya pambano kwa mpangilio wa mpangilio.
Kilikuwa na:

  • Sura 3 za Agano la Kale zinazojadili kuanguka kwa Shetani, Anguko la mwanadamu, na Mpango wa Wokovu.
  • Sura 13 kuhusu maisha na huduma ya Yesu na mitume.
  • Sura 25 kuhusu Uasi Mkubwa wa Kanisa la Kikristo la awali, Matengenezo, Vuguvugu la Kuja kwa Bwana, hadi kwa matukio ya mwisho wa dunia na mwisho wa dhambi.

Toleo la mwaka wa 1884

Hii ilikuwa na kichwa, Roho ya Unabii, Toleo la 4. Kama jina linavyoonyesha, ilikuwa sehemu ya mfululizo wa vitabu vinne, Roho ya Unabii.

Mfululizo mzima uliongeza maelezo zaidi kuhusu Pambano Kuu, kutoa maelezo zaidi kuliko yale yaliyowasilishwa katika toleo la mwaka 1858.

Ilikuwa imepangwa ili kila kitabu kiweze kujikita katika kipindi maalum kama ifuatavyo:

  • Kitabu cha 1, kilichochapishwa mwaka 1870: Kipindi cha Agano la Kale.
  • Kitabu cha 2, kilichochapishwa mwaka 1877: Maisha na huduma ya Yesu.
  • Kitabu cha 3, Kilichochapishwa mwaka 1878: Kuanzishwa kwa kanisa la Kikristo la awali na Matendo ya Mitume.
  • Kitabu cha 4, Kilichochapishwa mwaka 1884: Historia ya kanisa la Kikristo, ikianza na kuharibiwa kwa Yerusalemu mwaka wa 70 BK. Kisha kinageukia pambano linaloendelea leo na kuelekea mwisho wa nyakati.3

Ni toleo la 4 lililokuwa limeongezwa ili kuunda kitabu kinacho julikana kama Pambano Kuu leo. Kikijikita katika vipindi vya kihistoria vya Zama za Giza na Matengenezo.

Kuandika juu ya hili, alisoma vitabu vya historia kama Historia ya Matengenezo ya D’Aubigne, ambayo ilimsaidia kutambua na hivyo kuelezea kwa undani matukio mengi na wahusika aliowaona katika maono.4

Kitabu cha Roho ya Unabii Kitabu cha 4 kilichapishwa katika namna mbili:

– Moja, rangi ya zeituni, Kilichopewa jina, Pambano Kuu Kati ya Kristo na Malaika Wake na Shetani na Malaika Wake.
– Ya pili, katika kitambaa cheusi, Kilichopewa jina, Roho ya Unabii, Toleo la 4.

Kitabu kilipokelewa vizuri. Na ndani ya miaka 3, nakala 50,000 ziliuzwa.

Toleo la mwaka wa 1888

Ellen White alitembelea Ulaya kati ya 1885 hadi 1887.

Kutokana na mwingiliano wake na watu na ziara katika maeneo tofauti ya kihistoria, alitambua mazingira yake kuwa sawa na aliyoyaona katika maono. Maeneo kama Zurich, Uswisi, ambapo Zwingli alifanya kazi, na mabonde ya Waaldensia nchini Italia.

Haya yalikuwa maeneo muhimu katika pambano wakati wa Matengenezo.

Kisha wakati huo huo, kulikuwa na mipango ya kuchapisha Roho ya Unabii Kitabu cha 4 (Pia kinaitwa: Pambano Kuu Kati ya Kristo na Malaika Zake na Shetani na Malaika Zake) katika lugha za Ulaya.

Hivyo akaamua kuongeza maelezo zaidi ya matukio yaliyotokea Ulaya kwenye hati ya tafsiri.

Akifanya kazi hii, alisema kwamba “alikuwa mara nyingi na ufahamu wa uwepo wa malaika wa Mungu. Na mara nyingi mandhari ambayo nilikuwa naandika ilirudiwa kwangu tena katika maono ya usiku, hivyo kwamba ziliikuwa wazi na hai akilini mwangu.”5

Ni wakati huu ambapo aliandika Kisa chote cha Pambano kati ya Mungu na Shetani kikaongezwa na kuandikwa katika vitabu vitano tofauti, badala ya vitabu vinne.

Vitabu sasa vinajulikana kama mfululizo wa Pambano la Vizazi Vyote.

Pamoja, viliangazia muda wote wa Pambano Kuu kati ya Yesu na Shetani.

Hivyo, Mfululizo Ulioongezwa wa Roho ya Unabii, Kitabu cha 4 mwishowe kikawa kitabu cha mwisho katika mfululizo wa vitabu 5. Ilikuwa na kichwa, Pambano Kuu Kati ya Kristo na Shetani Wakati wa Enzi ya Kikristo.

Kiliangazia tangu kuharibiwa kwa Yerusalemu hadi mwisho wa Pambano.

Vitabu vingine 4 katika Mfululizo wa Pambano la Vizazi vyote ulikuwa na majina yafuatayo:

Leo, vitabu hivi vinachukuliwa kama seti na mara nyingi huuzwa pamoja.

Kitabu cha mwaka 1888 kikawa kile tunachokijua leo kama kitabu chenye jina, Pambano Kuu

Toleo la mwaka wa 1911 la Pambano Kuu.

Toleo hili ndio kitabu cha kawaida kinachotumiwa ulimwenguni kwa Kiingereza na tafsiri nyingine. Ni marekebisho ya toleo la mwaka 1888.

Lilirekebishwa ili kuhakikisha kwamba ukweli uliomo katika kitabu ulielezwa kwa namna bora kabisa kwa viwango tofauti vya wasomaji.

Kitabu kilichapishwa mwezi Julai 1911 na Pacific Press na Review and Herald Publishing Association.

Kwa miaka sasa, kimechapishwa na kusambazwa kwa wingi.

Huu ni mwitikio kwa uhamasishaji wa Ellen White wa kusambaza kitabu hiki, hata zaidi kuliko vitabu vyake vingine vyote:

“Pambano Kuu kinapaswa kusambazwa sana. Kina historia iliyopita, ya sasa, na ya baadaye. Katika muhtasari wake wa matukio ya mwisho ya historia ya dunia hii, kinatoa ushuhuda wenye nguvu kwa niaba ya ukweli. Nina shauku zaidi kuona usambazaji mpana wa kitabu hiki kuliko vingine vyote nilivyoandika; kwa sababu katika Pambano Kuu, ujumbe wa mwisho wa onyo kwa ulimwengu unatolewa kwa uwazi zaidi kuliko katika vitabu vyangu vingine.”6

Tangu chapisho lake la kwanza, kitabu hiki kimeisaidia roho zisizo hesabika kupata njia kwa Yesu na kupokea zawadi hii.

Hapa kuna nakala ya bure ya Pambano Kuu unayoweza kusoma au kusikiliza hata leo.

  1. Ellen G. White, Life Sketches of Ellen G. White, pp. 162-163. []
  2. Ellen G. White, Selected Messages, Book 3, (Review and Herald Publishing Association, 1980), p. 100. []
  3. Ellen G. White, The Great Controversy (1888), p. xi. []
  4. Ellen G. White, Selected Messages Book 3, p. 437. []
  5. Ellen G. White, Colporteur Ministry, p.128. []
  6. Ellen G. White, Letter 281, 1905. []

Je, Una swali kuhusu Waadventista? Uliza hapa!

Pata majibu kwa maswali yako kuhusu Waadventista Wasabato

Majibu Zaidi