Biblia Inasema Nini Kuhusu Deni?
Kuwa na wasiwasi kuhusu deni la kifedha kunaweza kutufanya tuamke tukiwa na kijasho chembamba.
Kwa watu wengi, deni linaonekana kama sehemu muhimu ya maisha. Lakini yeyote aliye na mikopo ya masomo inayomsonga au mlima wa bili za matibabu anajua sio jambo linalopendeza.
Na inaweza kutuacha tukijiuliza: Biblia inasemaje kuhusu deni? Je, deni ni dhambi? Ni jambo la kawaida? Au sio?
Biblia inasema katika Warumi 13:8, “Msiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana” (NKJV).
Lakini pia inasema, “Heri atendaye fadhili na kukopesha; Atengenezaye mambo yake kwa haki” (Zaburi 112:5, NKJV).
Maandiko yanasisitiza kanuni za kukopesha na kusamehe madeni zaidi kuliko deni la kifedha.
Wakati huo huo, inazungumzia kuhusu kuwa mkopaji anayewajibika na matokeo ya deni.
Hivyo hata ingawa Biblia haikukusudiwa kuwa mwongozo wa kifedha, tunaweza kujifunza kanuni nyingi zinazofaa katika kushughulikia deni. Hivyo basi, tupitie Maandiko na kujadili:
- Kama deni lenyewe ni dhambi
- Kanuni kumi za Biblia kuhusu deni la kifedha
- Kwa nini mambo haya ni muhimu kwetu leo
Hebu tuanze na habari njema: Biblia haihukumu mtu yeyote tu kwa kuwa na madeni.
Na tunapoangalia kile Maandiko yanachosema kuhusu deni la kifedha kwa ujumla, mwongozo wenye upendo wa Mungu na wema wake unang’aa.
Basi hebu tuanze kwa kushughulikia swali la kawaida.
Je, Biblia inasema kuwa deni ni dhambi?

Photo by Kaboompics.com
Hapa ni jibu fupi: Hapana. Biblia haiiti deni kuwa dhambi.
Hii inaonekana wazi hasa kwa jinsi Mungu anavyohamasisha kukopesha—jambo linalowafanya watu kuwa wadeni wetu. (Tutajadili hilo katika sehemu inayofuata).
Lakini pia tunaweza kuona onyo katika aya za Biblia kwamba deni sio kusudi la Mungu, pia:
“Tajiri humtawala maskini, Naye akopaye ni mtumwa wake akopeshaye” (Mithali 22:7, NKJV).
“Na kila mtu aliyekuwa katika hali ya dhiki, na kila mtu aliyekuwa na deni, na watu wote wenye uchungu mioyoni mwao, wakakusanyika kwake… [Daudi]” (1 Samweli 22:2, NKJV).
Je, ni ajabu Biblia inavyounganisha deni na uchungu, dhiki, na utumwa? Inaonekana kama deni linavyoonekana leo pia kwa sehemu kubwa.
Katika ulimwengu huu wenye dhambi, deni linaweza kutuletea matatizo makubwa. Linatuweka chini ya wale ambao hawana nia njema moyoni mwao. Linaweza kuwa kikwazo katika uwezo wetu wa kuelekea maisha yenye mafanikio, kutoa kila kitu tunachotaka kuwapa watoto wetu, au kusaidia mambo tunayojali.
Lakini tutagundua kwamba ingawa deni sio kusudi la Mungu, hali hiyo haibadilishi upendo wake kwetu au nia yake ya kutusaidia au kufanya kazi kupitia kwetu.
Na yeye hatuachi tukabiliane nalo peke yetu.
Katika Nehemia 5, watu wa Israeli walikuwa katika hali ya kukata tamaa kutokana na njaa. Wengi walilazimika kupata mikopo kwa ajili ya nyumba zao na ardhi – na hata kutoa watoto wao kama watumwa – ili kulipa chakula na kodi.
“Walakini miili yetu ni kama miili ya ndugu zetu, watoto wetu kama watoto wao; kumbe! Mnawatia utumwani wana wetu na binti zetu kuwa watumishi, na baadhi ya binti zetu wamekwisha kutiwa utumwani; wala hatuwezi kujiepusha na hayo; maana watu wengine wana mashamba yetu na mizabibu yetu” (Nehemia 5:5, NKJV).
Hivi ndivyo Nehemia anavyojibu:
“Nami nilikasirika sana, niliposikia kilio chao, na maneno hayo. Ndipo nikafanya shuri na nafsi yangu, nikagombana na wakuu na mashehe, nikawaambia, Mnatoza watu riba, kila mtu ndugu yake. Nikakutanisha mkutano mkubwa ili kushindana nao” (Nehemia 5:6-7, NKJV).
Nehemia ana wasiwasi kuhusu dhuluma kwa wale walio katika hali ya uhitaji mkubwa. Na anawakemea matajiri wa Israeli kwa kuwatoza viwango vya juu vya riba.
Hatumsikii Nehemia akiwalaumu watu waliokuwa na madeni. Hata anawakopesha pesa na nafaka yeye mwenyewe. (Lakini fahamu, hawakuwa wakikopa kwa ajili ya anasa na likizo, bali kwa sababu walikuwa wanateseka na njaa.)
Mpaka sasa, hatujaona deni likilaaniwa kama dhambi. Isaya 24:2 hata inasema Mungu hatuhukumu kulingana na hali yetu kifedha:
“….kama ilivyo hali yake akopeshaye, ndivyo itakavyokuwa hali yake akopaye….” (NKJV).
Lakini tunapata mitazamo mingi kuhusu kwa nini haichukuliwi kama “Mpango A.” Na tunaona kwamba Biblia inachukulia swala la kuwakopesha wengine kwa uzito.
Lakini hiyo ni kiduchu tu. Basi hebu tuchunguze mada kumi muhimu za kifedha kutoka katika Biblia.
Kanuni Kumi muhimu ambazo Biblia inatoa kuhusu deni
Kutoka katika Agano la Kale hadi Agano Jipya, Mungu anashughulikia mengi kuhusu maswala ya kifedha.
Na ni hekima ambayo bado tunahitaji leo.
Biblia inashauri ni lini, vipi, na nani wa kumkopesha—na juu ya wajibu unaoambatana na deni. Mungu anafundisha uwakili, msamaha wa deni, kuishi bila deni, na jinsi ya kumtegemea.
Lakini kwanza, hebu tupate maelezo kuhusu kukopesha.
Ushauri wa Biblia kwa wakopeshaji

Photo by Lukas
Biblia mara nyingi inahusisha kukopesha na ukarimu. Kwa hivyo si ajabu kwamba Mungu anahamasisha Wakristo kukopesha.
“Mchana kutwa hufadhili na kukopesha, Na mzao wake hubarakiwa” (Zaburi 37:26, NKJV.
Katika Agano Jipya, Yesu anasema:
“Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo” (Mathayo 5:42, NKJV).
Biblia pia inatoa ushauri sahihi kuhusu wakati na jinsi ya kukopesha.
Tuanze na wakati ambapo Biblia inasema tuwakopeshe wengine.
Wakati Biblia Inasema tukopeshe
Inasema kwamba tunapaswa kukopesha wale ambao ni maskini na wenye mahitaji:
“Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo?” (1 Yohana 3:17, NKJV).
“Na ikiwa ndugu yako amekuwa maskini, na mkono wake umelegea kwako, ndipo utamsaidia, atakaa nawe kama mgeni na msafiri” (Walawi 25:35, NKJV).
“Kama akiwapo mtu maskini pamoja nawe, nduguzo mmojawapo, ndani ya malango yako mojawapo, katika nchi yako akupayo BWANA, Mungu wako, usifanye moyo wako kuwa mgumu, wala usimfumbie mkono wako nduguyo maskini; lakini mfumbulie mkono wako kwa kweli, umkopeshe kwa kweli yatoshayo haja yake katika ahitajiayo” (Kumbukumbu la Torati 15:7-8, NKJV).
Jambo linalofanana katika aya zote tatu ni kutaja kuwakopesha ndugu. Lakini hilo lina maana gani?
Katika Nehemia na Kumbukumbu la Torati, “ndugu” inahusu walio ndani ya jamii yako.
Na katika Agano Jipya, Yesu anasema, “Kwa maana yeyote atakaye yafanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni, huyu ndiye ndugu yangu, na umbu langu na mama yangu” (Mathayo 12:50, NKJV).
Biblia inatuagiza kuwatunza watu wenye mahitaji – hasa wale walio katika makanisa yetu na jamii zetu.
Na hilo linajumuisha ndugu zetu wa moja kwa moja:
“Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini” (1 Timotheo 5:8, NKJV).
Lakini hilo halimaanishi kwamba kukopesha wageni ni kosa. Tumeona katika Mambo ya Walawi kwamba inachukuliwa kama jambo la kawaida kila mtu kuwatendea vizuri wageni na wasafiri.
Lakini upendo wa Mungu unang’aa kupitia sisi tunapokumbuka kuwabariki wahitaji walio karibu nasi.
Na hili halihusu pesa pekee. Inaweza maanisha kukopesha vyakula, magari, muda, vyumba vya ziada, au chochote unachoweza kuwa nacho kinacholingana na mahitaji.
Hivyo jibu la “lini” ni “popote unapopata fursa!”
Sasa tuangalie aya zinazojadili jinsi ya kukopesha.
Namna ya kukopesha katika Biblia

Photo by Kaboompics.com
Biblia inatuambia tukopeshe kwa ukarimu, na kawaida bila kutoza riba (Mathayo 10:8, Walawi 25:36-37).
Aya inayofuata inasema ni sawa kutoza riba kwenye mikopo kwa wageni, lakini sio kwa watu tunao husiana nao:
“Usimkopeshe ndugu yako kwa riba; riba kwa fedha, riba ya vyakula, riba ya kitu cho chote kikopeshwacho kwa riba. Mgeni waweza kumkopesha kwa riba, ila usimkopeshe ndugu yako riba; ili BWANA, Mungu wako, apate kukubarikia katika yote utiayo mkono wako, katika nchi uingiayo kuimiliki” (Kumbukumbu la Torati 23:19-20, NKJV).
“Ukimkopesha mtu aliye maskini, katika watu wangu walio pamoja nawe; usiwe kwake mfano wa mwenye kumdai; wala hutamwandikia faida” (Kutoka 22:25, NKJV).
Pia tunapaswa kutoa bila kutarajia au kudai chochote. Na utoe kwa ukarimu (Luka 6:30, Luka 6:35, NKJV).
Kumbukumbu la Torati 15:10-11 inaonyesha kwa nini Mungu hutuhamasisha kukopesha. Kwa sababu mpaka mwisho wa dunia, tutakutana na watu wanaohitaji:
“Mpe kwa kweli, wala moyo wako usisikitike utakapompa; kwa kuwa atakubarikia BWANA, Mungu wako, kwa neno hili katika kazi yako yote, na katika kila utakalotia mkono wako. Kwa maana maskini hawatakoma katika nchi milele; ndipo ninakuamuru na kukwambia, Mfumbulie kwa kweli mkono wako nduguyo, mhitaji wako, maskini wako, katika nchi yako” (NKJV).
Riba kubwa katika Biblia
Biblia inatuamuru kuepuka riba kubwa tunapokopesha. Na hiyo ni tofauti na riba ya kawaida. Hata leo, riba iliyozidi ni kinyume cha sheria na tuna sheria kuhusu hilo.
Kulingana na Idara ya Fedha ya Jimbo la Washington:
“‘Riba ya kupita kiasi’ ni kitendo haramu cha kutoza riba kwenye deni…kwa kiwango kikubwa kuliko kilichoruhusiwa chini ya sheria yoyote inayotumika… .”
Fikiria viwango vya kadi za mkopo—na zaidi.
Hivyo ushauri wa Biblia kuhusu kuwa wakopeshaji wanaowajibika ni wa milele:
“Hakutoa fedha yake apate kula riba, Hakutwaa rushwa amwangamize asiye na hatia. Mtu atendaye mambo hayo hataondoshwa milele” (Zaburi 15:5, NKJV).
Tuangalie tena ushauri wa Kibiblia kwa wakopeshaji.
Inasema tutoe bure, toza riba kidogo au usitoze kabisa, na usitarajie kupata chochote.
Lakini hilo linaweza kuonekana kuwa la kutisha. Au la kipumbavu kidogo. Hatutapata hasara? Hatutatumika vibaya?
Ingawa Mungu anataka tuishi kama wakopeshaji wenye ukarimu, pia anasema ni busara kutafuta uelekevu (Mathayo 10:16, NKJV).
Lakini kuelewa uwakili wa Kibiblia unaweza kusaidia kupunguza hofu hiyo pia.
Uwakili na madeni
Linapokuja swala la kukopesha, ni muhimu kukumbuka kwamba kila kitu tulicho nacho kinatoka kwa Mungu (1 Mambo ya Nyakati 29:14, Zaburi 50:10, Hagai 2:8). Na Yeye anaweza kwa urahisi kuziba pengo la kile tunachokopesha.
Uwakili wa Kibiblia maana yake ni kwamba tunasimamia kile tulichonacho (kama pesa zetu, muda, na rasilimali) kwa ajili ya Mungu.
Yesu anaweka hilo wazi katika Luka 16:1-8 alipoeleza mfano wa tajiri ambaye anamfuta kazi wakili wake wa pesa. Anamshitaki meneja huyo kwa “anatapanya mali zake” (NKJV).
Kabla ya wakili kuondoka, anazunguka kwa kila mtu ambaye anamdai bwana wake pesa na kupunguza madeni yao. Analenga kupata upendeleo wa wengine katika jamii ili asije akasahauliwa.
Katika mwisho, tajiri anamsifu wakili wake wa zamani kwa jinsi alivyo shugulika na wadeni.
Ni ajabu kumsifu msimamizi kutoka katika mtazamo wa kifedha. Lakini inasaidia tunapolitazama kusudi la pesa kupitia mtazamo wa Mungu.
Tim Mackie, PhD, profesa wa masomo ya Biblia na mkurugenzi wa ubunifu wa BibleProject, anashiriki hitimisho hili kutoka katika utafiti wake kuhusu mfano huu:
“Ingawa ni jambo lisilowezekana kwamba bwana halisi angemsifu mtumwa kwa kufanya hivi, hiki ndicho hasa ambacho Mungu angefanya kuwasifu watumishi wake kwa kutumia fedha zake ipasavyo. Ambayo sio kuzitumia kama suluhisho la mwisho, bali kuzitumia kama chombo cha kujenga mahusiano. Na kilicho muhimu zaidi ni mitandao ya mahusiano, na msaada, na huduma unayojenga.”1
Tunapojitazama kama mawakili wa Mungu, inaweza kutusaidia kukunjua mikono yetu tunapokopesha.
Lakini uwakili mzuri pia unaathiri jinsi tunavyoyachukulia madeni.
Mungu hutupa “kila kutoa kuliko kwema na kila kitolewacho kilcho kamili” (Yakobo 1:17, ESV). Yeye hutupa uwezo wa kupata pesa (Kumbukumbu la Torati 8:18). Na Yeye hutupa tu kile anachojua tunaweza kukisimamia vizuri (1 Wakorintho 10:13).
Tunapotaka kitu kinacho hitaji deni, hizo ni aya za Biblia zinazofaa kuzingatiwa.
Hebu tuangalie kanuni zaidi za Biblia kuhusu kukopa.
Kukopa na kulipa deni

Photo by Mikhail Nilov
Biblia inasema tulipe deni tunalodaiwa—na tufanye haraka. Pia inasema tusichukue deni isipokuwa tunajua tuna njia za kulilipa.
“Asiye haki hukopa wala halipi, Bali mwenye haki hufadhili, hukirimu” (Zaburi 37:21, NKJV).
“Wewe ukimwekea Mungu nadhiri, usikawie kuiondoa; kwa kuwa yeye hawi radhi na wapumbavu; basi uiondoe hiyo ulioiweka nadhiri. Ni afadhali usiweke nadhiri, Kuliko kuiweka usiiondoe” (Mhubiri 5:4-5, NKJV).
“Enenda ukayauze mafuta haya, uilipe deni yako; nayo yaliyosalia uyatumie wewe na watoto wako” (2 Wafalme 4:7, NKJV).
Tulijifunza hapo awali kwamba deni sio bora, kwa hiyo ni jambo la maana kwamba Mungu anatarajia watu wake walipe madeni bila kukawia:
“Usiache macho yako kupata usingizi, wala kope za macho yako kusinzia. Ujiponye kama paa na mkono wa mwindaji. Na kama ndege katika mkono wa mtega mitego” (Mithali 6:4-5, NKJV).
Dave Ramsey, Mkristo mtaalamu wa maswala ya fedha, anasema kuhusu deni, “Duma anaifuata familia yako. Kimbia! …Tunagundua kuwa watu hutoka kwenye deni wanapopata nguvu ya paa”.2
Kulipa deni haraka kunahusisha pia chochote tunachokopa. Hata kama inamaanisha kubadilisha kitu cha mtu mwingine ambacho tumekipoteza au kukiharibu (Kutoka 22:14, 2 Wafalme 6:5-7).
Lakini haimaanishi kwamba ikiwa tumezama katika deni au tumewahi kufilisika, tunapaswa kuishi kwa aibu. Tutaona baadaye kwamba Biblia inasema mengi kuhusu msamaha wa deni.
Kwanza, hata hivyo, tupate kanuni za kuishi ndani ya uwezo wetu.
Kile Biblia inachosema kuhusu kuishi ndani ya uwezo wetu
Mwisho wa siku: Maoni ya Biblia kuhusu kukopa pesa ni kwamba ni bora kuishi ndani ya uwezo wetu.
“Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia?” (Luka 14:28, NKJV).
“Kwani BWANA, Mungu wako, atakubarikia, kama alivyokuahidi; nawe utakopesha mataifa mengi, lakini hutakopa; …..” (Kumbukumbu la Torati 15:6, NKJV, msisitizo umeongezwa).
Lakini mara nyingine inaweza kuonekana kana kwamba haiwezekani, sivyo? Na mara nyingine tunakumbwa na matumizi yasiyotarajiwa na yanayoturudisha nyuma.
Lakini haijalishi tuko katika hali gani, Biblia inatupa changamoto kuridhika na tulivyonavyo (Waebrania 13:5, Wafilipi 4:11-13, Luka 12:15). Na inatupa maswali tunayoweza kujiuliza tunapojikuta tunavutwa kuchukua deni ambalo huenda halihitajiki, kama vile:
- Je, ni mapenzi ya Mungu? (Yakobo 4:15)
- Je, ni tamaa au ni hitaji? (1 Timotheo 6:6-8)
- Je, tunajaribu kuwapendeza watu? (Mhubiri 5:10)
- Je, tunaharakisha sana? (Mithali 21:5)
Je, kuhusu kulipa zaka? Je, tunaweza kusitisha wakati tunadaiwa ili tuishi kulingana na uwezo wetu?
Hatutagusia aya zote kuhusu zaka.3 Lakini katika Luka 21:3-4, Yesu anaonyesha kwamba anataka tutoe zaka, bila kujali hali yetu:
“Akasema, Hakika nawaambia, huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote; maana hao wote walitia sadakani katika mali iliyowazidi, bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo” (NKJV).
Aina ya mwisho ya deni tutakayoangalia inahusisha kusaini mkopo kwa ajili ya mtu mwingine (mdhamini).
Udhamini katika Mikopo

Photo by Scott Graham on Unsplash
Maneno mengi ya hekima yanatuonya dhidi ya aina hii ya makubaliano. Hii ni tofauti na kumkopesha rafiki aliye na uhitaji. Ni kuwajibika kisheria kwa deni la mtu mwingine.
“Aliyepungukiwa na akili hupana mkono na mtu; Na kuwa mdhamini mbele ya mwenzake” (Mithali 17:18, NKJV).
Na hapa kuna sababu ya ushauri huo:
- Inatufunga katika makubaliano ambayo hatuna udhibiti mzuri juu yake (Mithali 6:1-2).
- Ikiwa mdaiwa hatalipa, tunabaki na deni hilo (Mithali 22:26-27).
- Inaweza kutuweka katika hatari (Mithali 11:15).
Hivyo mithali hizi hazituambii tusisaidie au kukopesha, bali kuwa waangalifu kuhusu makubaliano ya kisheria ambayo yanaweza kukubebesha majukumu ya mtu mwingine.
Kusamehe na Kufuta madeni
Yesu alitumia mifano kuhusu kufuta madeni ya kifedha ili kuwakilisha msamaha wa dhambi. Na inatuonyesha kwamba Anatamani kutusaidia katika ustawi wetu wa kiroho na kifedha (Mathayo 18:23-35, Luka 7:41-43).
Katika Filemoni 1:18-19, Paulo anaandika barua nzuri kwa mtumwa ambaye alikimbia. Anamwambia bwana wa mtumwa huyo,
“Na kama amekudhulumu, au unamwia kitu, ukiandike hicho juu yangu. Mimi Paulo nimeandika kwa mkono wangu mwenyewe, mimi nitailipa” (NKJV).
Mtumwa pekee alikuwa anawajibika kwa deni lake. Paulo hakuwa mdhamini. Lakini anajitolea kulipa deni la mtumwa, kutupatia mfano wa kipekee wa kile Kristo Yesu alichofanya alipokufa kwa ajili yetu.
Na hilo bado linatokea leo.
Mtu mmoja alipambana na deni la mkopo wa wanafunzi kwa miaka minane. Kisha mfadhili asiyejulikana akalipa deni lote la $139,000 ambalo alikuwa amebaki nalo.
Visa kama hivyo vinatushangaza. Lakini katika Agano la Kale, Mungu alifanya msamaha wa deni kuwa mazoea ya kawaida:
Katika Mambo ya Walawi 25:10, Mungu alitenga kila mwaka wa 50 kuwa “kutangaza uhuru katika nchi” (NKJV). Katika huo, kila mtu alipata kile walichopoteza kupitia deni.
Na kila baada ya miaka saba, “Kila mkopeshaji na akiache alichomkopesha mwenziwe….” (Kumbukumbu la Torati 15:1-2, NKJV).
Lakini kuna zaidi.
Wakolosai 2:14 inazungumzia Yesu “akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake” (NKJV). Na katika Mathayo 6:12, anasema tuombe: “Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu” (NKJV).
Kusamehe deni ni kitu halisi ambacho wengi wanatamani na wanaweza kuelewa. Hivyo Biblia hutumia kufuta madeni kuelezea uzuri wa dhambi zilizosamehewa.
Na hilo linatupeleka kwenye swali lingine.
Je, ni sawa kuomba Mungu atusaidie kufuta madeni yetu ya kifedha?
Hebu tujadili hilo kabla hatujamaliza.
Kutemgemea Mungu dhidi ya deni
Tunajua kwamba Mungu haachi watu wake kushughulikia mambo peke yao. Yeye ndiye mkopeshaji wa mwisho (Zaburi 37:24-26, NKJV).
Tunaweza kwa ujasiri kumuomba Mungu msaada, hata tunapokuwa katika hali mbaya tuliyosababisha wenyewe (Waebrania 4:16,NKJV).
Mungu pia hutukumbusha kwamba ana vya kutosha kushughulikia mahitaji yetu yote (Wafilipi 4:19).
Mungu anaahidi kutusaidia tunapofanya kuwa desturi kuepuka deni na kumtegemea (Mathayo 6:31-33).
Anataka kutuweka katika hali ambapo hatulazimiki kukopa:
“Atakufunulia BWANA hazina yake nzuri, nayo ni mbingu, kwa kutoa mvua ya nchi yako kwa wakati wake, na kwa kubarikia kazi yote ya mikono wako; nawe utakopesha mataifa mengi, wala hutakopa wewe” (Kumbukumbu la Torati 28:12, ESV, mstari ulioongezwa).
Hivyo, ingawa mambo hayawezi kuwa mazuri kifedha sasa, tambua kwamba Mungu daima ana mpango kwa kila mmoja wetu.
Jinsi ya kutumia kanuni za Biblia kuhusu madeni leo

Photo by Kaboompics.com
Jumla ya yote, Biblia inahimiza kutoa kwa ukarimu na kukopa kwa tahadhari. Na ikiwa tunasumbuliwa na deni (au mojawapo ya changamoto kubwa za maisha), hatuhitaji kujisikia kama tumekwama mwisho wa barabara.
Vidokezo hivi vya kuhusu kuwa huru kutoka deni ni njia inayoweza kutusaidia kupata kasi.
Kwanza, Biblia inasema ni busara kuwa na washauri wanaotoa mwongozo uliojengwa katika Biblia (Mithali 11:14). Kwa hivyo ni vyema kutafuta programu za wataalamu wa fedha wa Kikristo kama:
Pia tunaweza kulazimika kufanya kazi ya ziada kwa muda. Lakini haitakiwi kuwa jambo la kuchosha.
Wakolosai 3:23 inatuambia kukumbuka tunayemfanyia kazi: “Fanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu” (NKJV).
Na hili linaweza kuonekana la kawaida, lakini mara kwa mara tunahitaji kukumbushwa kwamba tunaweza kuomba Mungu atuonyeshe njia. Kwa Kila Siku.
Kufuata kanuni za Biblia kuhusu deni la kifedha kunaweza kuturuhusu:
- Kuwa na uhuru wa kumfuata Mungu mahali ambapo anatuongoza
- Kuwa na mahusiano bora katika jamii
- Kuishi bila msongo wa mawazo
- Kuacha kazi zisizofaa kwa kazi tunayoipenda6
- Kumtukuza Mungu kwa kumruhusu atupatie mahitaji yetu
- Kuacha kulinganisha maisha yetu na ya wengine
- Kuwa watoaji wenye ukarimu
Na mengi zaidi.
Labda tayari unaishi maisha yasiyo na deni. Lakini kama bado hujafika huko, hiyo ni sawa. Mungu anaelewa hali ya kila mtu binafsi na anatupatia Roho Mtakatifu kuwa mwongozo wetu katika changamoto na maamuzi yote ya maisha.
Ungependa kujua zaidi?
Kurasa zinazohusiana
- “What Does Jesus Say About Money?” in BibleProject, hosted by John Collins and Tim Mackie, July 8, 2024, podcast, 22:27. [↵]
- “Dumping Debt: Freedom from Debt – Sermon by Dave Ramsey.” Christian.Sermons Daily. January 1, 2016. Video, 17:10:00. [↵]
- Leviticus 27:30-32, Deuteronomy 14:28-29, Proverbs 3:9, Malachi 3:8-10, Hebrews 7:4, Genesis 14:20, Genesis 28:22, Matthew 23:23, 2 Corinthians 8:5, Mark 12:41-44, 2 Chronicles 31:4-9 [↵]
- “Financial Peace University.” Ramsey Solutions, 2024. [↵]
- “About Us.” I was Broke. Now I’m Not. 2016. [↵]
- Coleman, Ken. 2021. From Paycheck to Purpose. Ramsey Press. [↵]
Majibu Zaidi
Hadithi za Uponyaji Katika Biblia na Maana Yake Kwako
Umewahi kuhisi kana kwamba isingewezekana kwako kuponywa? Kweli, kuna visa vya watu wanaoshinda changamoto zilizoshindikana au kupata uponyaji wa kimiujiza wa afya zao.




