Mazishi mengi ya Waadventista wa Sabato yanafanana na yale ya madhehebu mengine ya Kiprotestanti, kama vile Wamethodisti, Wabatisti, au Wapresbiteri, lakini unaweza kupata tofauti chache au taratibu za pekee.
Waadventista wanachukulia kifo kuwa matokeo ya kuhuzunisha ya dhambi. Ni wakati wa kuomboleza na kutambua udhaifu wa maisha, na inapaswa kuheshimiwa kwa kiasi kinachofaa cha heshima ya kusikitisha kwa wale wanaoathiriwa.
Daima ni ngumu kukabiliana na kifo, iwe tunafikiria kuhusu wapendwa wetu wenyewe au ya mtu tunayemjali.
Waadventista pia wanatazamia kwa imani ufufuo wakati wa Kuja Mara ya Pili kwa Kristo, wakijua kwamba ufufuo na uzima wa milele pamoja na Yesu ni baraka ya kutazamia. Ingawa tunatambua kwamba kifo ni tukio la kusikitisha, kuna kiwango cha faraja na amani tunachoweza kushikilia kama waamini, tukijua tutakutana tena wakati wa kurudi kwa Yesu.
Hebu tuangalie kwa karibu zaidi imani hizi, na jinsi washiriki wa Kanisa la Waadventista wa Sabato wanavyoziishi.
- Wanavyoamini Waadventista kuhusu kifo
- Mazoea ya mazishi ya kawaida ya Kiadventista
- Mazoea ya mazishi ya kawaida
- Jinsi Waadventista wanavyo wasaidia waliofiwa
Tuanze kwa kutazama msingi wa maandiko kuhusu jinsi tunavyochukulia kifo.
Waadventista wanaamini nini kuhusu kifo

Photo by Sandy Millar on Unsplash
Unaweza kusoma ukurasa rasmi wa Imani ya Msingi kuhusu mada hii, lakini hapa kuna muhtasari.
Waadventista Wasabato wanaamini kwamba wakati mtu anapokufa, mwili wake unaoza (Mwanzo 3:19) kwani hawana tena “pumzi ya uhai” (Mwanzo 2:7) ndani yao. Na wakati pumzi hii ya uhai inamrudia Mungu, ni kana kwamba mtu huyo yuko katika hali ya kutokujitambua. Kama usingizi, hawana ufahamu wa chochote.
“Kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa” (Mhubiri 9:5, NKJV).
Hakuna sehemu ya mtu aliyekufa inayofanya kazi au kuwa na ufahamu—sio mwili, wala roho au nafsi. Hawapo katika ulimwengu wa roho ambao unaweza kuwasiliana na ndugu zao walio hai.
Wafu hawatajua chochote mpaka Yesu Kristo arudi wakati wa Kurudi Kwake mara ya Pili na kuwafufua kwa uzima wa milele.
Kwa sababu tunaamini hivi, hatuamini mtu yeyote anakwenda moja kwa moja mbinguni au kuzimu mara baada ya kufa. Kwa hivyo desturi zetu zinazohusiana na kifo hazizungumzii au kurejelea kifo kama hatua ya kuingia mbinguni au kuzimu. Tunawatambua waliokufa kama wanao “pumzika” kaburini.
Kwa sababu wako katika pumziko, mazishi ya Waadventista mara nyingi huwa na kivuli cha matumaini, licha ya huzuni kuwa kitu cha kawaida na cha afya kuambatana na kufiwa (Mhubiri 3:4). Lakini imani yetu inatukumbusha kwamba Kristo alishinda kifo na aliahidi atarudi kutuchukua sote kwenda mbinguni, akishinda kifo milele (1 Wakorintho 15:19-26).
Kitu cha kwanza ambacho mtu aliyekufa atakiona ni Yesu akirudi.
Kwa kuzingatia imani hii, hebu tuangalie baadhi ya desturi za mazishi ya Waadventista.
Desturi za mazishi ya Kiadventista
Kwa kauli rasmi, Waadventista hawashikilii aina moja maalum ya mazishi. Tunafuata kile ambacho wakristo wengi hufanya na kuzika au kuchoma wale waliokufa.
Kuzika wafu ilikuwa desturi ya Kiyahudi (1 Wafalme 2:10, 1 Wafalme 15:24, 2 Wafalme 20:21) ambayo iliendelezwa katika Ukristo.1
Kuchoma maiti pia ni jambo la kawaida na linaweza kufaa kwa sababu nyingi. Ingawa Biblia haitaji moja kwa moja, inatupa mfano wa wakati kuchoma ilipotumiwa. Katika 1 Samweli, tunasoma kuhusu vifo vya Mfalme Sauli na wanawe wakati wa vita.
Waisraeli wengi kufikia wakati huo walikuwa wamechoshwa na Sauli na walitamani sana Daudi awe mfalme. Lakini watu wa Yabesh-Gileadi, ambao Sauli aliwahi kuwaokoa, walimkumbuka kwa wema (1 Samweli 11). Kwa heshima, “wakautwaa mwili wake Sauli na miili ya wanawe, na kuiondoa ukutani kwa Beth-Shani; nao wakaja Yabeshi, na kuiteketeza huko. Kisha wakaitwaa mifupa yao, na kuizika chini ya mkwaju huko Yabeshi, nao wakafunga siku saba” (1 Samweli 31:12-13, NKJV).
Miili hii labda ilikuwa imeharibiwa na haikuwa ya kupendeza kuangalia, na kuwachoma ilikuwa ishara ya heshima.
Kulingana na imani zetu, mchakato wa mazishi kwa kiasi kikubwa unatokana na sababu za vitendo na za kihisia. Ingawa kunaweza kuwa na maana ya ishara ndani ya mila za mazishi, hakuna umuhimu wa kudumu kwa mtu aliyefariki na haitaleta tofauti katika jinsi matukio ya ufufuo yanavyotokea.
Kwa namna yoyote ile marehemu alivyozikwa, bado atafufuliwa na kupewa uzima Yesu atakaporudi. Hivyo, Waadventista huacha uamuzi wa mazishi au kuchoma uwe chini ya watu binafsi na familia zao.
Mtazamo huu pia unaelezea sababu nyingi za mazishi ya Waadventista kuchukuliwa kuwa ya kiasi na yenye uhalisia, mara chache maonyesho ghali au ya kifahari hupewa kipaumbele. Kwa ujumla, tunapendelea zaidi kuzingatia kuwasaidia na kuwafariji wale wanaoomboleza.
Desturi za mazishi zinazofanywa mara kwa mara katika jamii za Waadventista.
Kawaida, wakati mtu anapofariki, familia ya karibu huchukua hatua ya kuandaa mazishi. Kulingana na hali, ibada ya mazishi inaweza kufanyika kati ya siku chache au wiki kadhaa baada ya kifo.
Ni kawaida kwa Waadventista kuepuka kufanya mazishi siku ya Sabato, hasa kwa sababu inahusisha kiasi kikubwa cha kazi, mipango, safari, na malazi. Siku ya Sabato, Waadventista wanafanya pumziko kutoka shughuli za kila siku kuwa kipaumbele na kuzingatia kutumia muda na Mungu.
Kusherekea Maisha
Jamii nyingi za Waadventista pia hufanya “sherehe ya maisha” au ibada ya kumbukumbu, iwe kama nyongeza kwa mazishi rasmi au badala yake. Hizi zinaweza kufanyika hadi miezi kadhaa baada ya kifo cha mtu.
Kwa ujumla, ibada hizi huchukua nafasi ya mazishi ikiwa mwili ulichomwa au mazishi yanapaswa kucheleweshwa zaidi ya wakati unaofaa kwa kuzikwa.
Au katika kesi ya jamii kubwa za Waadventista, familia inaweza kufanya ibada ndogo ya kaburini kwa marafiki na familia karibu, na ibada ya kumbukumbu baadaye ili kuwajumuisha wengine katika kukumbuka kwa upendo mpendwa wao.
Kutazama maiti
Siku moja kabla au siku ya mazishi, Waadventista wanaweza kukutana ili kuona mwili, au kipindi cha muda (kawaida masaa machache) ambapo marafiki na familia wanaweza kuja nyumbani kwa mazishi au kanisani na kuzungumza na jamaa wa marehemu. Huenda hii ikawa ni fursa ya kuona mwili wazi, au familia inaweza kuonyesha picha marehemu.
Mazishi

Photo by The Good Funeral Guide on Unsplash
Mazishi kawaida hufanyika kanisani au nyumbani kwa waliofiwa. Watu wanaohudhuria wanaweza kuvaa nguo nyeusi za kawaida au hakuna vito, kutokana na imani zetu kuhusu mavazi. Ibada mara nyingi hujumuisha muziki, maombi, kusoma kwa kumbukumbu ya marehemu, kusoma maandiko matakatifu, maneno machache na baraka, kutoka kwa mchungaji.
Mahubiri ya mchungaji yanaweza kuelekezwa kwenye tumaini tulilonalo katika Mungu na mpango wake, kwa sababu Wadventista wote wanatazamia siku ambayo Yesu atarudi wakati wa Kurudi Kwake mara ya Pili, na tutawaona tena wapendwa wetu mbinguni. Ibada nzima huwa na hisia za tumaini, badala ya huzuni kuu, ingawa tukio hilo halikosi huzuni.
Huduma huwa haichukui muda mrefu – dakika 30 hivi, ingawa inaweza kutegemea idadi ya watu wanaoshiriki kumbukumbu.
Ikiwa familia itachagua kuwa na huduma ya kaburini, kila mtu ataelekea kwenye kaburi, ambapo mchungaji mara nyingi huwa na huduma fupi ya kaburini. Washiriki wataweka maua juu ya jeneza, na litashushwa ardhini.
Katika baadhi ya matukio, familia inaweza kutoa chakula baada ya huduma ya mazishi kwa wageni.
Ingawa hii ni ramani ya jumla ya mazishi ya Mwadventista, kuna mabadiliko mengi unayoweza kutarajia kuona. Inategemea mapendeleo ya familia na maombi ya mtu binafsi, mradi isipingane na imani rasmi za kanisa.
Pia inatofautiana sana kulingana na eneo la ulimwengu unapoishi. Tamaduni zote zina mila zao ndani ya Uadventista, na ni muhimu kukumbuka kwamba huenda zisionakane kabisa kama tuliyoelezea.
Mazishi ni wakati wa huzuni, na Waadventista wanatafuta kutoa faraja kwa wapendwa wanaolia. Hebu tuongee kuhusu hilo.
Jinsi Waadventista wanavyo wasaidia waliofiwa
Mazishi ni wakati mgumu kwa wapendwa, ambao hubeba huzuni na mara nyingi mzigo wa kifedha pia.
Wakati mwingine, familia ya marehemu hupendelea kuomboleza kwa faragha, na matakwa yao yanapaswa kuheshimiwa. Lakini kwa kadiri inavyowezekana, Waadventista wanajaribu kuwasaidia marafiki zao wakati huu wa huzuni. Wanaweza kutuma maua au zawadi kwenye nyumba ya familia, ili kuwajulisha wanawawazia mema na kuwaombea.
Nyakati nyingine, washiriki wa kanisa wanaweza kupeleka chakula kwa familia. Mazishi huhusisha mipango mingi, na wakati mwingine jambo la mwisho ambalo wafiwa wanataka kufikiria ni kuamua watakula nini, au watahudumia vipi wale wanaozuru kutoka nje ya mji. Inaweza kuwa mzigo wa ziada kupanga na kuandaa milo hiyo, hivyo familia ya kanisa mahalia hujaribu kusaidia kadiri wawezavyo.
Kutembelea washiriki wanao-omboleza kunaweza pia kuthaminiwa, ikiwa watafanya hivyo. Nyakati nyingine washiriki wa familia walio na huzuni huhitaji mtu wa kuzungumza naye kwa sababu mbalimbali: kuondoa mawazo yao juu ya huzuni yao, kuwa na rafiki wa kuzungumza naye kuhusu maandalizi, au kuwa na mtu wa kuwafariji na kuwatuliza katika wakati huzuni na mashaka yanapozidi.
Jambo muhimu unaloweza kufanya Mwadventista unayemjua amepoteza mwanafamilia ni kufanya bidii yako kuelewa mahitaji yao binafsi yanaweza kuwa nini, na jaribu kuwasaidia kulingana na mahitaji hayo. Tafuta njia za kuwaonyesha kwa dhati kwamba unawajali.
Kifo cha mpendwa ni jambo gumu sana kushughulika nalo, hata kwa Wakristo kama Waadventista ambao tunajua tutawaona wanafamilia wetu wa Kikristo baada ya ufufuo.
Huku tukihakikisha kwamba hatupuuzi huzuni hii ya muda tunayopitia baada ya kupoteza, tunatambua kwamba ni muhimu kushikilia tumaini hilo ambalo Yesu anatupa, hata katika majaribu yetu makali. Aliahidi kamwe hatutupi au kutuacha (Waebrania 13:5).
Na, jambo bora zaidi ni kwamba, Yeye ameahidi kwamba hisia mbaya hizi watu wanazopitia sasa zitakoma siku moja. Yesu atakaporudi,
“. . . Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena, kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita” (Ufunuo 21:4, NKJV).
Huzuni yetu na maumivu hayatakuwapo milele! Tutawaona wapendwa wetu siku moja, siku ambayo kifo kitatoweshwa milele. Hili ndilo tumaini ambalo Waadventista wanashikilia.
Ikiwa ungependa kujifunza zaidi kile Biblia inasema kuhusu wakati huu wa maombolezo,
Kurasa Zinazohusiana
- Reid, George W, “Cremation,” Adventist Biblical Research.org, General Conference of Seventh-day Adventists, https://www.adventistbiblicalresearch.org/materials/cremation/. [↵]
Majibu Zaidi
Filamu za Kiadventista: Mahali Imani na Filamu Zinapokutana
Tangu mwanzo, lengo la Kanisa la Waadventista wa Sabato limekuwa kueneza kweli ya Mungu katika Biblia.
Ni nini Mtaalam wa Matibabu wa Kiadventista?
Mmishonari wa matibabu katika Kanisa la Waadventista ni mtu anayejali mahitaji ya matibabu ya watu kama njia ya kuonyesha upendo wa Yesu.
Je, Waadventista Wasabato Wanasherehekea Siku Kuu Zinazohusiana na Pasaka?
Kufufuka kwa Yesu, kunakoadhimishwa katika siku kuu nyingi zinazohusiana na Pasaka, ni muhimu katika imani za Kanisa la Waadventista wa Sabato.
Chakula cha Pamoja Katika Kanisa la Kiadventista: Mahali Ambapo Chakula na Urafiki Vinakutana
Mara nyingi, kawaida kwenye ratiba inayotofautiana kutoka mara moja kwa wiki hadi mara moja kwa mwezi hadi mara moja kwa robo, kanisa la Waadventista litakuwa na “karamu za ushirika,” mara nyingi zikiitwa chakula cha mchana cha pamoja.
Je, Mahubiri ya Waadventista wa Sabato Yako Namna Gani?
Karibu katika kila Kanisa la Waadventista wa Sabato, mahubiri ndiyo kitovu cha ibada kuu—kama ilivyo kwa madhehebu mengi ya Kikristo ya Kiprotestanti.
Wasimamizi wa Waumini Wana Nafasi Gani Ikilinganshwa na Wachungaji?
Neno “Usimamizi wa kidini” linatokana na neno la Kigiriki laikos, ambalo maana yake ni “wa watu.”
Muundo wa Uongozi wa Kanisa la Waadventista wa Sabato.
Kanisa la Waadventista wa Sabato lina mfumo wa uwakilishi unaounganisha makanisa yake zaidi ya 90,000 ulimwenguni na kuwapa washiriki wake nafasi katika kufanya maamuzi.
Kitabu cha Nyimbo cha Waadventista Wa Sabato
Kitabu cha nyimbo cha Waadventista wa Sabato ni kitabu cha nyimbo kinachotumiwa ulimwenguni kote na makanisa mengi ya Waadventista wakati wa ibada zao.












