Kwa Nini kuna Wema na Uovu Duniani?

Asili ya binadamu inaweza kufanya matendo ya kujitoa mhanga na ya shujaa zaidi—askari akitoa maisha yake kwa ajili ya nchi yake, mama kulinda watoto wake dhidi ya madhara, mtu kuruka ndani ya maji mengi yaendayo kasi kwa ajili kumwokoa mtu anayezama.

Vivyo hivyo, watu pia hufanya baadhi ya matendo ya ubinafsi na ya kikatili zaidi—uhalifu wa kivita, mauaji ya kikabila, ubakaji, unyanyasaji.

Kwa nini ulimwengu wetu una mgongano huu kati ya wema na uovu?

Dunia yetu ilianza ikiwa kamili na isiyo na dhambi, lakini Biblia inatuambia kuhusu kisa cha malaika mwenye kiburi ambaye aliamua kupinga kanuni ya Mungu ya kujitoa kwa upendo na kuleta ubinafsi katika ulimwengu wetu. Aliwajaribu wanadamu wa kwanza kuwa na mashaka juu ya wema wa Mungu na kuchagua maarifa ya uovu.

Tangu wakati huo, mapambano kati ya wema na uovu yameendelea.

Kwenye ukurasa huu, tutachunguza kile Biblia inachosema kuhusu tatizo hili la uovu na suluhisho lake.

Tutachunguza:

Hebu tuanze.

Wema ni nini, na uovu ni nini?

As the world feels like it's getting darker, the Bible opens to us the light of God's love and sin's darkness.

Photo by Aaron Burden on Unsplash

Wema unahusu kuwa na maadili bora. Mtu anayesaidia wahitaji na kukuza ustawi wa jamii huchukuliwa kuwa mwema.

Kwa upande mwingine, uovu humaanisha kutokuwa na maadili au uasi —ambao hupelekea bahati mbaya au mateso. Kwa mfano, wengi wangesema Hitler alikuwa mtu mwovu kwa ukatili wake.

Tofauti kati ya wema na uovu—na jinsi nguvu hizo mbili zinavyofanya kazi—ni somo ambalo limechanganya wengi.

Wataalam wa theolojia, wanafalsafa, na hata wanasayansi wamejaribu kueleza mambo haya mawili- uwepo wa wema na uovu duniani na ndani yetu.

Hapa kuna baadhi ya mitazamo yao:

  • Mtakatifu Agusto wa Hippo alielezea uovu kama “wema ulioharibika” unaotokea wakati wanadamu wanapochagua “jema dogo.”
  • Thomas Aquinas aliona uovu kama ukosefu wa wema na aliamini kuwa athari yake ni kubwa.
  • Katika Ubudha, wema na uovu sio vitu vinavyopingana. Badala yake, ni sifa zinazohusiana zilizopo ndani yetu kwenye wigo, na tunaweza kukuza wema kuliko uovu.
  • C.S. Lewis, mhubiri wa Kikristo wa karne ya 20, aliona uovu kama wema ulioharibika ambao unawezekana kutokana na nia huru ya mwanadamu.1
  • Wanabaiolojia wa uibukaji wanaamini kwamba wema na uovu una asili yake katika ubinafs. Hata matendo yanayoweza kusaidia wengine na kuonekana kuwa sio ya kibinafsi ni njia zilizojificha za kujitazama wenyewe.

Waadventista pia wameangalia mada hii na kuielewa kulingana na mafundisho ya Biblia kuhusu hilo.

Hebu tuangalie hilo.

Ni nini mtazamo wa Biblia kuhusu wema na uovu?

Biblia inakiri uwepo wa wema na uovu. Wema unatokana na Mungu mwenyewe —upendo usio na ubinafsi. Uovu, kwa upande mwingine, ni tofauti na Yeye na tabia Yake. Ulianza kutokana na uamuzi wa kiumbe kugeuka mbali na wema wa Mungu.

Hapa kuna zaidi kuhusu asili ya wema na uovu.

Mungu ndiye chanzo cha wema wote

Biblia inatuambia kwamba kila kitu kilianza kuwa “chema sana” (Mwanzo 1:31, UV030)—na kwamba Mungu aliumba kila kitu kwa ukamilifu.

Mungu Mwenyewe ni mwema. Hivyo kila kitu anachofanya au kuumba pia ni chema.

Biblia pia inasema, “Mungu ni upendo” (1 Yohana 4:8, UV030).

Basi, Mungu ni mkamilifu na mwenye upendo. Yeye ni mwenye haki, mwenye rehema, na mwenye fadhili. Yeye hufanya kazi kwa kanuni ya unyenyekevu na upendo usio na ubinafsi.

Mungu alijua tungejitahidi kuelewa maana ya kuwa wema, hivyo anafunua wema wake kupitia Biblia.

Amri Kumi, zilizotolewa kwetu na Mungu, ni chanzo muhimu kwa hili. Badala ya kuwa orodha ya mambo ya kufanya na kutofanya, zinaelezea tabia Yake na maana ya kuwa mwema—yaani kumpenda Mungu na watu.

Silhouette of a man gazing at stars as we learn about God who revealed His character of love and grace to Moses.

Photo by Greg Rakozy on Unsplash

Lakini sio Amri Kumi tu zinazoonyesha wema. Katika Biblia nzima, Mungu hutufundisha jinsi ya kupenda kama yeye anavyopenda. Na tunaposhindwa, kama sote tunavyofanya, Yeye hutuambia atazidi kutupenda na kutuongoza.

Tunapata mifano zaidi ya wema katika Biblia, kama tabia zinazostahili kutafutwa na kukuzwa na namna bora zaidi ya kuishi katika uhai wetu.

Kwa msaada wa Roho Mtakatifu, tunaweza kuwa na matunda ya Roho: “Upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi” (Wagalatia 5:22-23, UV030).

Lakini kujua lililo jema na kuwa mwema ni mambo tofauti kabisa, kama alivyo bainisha Paulo:

“Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati, Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo” (Warumi 7:18-19, UV030).

Kwa hiyo, uovu unaotushawishi tusitende mema ni nini?

Uovu ni nguvu inayopingana na Mungu

Uovu ni kutokuwepo kwa wema na unatokana na ubinafsi. Ni matokeo ya kuchagua kuishi mbali na Mungu, chanzo cha wema wote.

Kama Muumbaji, Mungu aliwaumba wanadamu wakiwa na uwezo wa kupenda.

Lakini hakutufanya kuwa roboti. Badala yake, Mungu alitupa akili na uwezo wa akili wa kuchagua ni nani wa kumpenda, na Yeye hufanya kazi kwa bidii kutunza uhuru wetu wa kuchagua. Hapo ndipo upendo wetu unapokuwa halisi – tunapokuwa na uwezo wa kuchagua kupenda.

Tunapokuwa na uwezo wa kuchagua, Mungu anaelewa kwamba tunaweza kufanya uchaguzi mwingine, ambao sio Yeye na sio uchaguzi mwema. Tunaweza kuchagua kuishi maisha ya utumishi, yanayolingana na upendo Wake, au tunaweza kuchagua maisha kwa ajili yetu wenyewe—yale ya kibinafsi ambayo mwishowe ni kutoridhika na uharibifu.

Lakini kabla hatujachagua, tunahitaji kuelewa hadithi nzima.

Kwa nini kuna uovu? Hata hivyo uovu ulitoka wapi?

Sio kutoka kwa Mungu, kama tutakavyoona (Yakobo 1:13–15).

Uovu ulianzaje?

Uovu ulizaliwa wakati malaika aliyeitwa Lusifa alipokuwa na wivu dhidi ya Mungu. Ingawa Lusifa alionekana kuwa na kila kitu kama malaika mzuri na mwenye nguvu mbinguni, alitaka zaidi (Ezekieli 28:13–15).

Hakutaka kumwabudu Mungu.

Alitaka kuwa Mungu (Isaya 14:12-14).

Hivyo katika ukamilifu wa mbinguni, upande unaopingana na uovu ulitokea. Lusifa alichagua maisha yenye kujifikiria mwenyewe na kugeuka dhidi ya Mungu na maisha yake kamili mbinguni.

Alifanya uchochezi miongoni mwa malaika na kuleta mashaka akilini mwao na kuwaongoza kuhoji mamlaka na upendo wa Mungu.

Kwa hivyo, alianza uasi dhidi ya Mungu na wote waliokuwa waaminifu kwake.

Hatimaye, Lusifa na theluthi moja ya malaika aliowashawishi walifukuzwa kutoka mbinguni na kutupwa chini duniani (Ufunuo 12:4, 7-8).

Ndipo Lucifer akajulikana kama Shetani, Ibilisi, na “mtawala” wa dunia. Akaanza kazi yake ya kuwapotosha na kuwafanya watu duniani kuwa na mashaka kuhusu Mungu pia (Ufunuo 12:9).

Na kazi yake ya udanganyifu inaendelea hata leo.

Upinzani wa Shetani mara kwa mara katika uumbaji kamili wa Mungu husababisha mapambano tunayopitia kila.

Mgogoro unaojulikana kwa Waadventista kama Pambano kuu—vita vilivyoanza mbinguni na vimeendelea ulimwenguni mwetu vizazi na vizazi.

Ni nini matokeo ya uovu?

Eve plucking forbidden fruit from the tree of the knowledge of good & evil when Satan deceived her with his lie.

Photo by Georgia de Lotz on Unsplash

Wakati uovu ulipoingia ulimwenguni mwetu, ulitutenganisha na Mungu na kusababisha mwanya kati ya wanadamu wa kwanza. Maumivu, mateso, na ugumu vikawa sehemu ya kawaida ya maisha.

Lakini jinsi gani uovu uliifikia familia ya wanadamu?

Wakati Shetani alipotupwa duniani, alikuwa na shauku kubwa ya kumpinga Mungu kwa kila njia inayowezekana. Alianza kuharibu uumbaji wa Mungu.

Aliingia Bustani ya Edeni ambapo Adamu na Hawa—wanadamu wa kwanza—walikuwa wakiishi.

Mungu alikuwa ameumba Bustani iwe nyumbani kwa Adamu na Hawa milele, akawapa kila kitu walichohitaji ili kuishi—maji safi, mimea kwa ajili ya kula, wanyama wa kwa ajili ya kutunza, na, la muhimu zaidi, uwepo wa Mungu.

Haya yote yalikuja na muundo. Unaweza hata kuziita “sheria”.

Lakini sheria hizi hazikuwekwa ili kuwazuia. Mungu aliweka sheria hizo ili kuwalinda Adamu na Hawa wasifanye maamuzi ambayo yangewadhuru.

Walikuwa na uwezo wa kutawala Bustani nzima, isipokuwa “walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile” (Mwanzo 2:17, UV030). Mungu aliwaagiza wasile kutoka kwenye mti huo kwa sababu kama wangefanya hivyo, wangekufa.

Lakini Shetani alikuja na kumdanganya Hawa, akisema:

“Hakika hamtakufa, kwa maana Mungu anajua ya kuwa siku mtakapokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya” (Mwanzo 3:4–5, UV030).

Uongo ulikuwa kwamba hangekufa.

Lakini alifunika hilo kwa ukweli—kwamba angejua mema na mabaya. Na ukweli huo uliambatana na kauli kwamba angekuwa “kama Mungu,” jambo linalovutia.

Kwa kuamini uongo, Hawa na mumewe Adamu walikula tunda lililokatazwa (Mwanzo 3:6). Hapo ndipo walipoelewa uovu, ambao hawakujua awali. Macho yao yalifunguka lakini sio kwa kitu chochote walichotaka kuona au kupitia.

Mpaka wakati huo, walikuwa wanajua mema tu. Lakini kupitia majaribu ya Shetani, Adamu na Hawa wakajua upande mwingine—uovu:

“BWANA Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya.” (Mwanzo 3:22, UV030).

Ingawa Adam na Hawa hawakufa wakati huo, walifungua mlango kwa kifo kuingia duniani. Tofauti na mpango wa awali wa Mungu kwa mwanadamu, wao na vizazi vyao vya baadaye wangeishi, na kisha kufa.

Uovu pia ulileta matokeo machungu yafuatayo:

  • Mafarakano na Mungu na aibu inayowafanya wanadamu kutaka kujificha kutoka kwa Mungu (Mwanzo 3:7–11)
  • Kupoteza haki ya Bustani ya Edeni na Mti wa Uzima (Mwanzo 3:23–24)
  • Maumivu wakati wa kujifungua (Mwanzo 3:16)
  • Uchovu unaotokana na kazi (Mwanzo 3:17–19)
  • Mahusiano yaliyo haribika na vikwazo zaidi katika kuwa na mahusiano yenye furaha (Mwanzo 3:16)
  • Mwelekeo wa kutenda dhambi (Warumi 7:15–20)
  • Kifo (Mwanzo 3:19)

Hayo—na mengine mengi—ndiyo tunayoendelea kupambana nayo.

Jambo la kushukuru ni kwamba, Mungu ana mpango ili tusipambane nayo milele.

Suluhisho la uovu katika ulimwengu huu ni nini?

Silhouette of Jesus Christ with a crown of thorns on His head as He came to conquer evil

Photo by Rodolfo Clix

Kwa kuwa uovu unaleta kifo, na tusingeweza kujiokoa kutokana na tabia yetu ya kuuelekea uovu(mwelekeo wa kwenda kinyume na sheria ya upendo ya Mungu), Mungu alikuja na mpango wa kutuokoa—Alimtuma Yesu. Yesu Kristo, Mwana wa Mungu kwa ajili yetu na kuchukua hatima yetu ya dhambi juu Yake mwenyewe.

Tazama, Mungu anajua kwamba tunapofanya uamuzi dhidi yake na kupitia matokeo yake, tunakuwa vipofu kiasi cha kushindwa kuona upendo wake na tunakuwa wagumu katika uasi wetu dhidi yake. Hatuwezi kuwa na upendo kamili au wema bila msaada wake (Warumi 3:22–24).

Hivyo akapata njia ya kuonyesha upendo wake kwetu na kuturejesha kwake. Mpango wa kutuokoa kutokana na nafsi zetu – ikiwa tutamchagua Yeye.

Ili kutimiza hilo, Alimtuma Yesu.

Biblia inatuambia, “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” (Yohana 3:16, UV030).

Yesu alikuja duniani kuishi kama mwanadamu. Aliacha kila kitu kilichomfanya awe mungu na kwa maombi aliendelea kuwa na uhusiano na Baba yake Mungu.

Alizaliwa kama mwanadamu, akaishi maisha ya taabu na umaskini, na kufa mbadala wetu, akibeba matokeo ya dhambi—kifo (Warumi 6:23).

Hata hivyo, Alifufuka. Na kwa njia ya ufufuo wake, tunaweza kuishi tena.

Kwa sababu yeye alikuwa mwanadamu pekee aliyeishi duniani bila dhambi, yeye ndiye pekee aliyeweza kuchukua dhambi zetu, kufa mbadala wetu, na kuweza kufufuka (1 Yohana 3:5). Kifo kisingeweza kumshikilia.

Kwa kukubali kafara yake kama zawadi, dhambi zetu zinafunikwa. Hatuhitaji kufa tena (1 Timotheo 2:5-6).

Hili ndilo tumaini la Wakristo —hatujaachiwa kupambana peke yetu, hata kama sisi ni watu waovu zaidi.

Kifo cha Yesu pia kinatupa wazo dhahiri la uchaguzi wetu kati ya wema na uovu. Kafara yake ilionyesha jinsi upendo ulivyo na kudhihirisha mapambano kati ya upendo na nafsi, mema na mabaya.

Na unatupatia uwezo wa kuchagua kati ya wema na uovu.

Tunapofanya uamuzi wa kuwa sehemu ya mpango wa Mungu, tuna hakika ya kujua kuwa tunashiriki kitu kikubwa zaidi kuliko sisi wenyewe. Maisha ni ya thamani kwa sababu ya tumaini la maisha ya milele yenye furaha pamoja na Mungu siku moja (Yohana 14:2–3).

Siku ambayo uovu utaangamizwa.

Kutakuwa na mwisho wa uovu

Maisha tunayopaswa kuishi—yenye mvutano kati ya wema na uovu—ni matokeo ya wanadamu wa kwanza kutaka kuona wenyewe jinsi wema na uovu unavyoonekana. Sasa, tunakabiliwa na uchaguzi kati ya nguvu hizi zinazopingana kila siku.

Lakini hatutalazimika kupambana na tatizo la uovu milele. Kutakuwa na wakati ambapo uso wote wa uovu utafunuliwa kabisa. Wale wetu wanaomfuata Yesu wataponywa, na tukiwa na ufahamu wetu kuhusu kilichotokea duniani hapa, kamwe hatutageuka tena kuelekea uovu.

Zaidi ya hayo, muda wa Shetani utakuwa umekwisha. Ataangamizwa (Ufunuo 20:7–10).

Na wanadamu, kwa hiari yao wenyewe, watachagua kumpenda Kristo na kuishi naye milele katika ukamilifu na amani (Ufunuo 21:4).

Ili kujifunza zaidi kuhusu mpango wa Mungu wa kutuokoa kutoka kwa uovu,

Vitu vya Kukumbuka

  • Mungu hakuumba uovu. Uovu ulitokana na moyo wa ubinafsi wa Lusifa (Yohana 8:44).
  • Dhambi, au uovu, ni uvunjaji wa sheria ya Mungu ya upendo (1 Yohana 3:4; Mathayo 22:37–40).
  • Mungu anaupenda ulimwengu wote wala hataki mtu yeyote apate matokeo ya uovu—kifo (Yohana 3:16).
  • Njia pekee ya kuondoa dhambi na uovu katika maisha yetu ni kumwamini Yesu na kumwomba atutakase (Isaya 1:16–19).
  • Tukiziungama dhambi zetu, Mungu atatusamehe na kutusaidia kushinda uovu katika maisha yetu (1 Yohana 1:9).
  • Tukiendeleza uhusiano na Yesu na kuishi ndani ya mipaka ya uhusiano huo, Yeye hutulinde tusianguke tena katika uovu na dhambi (Yohana 14:15; Yuda 1:24).
  • Uovu utaharibiwa mwishoni, na hautatokea tena kamwe (Nahumu 1:9).

Chagua Masomo ya Biblia Mtandaoni

Unataka kuendelea kujifunza? Pata habari zaidi kuhusu Yesu, mwanadamu, mpango wa wokovu, na jinsi Mungu anavyokupenda kiasi cha kutosha kujitolea kila kitu, ili tu kukupatia nafasi ya kumchagua.

Wakati mwingine inaweza kuwa ngumu kujua pa kuanzia, ndio maana tunatoa chaguo za masomo ya Biblia mtandaoni bure, rahisi kutumia, unaweza kufanya wakati wowote, mahali popote, na kwa kasi yako mwenyewe.

Shule hii ya Biblia mtandaoni itakuelekeza kupitia mada kuu za Maandiko, ikivunja dhana ngumu za Biblia katika vipande vidogo, ambavyo vinaweza kukusaidia kupata majibu ya maswali magumu zaidi ya maisha.

Kurasa zinazohusiana

  1. Arn, Jackson, Mere Christianity, Book 2 (HarperCollins Publishers, 1952), pp. 29–31. []

Je, Una swali kuhusu Waadventista? Uliza hapa!

Pata majibu kwa maswali yako kuhusu Waadventista Wasabato

Majibu Zaidi

Kila Kitu Kuhusu Agano la Kale na Jipya katika Biblia

Kila Kitu Kuhusu Agano la Kale na Jipya katika Biblia

Kila Kitu Kuhusu Agano la Kale na Jipya katika Biblia“Agano" ni mada iliyoenea kote katika Biblia. Wakristo mara nyingi hutofautisha agano la kale na jipya wanapoyazungumzia, lakini kwa kweli, Maandiko yanarejelea hatua au kufanywa upya tofauti wa agano moja. Ndiyo...