Huenda ukawa na rafiki wa Kiadventista ambaye anatumia vyakula vinavyotokana na mimea peke, au labda unahudhuria Kanisa la Waadventista Wa Sabato kwa mara ya kwanza na unagundua kwamba hakuna nyama kwenye chakula cha pamoja.
Hii si jambo lisilo la kawaida katika Uadventista.
Kwa kweli, takriban 36% ya Waadventista ni watumiaji wa vyakula vinavvyotokana na mimea kwa sehemu, maana yake hawali nyama au samaki lakini wanaweza kula mayai au maziwa. Asilimia nyingine 16% hula samaki au nyama mara kwa mara, kulingana na Tafiti za Afya ya Waadventista zilizofanywa na Chuo Kikuu cha Loma Linda.1
Kwa vyovyote vile, labda unajiuliza ni kwa nini wanafanya hivyo.
Utumiaji wa chakula cha mimea umekuwa maarufu ndani ya Uadventista wa Sabato kwa sababu tunathamini afya binafsi na tunaamini kuwa lishe inayotokana na mimea ni njia nzuri ya kutunza miili yetu, kudumisha ustawi, na kumheshimu Mungu (1 Wakorintho 6:20; 10:31; Warumi 12:1-2). Mungu awali aliwapa wanadamu lishe iliyotokana na mimea, kulingana na Mwanzo 1:29, na leo, utafiti unaonyesha faida za lishe yenye kiasi cha chini cha bidhaa za wanyama na yenye matunda, mboga, nafaka, na karanga.
Hata hivyo, shauku ya kutumikia Mungu kwa njia hii haimaanishi kuwa ni njia ya kuwa “mtakatifu zaidi” au kwa namna fulani kupata wokovu. Waadventista wanakusudia kuishi kwa namna hii kama mwitikio kwa kile ambacho Mungu amefanya kwetu kama wanadamu.
Ili kufafanua zaidi kwa nini utumiaji wa vyakula vya mimea ni maarufu miongoni mwa Waadventista, tutaanaglia:
Kwa kuanza, hebu tugeukie mtazamo wa Biblia.
Biblia inasemaje kuhusu chakula kianchotokana na mimea?

Photo on Pexel
Tunaposoma kuhusu Adamu na Hawa wakiishi Bustani ya Edeni, tunagundua kwamba mpango wa awali wa Mungu kwa mwanadamu ulijumuisha lishe ya mimea. Aliwaambia wanadamu wapya:
“Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu;” (Mwanzo 1:29, SUV).
Na inaeleweka kwamba Mungu angekuwa amewapa Adamu na Hawa chakula ambacho kingekua kwa njia endelevu kwao. Na katika ulimwengu kamili bila kifo cha aina yoyote, kuchinja wanyama ingekuwa jambo lisiloeleweka.
Haikuwa mpaka baada ya gharika ambapo Mungu aliporuhusu moja kwa moja wanadamu kula nyama (Mwanzo 9:3-4). Baada ya gharika, mimea ya dunia ilikuwa imeharibiwa na ingechukua muda kukua na kuweza kutoa chakula tena.
Kwa sababu hii, Mungu alimwagiza Nuhu kuwaingiza kwenye safina wanyama saba wa kila aina “safi” (Mwanzo 7:2-3).
(Mambo ya Walawi 11 na Kumbukumbu la Torati 14 yanaeleza kwa undani zaidi ni nyama ipi inayohesabiwa kuwa “safi”.)
Baada ya wakati wa gharika, watu wengi katika Biblia walikula nyama. Ilikuwa ni lazima katika jamii ambapo chakula safi haikuwa rahisi kupatikana na halingeweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu. Hivyo, ili kukidhi mahitaji yao ya lishe, walivua wanyama ili kuhudumia familia zao.
Mahali fulani leo, inaweza kuwa vigumu kuwa mtumiaji wa chakula cha mimea au kutoa lishe ya kutosha kutokana na ukosefu wa chaguzi za vyakula hivyo. Lakini waadventista wengi wanaoishi sehemu zenye upatikanaji rahisi wa matunda, mboga, nafaka, na dengu mwaka mzima huchagua lishe ya mimea ili kula karibu na lishe ya awali kadri iwezekanavyo.
Na sayansi ya kisasa inaendelea kuonyesha faida za kula njia hii, kama tutakavyoona katika sehemu inayofuata.
Kile sayansi inachosema kuhusu chakula cha mimea
Chakula bora cha mimea, kilicho na matunda, karanga, mboga, na mbaazi, kina faida nyingi kwa afya ya mwili, kama ilivyoonyeshwa na utafiti uliofanywa katika miaka 20 iliyopita. Kula mboga kunahusishwa na:2
- Shinikizo la damu lililopungua, cholesterol ya LDL, na BMI
- Hatari ndogo ya magonjwa ya moyo
- Hatari ndogo ya kansa
- Hatari ndogo ya kisukari cha aina ya 2
- Hatari ndogo ya unene kupita kiasi3
Tafiti za Afya za Waadventista, zilizofanywa na Chuo Kikuu cha Loma Linda, zimeangalia uhusiano kati ya mtindo wa maisha na afya kwa Waadventista wa Sabato. Utafiti wa Afya ya Waadventista-1 uliwahoji zaidi ya watu 34,000 kwa kipindi cha miaka 14 na kugundua uhusiano muhimu kati ya lishe ya mboga yenye nyuzinyuzi nyingi na hatari ndogo ya kansa.
Utafiti wa pili wa Afya za Waadventista-2, uliohusisha zaidi ya washiriki 94,000, ulitoa ufahamu zaidi. Uligundua kwamba Waadventista ambao hawali nyama walikuwa na hatari ndogo ya kupata ugonjwa wa kisukari aina ya pili.4
Uchambuzi mwingine wa data kutoka Utafiti wa Afya za Waadventista-2 uligundua kwamba Waadventista waliopata protini kutoka kwenye vyakula kama vile dengu, karanga, na mbegu walikuwa na hatari ndogo ya kufa kutokana na magonjwa ya moyo kuliko wale waliopata protini kutoka kwa nyama.5
Urefu wa maisha ya Waadventista pia unazungumza kuhusu mtindo wao wa maisha na namna wanavyokula.
Watafiti waligundua kuwa wanaume Waadventista huko California ambao ni watumiaji wa vyakula vinavyotokana na mimea waliishi karibu miaka 10 zaidi kuliko wenzao.6
Kwa kweli, Loma Linda, California, eneo lenye mkusanyiko mkubwa wa Waadventista, lilivuta usikivu wa mtafiti Dan Buettner alipokuwa akitafiti “Blue Zones,” au maeneo duniani ambapo watu huishi maisha marefu sana (mara nyingi zaidi ya miaka 100) na afya bora kuliko idadi ya watu wa kawaida.
Aliita Loma Linda kama moja ya Blue Zones hizo kwa sababu ya Waadventista wengi wanaoishi huko ambao ni makini kuhusu afya na hula chakula cha mimea au hawatumii nyama kabisa.
Ingawa lishe siyo sababu pekee ya afya na maisha marefu katika Blue Zones, ni moja ya sababu muhimu. Wakazi wengi wa Blue Zone hula 95% ya vyakula vya mboga, wakila nyama mara chache na kuzingatia vyakula visivyosindikwa, kama vile mbaazi, mboga, matunda, karanga, na nafaka nzima. Ikiwa wanakula nyama, kwa kawaida ni nyama nyeupe, kama samaki, na wantumia kidodgo au hawatumii kabisa nyama nyekundu.7
Faida za afya za kuwa mlo unaotokana na mimea zinaendana na shauku ya Waadventista kumheshimu Mungu kwa kuwa mawakili wema wa miili ambayo Mungu ametupa, wakijitahidi kudumisha ustawi kwa njia nyingi iwezekanavyo. Hebu tuangalie hilo.
Sababu za kiroho za Waadventista kuchagua lishe ya mimea

Photo by Pablo Merchán Montes on Unsplash
Pamoja na kujitahidi kuwa rafiki wa mazingira na huruma kwa wanyama, Waadventista wanaona kuwa kuishi kwa afya ni namna nzuri ya kutumikia na kumheshimu Mungu ipasavyo. Kifungu kimoja tunachoweza kutegemea katika Maandiko ni 1 Wakorintho 6:19-20:
“Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu, wala ninyi si mali yenu wenyewe? Kwa maana mlinunuliwa kwa thamani; basi mtukuzeni Mungu katika miili yenu” (SUV).
Kwa kuwa miili yetu ni “hekalu la Roho Mtakatifu”—njia ambayo Mungu anatumia kuongea na akili zetu—tunatafuta kutunza miili yetu, kiroho, kiakili, na kimwili. Hivyo inaeleweka kwa afya njema kuwa kipaumbele.
Kula vyakula vyenye afya ni moja ya mambo hayo. Inasaidia kudumisha akili zetu wazi, hivyo kuwa rahisi kumkaribia Mungu na kumtumikia kwa ufanisi zaidi.
Mtume Paulo anahitimisha wazo hili la kumheshimu Mungu katika barua yake kwa kanisa la Korintho:
“Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu” (1 Wakorintho 10:31, SUV).
Na kwa kweli hili linahusu hasa —kumtumikia Mungu na kuuelekeza maisha yetu kwake. Kufanya chaguzi za kiafya kunasaidia lengo hilo kuu.
Elige un estudio bíblico en línea
¿Quieres seguir aprendiendo? Descubre más sobre Jesús, la humanidad, el plan de salvación y cómo Dios te ama lo suficiente como para sacrificarlo todo, solo para darte la oportunidad de elegirlo a Él.
A veces puede ser difícil saber por dónde empezar, por eso ofrecemos opciones gratuitas y fáciles de usar para estudiar la Biblia en línea, que puedes hacer en cualquier momento, en cualquier lugar y a tu propio ritmo.
Esta escuela bíblica en línea te llevará a través de los principales temas de las Escrituras, desglosando los conceptos complejos de la Biblia en piezas fáciles de digerir, que pueden guiarte hacia las respuestas a las preguntas más desafiantes de la vida.
Kurasa zinazohusiana
- “Adventist Health Study–2,” Loma Linda University. [↵]
- “Becoming a vegetarian,” Harvard Health Publishing. [↵]
- “Plant-based nutrition: Exploring Health Benefits for Atherosclerosis, Chronic Diseases, and Metabolic Syndrome—A Comprehensive Review,” Nutrients, July 2023. [↵]
- Sabaté, Joan, et al. “Unscrambling the relations of egg and meat consumption with type 2 diabetes risk,” National Library of Medicine, November 1, 2018. [↵]
- Tharrey, Marion, et al. “Patterns of plant and animal protein intake are strongly associated with cardiovascular mortality: the Adventist Health Study–2 cohort,” National Library of Medicine, October 1, 2018. [↵]
- “Findings for Longevity,” Loma Linda University Health. [↵]
- “Top Reasons Why Blue Zones are the Healthiest Places to Live,” Plant Whys. [↵]
Majibu Zaidi
Njia 12 Halisi za Kukabiliana na Wasiwasi
Njia 12 Halisi za Kukabiliana na WasiwasiTAHADHARI: Maudhui haya ni kwa madhumuni ya taarifa tu. Hayawakilishi ushauri wa kitaalamu wa matibabu, na haikusudiwi kama mbadala wa matibabu ya kitaalamu ya afya ya akili. Ni rahisi kushikwa katika mzunguko wa wasiwasi. Hasa...
Jinsi ya Kutuliza Fikira za Wasiwasi, Kwa Kutumia Biblia
Jinsi ya Kutuliza Fikira za Wasiwasi, Kwa Kutumia BibliaUlikuwa unategemea simu kutoka kwa binti yako nusu saa iliyopita, na bado hajapiga simu. Pia hajibu simu zako. Unahisi moyo wako ukidunda huku mawazo yako yakikimbia: labda amepata ajali ya gari?, Vipi kama kitu...





