Biblia—bila shaka—ndiyo kitabu muhimu zaidi. Ni kipimo tunachotumia kupima maandishi mengine yote, ikiwa ni pamoja na yale ya Ellen White.
Kanisa la Waadventista Wa Sabato linaamini kwamba “maandishi ya Ellen White sio mbadala wa Maandiko Matakatifu. Hayawezi kuwekwa kwenye kiwango sawa. Maandiko Matakatifu yanasimama peke yake, kiwango cha pekee ambacho maandishi ya Ellen White na yale mengine yote lazima yapimwe kwayo na kuwa chini yake.”1
Tunaelewa kwa nini unaweza kuuliza swali hili, ingawa. Ni kweli kwamba Ellen White ni kielelezo cha pekee katika Uadventista ambaye ametupatia ufahamu mwingi kuhusu mada mbalimbali za Kimaandiko, kama vile Sabato, Ujio wa pili wa Kristo, na Pambano Kuu kati ya Kristo na Shetani linaloendelea katika Biblia.
Akiongozwa na Roho Mtakatifu, alipokea na kushiriki ufahamu kutoka kwa Mungu uliosaidia kuthibitisha kweli za Kimaandiko ambazo baadaye zilikuwa mafundisho ya Uadventista.
Lakini maandishi yake yote yameelekeza kwenye kusoma Maandiko kwa kina zaidi ili kuelewa dhana hizi. Zinatoka kwenye Biblia, sio kutoka kwenye maandishi yake.
Yeye mwenyewe asingesita kusema kwamba Biblia ni muhimu zaidi kuliko maandishi yake. Tutafafanua baadhi ya maneno yake tunapochunguza mada hizi:
- Kwa nini Biblia ni muhimu zaidi
- Ellen White alisemaje kuhusu maandishi yake
- Jinsi ya kutumia maandishi ya Ellen White katika safari yako ya kiroho
Tuanze.
Kwa nini Biblia ni muhimu zaidi

Photo by John-Mark Smith
Biblia ndio mamlaka kuu na chanzo cha ukweli. Kila kitu kingine chochote —pamoja na maandiko ya Ellen White— lazima ipimwe kwa kigezo hiki (Isaya 8:20).
Kama mwanahistoria na mwandishi wa Kikristo George Knight alivyo bainisha katika mahojiano, “Bila Biblia, hatungekuwa na Ellen G. White. Mamlaka yake inatokana na mamlaka ya Maandiko.”2
Baada ya yote, ni Biblia inayotuambia kwamba roho ya unabii itakuwa moja ya karama za Roho katika siku za mwisho (Matendo 2:17; Waefeso 4:11-13) na inatupatia vipimo vya nabii:
“Karama ya unabii imejengwa daima juu ya Maandiko na kupimwa na Maandiko.”3
Biblia pia ina lengo tofauti zaidi ya maandishi ya Ellen White.
Ni kitabu kisichopitwa na wakati kinachotoa kanuni zinazoweza kutumika kwa nyakati zote. Ni kigezo chetu cha kutathmini kila eneo lingine la maisha. Na ni msingi wa kila fundisho.
Kwa upande mwingine, maandishi ya Ellen White yalikuwa kwa wakati na lengo maalum—na lazima yapatane na kipimo cha Maandiko. Hayakukusudiwa kutoa msingi wa mafundisho bali tu kutoa ufahamu mkubwa zaidi wa mafundisho katika Biblia.
Hivi ndivyo Gerhard Pfandl, mkurugenzi mstaafu wa Idara ya Utafiti wa Biblia ya Waadventista wa Sabato, anavyoliweka hili. Alisema maandiko ya Ellen White ni:
“…Ujumbe wa Mungu kwa watu fulani…wakati fulani katika historia—wakati wa mwisho. Maandiko yake sio viwango vipya au vya ziada vya mafundisho, bali ni msaada kwa kanisa katika wakati wa mwisho.”4
Ellen White mwenyewe alielewa wazi jukumu lake. Basi tuangalie alichokisema.
Alichosema Ellen White kuhusu maandiko yake mwenyewe na Biblia

Ellen G. White, circa 1878 – Photo courtesy of the Ellen G. White Estate, Inc.
Ellen White aliona Biblia—Agano la Kale na Agano Jipya—kama mamlaka kuu na mwongozo kwa kila sehemu ya imani na maisha ya Kikristo. Aliita maandishi yake “mwanga mdogo wa kuwaongoza wanaume na wanawake kwenye mwanga mkubwa”—Maandiko Matakatifu na Yesu Kristo.5
Aliunga mkono na kusimamia kanuni ya Kiprotestanti ya sola scriptura (Biblia pekee):
“Katika neno lake, Mungu ameweka kwa wanadamu maarifa yanayohitajika kwa wokovu. Maandiko Matakatifu yanapaswa kukubaliwa kama ufunuo wenye mamlaka, usioweza kukosea mapenzi yake. Ni kipimo cha tabia, Hufunua mafundisho, na ni kipimo cha uzoefu.”6
“Mungu atakuwa na watu duniani kudumisha Biblia pekee, kama kigezo cha mafundisho yote na msingi wa mageuzi yote.”7
Na akatambua kuwa Biblia ilikuwa kigezo cha kupimia mafundisho yake yote pia.8
Lakini mara kwa mara, watu waliomsikiliza Ellen White na kusoma maandishi yake waliyatumia vibaya. Katika visa hivi, alilazimika kutoa maonyo makali—na kwa haki.
Hakutaka kamwe Neno la Mungu lidharauliwe au kupuuzwa kwa njia yoyote kwa sababu ya alichosema.
Hapa kuna mfano wa makaripio aliyolazimika kuandika kwa viongozi wa kanisa katika Mkutano Mkuu kwa sababu hawakufuata mwongozo wa Mungu:
“Usinukuu maneno yangu tena maisha yako yote, mpaka uweze kutii Biblia.”
“Unapofanya Biblia iwe chakula chako, nyama yako, na kinywaji chako, unapofanya kanuni zake kuwa sehemu ya tabia yako, utajua vizuri jinsi ya kupokea ushauri kutoka kwa Mungu. Ninatukuza Neno lenye thamani mbele yako leo. Usirudie niliyosema, ukisema, ‘Dada White alisema hivi,’ na ‘Dada White alisema vile.’ Chambua kile Bwana Mungu wa Israeli anachosema, kisha fanya kile Anaagiza.”9
Wakati mmoja, hata alibainisha kwamba vitabu vyake vya Ushuhuda kwa Kanisa visingehitajika kama watu wa Mungu wangalikuwa wamesoma Maandiko!
Lakini kwa sababu walikuwa wamepuuza Neno lake, Mungu alimpa Ellen White ujumbe wa kuwaonyesha watu njia ya kurudi kwenye mafundisho yake na kuwaonyesha jinsi ya kuyatumia katika maisha yao.10
Basi, maandishi yake yana nafasi gani leo?
Jinsi ya kutumia maandishi ya Ellen White katika safari yako ya kiroho

Photo by Emmanuel Phaeton on Unsplash
Maandiko ya Ellen White yanaweza kutupa mwongozo uliovuviwa, ufahamu, na faraja. Lakini hayapaswi kuchukua mahali pa kujifunza Biblia. Endelea kuweka Biblia kama msingi wa imani yako, maamuzi, na matendo yako.
Ikiwa utagundua kuwa maandiko ya Ellen White yanakuzuia usitumie muda katika Biblia, basi inaweza kuwa wakati wa kujipanga upya. Baada ya yote, alitaka tuweze kusoma Biblia zetu zaidi na kufuata tunachokipata huko. Hio ilikuwa moja ya madhumuni makubwa ya maandishi yake mwanzoni!
Lakini kwa kweli, tunapotumia maandishi yake ipasavyo, inaweza kuongeza thamani ya maandiko kwetu na kutuongoza kutaka kujiunza zaidi. Pia inaweza kutusaidia katika maandishi hayo maishani mwetu
Hapa kuna vidokezo vichache ili kupata aina hiyo ya uzoefu:
- Unapojifunza kitu kipya katika vitabu vyake, rudi katika Biblia na uchunguze kwa makini.
- Tafuta kanuni kuu kutoka katika Maandiko. Jaribu kuelewa muktadha ambao alikuwa anaandika. Mara nyingi alizungumzia watu maalum katika maeneo maalum na hali maalum, hivyo ni muhimu kupata lengo kuu badala ya kushikilia maagizo yaliyojitenga.
- Usianzishe mafundisho mapya kutoka katika maandiko ya Ellen White. Yeye mwenyewe alisema hili halikuwa lengo la maandishi yake.11
Hatua hizi rahisi zinaweza kwenda mbali katika kuzuia kutokuelewana na kudumisha maandishi ya Ellen White katika jukumu lake lililotolewa na Mungu.
Na ikiwa unajiuliza uanze wapi, vitabu hivi ni bora kwa kuona jinsi anavyoakisi ukweli wa Biblia:
- Hatua kumuelekea Kristo
- Tumaini la vizazi vyote
- Mafundisho ya Kristo kwa Vielelezo
- Mawazo kutoka kwenye Mlima wa Baraka
Biblia ndiyo kanuni ya imani na Uzoefu wa Waadventista.
Ikiwa Ellen White angekuwa hai leo na tukamuuliza kuhusu umuhimu wa maandishi yake, huenda angesema:
“Nakushauri, mpendwa msomaji, neno la Mungu liwe kipimo cha imani yako na matendo yako.”12
Waadventista wa Sabato wanaendelea kuzingatia ushauri huu kwa umakini.
Ingawa tunathamini sana ushauri wake, ambao ulivuviwa na Roho Mtakatifu, tunajenga imani yetu kwenye Biblia na kuruhusu ushauri wake kutuongoza kurudi katika Biblia.
Lakini ingawa Waadventista hawaweki maandishi ya Ellen White juu ya Biblia, huenda bado ukajiuliza ikiwa kuamini karama yake ya unabii ni sharti la kuwa Mwadventista. Gundua jibu la swali hili hapa: “Je, Lazima Nimwamini Ellen White Ili Niwe Mwadventista?“
Kurasa zinazohusiana
- Seventh-day Adventists Believe, p. 227 [↵]
- “Ellen White vs The Bible w. Dr. George Knight | Biblios 14,” SECmedia [↵]
- Ibid. [↵]
- Pfandl, Gerhard, “The Authority of the Ellen G. White Writings” [↵]
- White, Ellen G., The Review and Herald, January 20, 1903, quoted in The Colporteur Evangelist, p. 37 [↵]
- White, Ellen G., The Great Controversy, p. vii [↵]
- Ibid., p. 595 [↵]
- Ibid., p. vii [↵]
- White, Ellen G., Selected Messages, Book 3, p. 33 [↵]
- White, Ellen G., Testimonies for the Church, vol. 5, p. 664 [↵]
- White, Ellen G., A Sketch of the Christian Experience and Views of Ellen G. White, p. 63 [↵]
- Ibid. [↵]
Majibu Zaidi
Ellen White anasema nini kuhusu Maombi?
Je, umewahi kuwa na mzigo ambao ulihitaji kumwambia mtu, lakini uliogopa kuhukumiwa ikiwa ungefanya hivyo?
Ellen G. White Alisaidia Vipi Katika Kuanzisha Kanisa la Waadventista wa Sabato?
Ellen G. White, mwanamke mnyenyekevu kutoka Gorham, Maine, alikuwa mmoja wa waanzilishi wa Kanisa la Waadventista wa Sabato na kiongozi muhimu tangu mwanzo wake.
Ellen White na Kitabu cha Pambano Kuu
Pambano Kuu ni moja ya vitabu vya Ellen G. White vinavyo thaminiwa zaidi na Waadventista wa Sabato.
Roho ya Unabii Ni nini (Kitabu cha 1-4) na Ellen G. White?
Kutumia unabii wa Biblia katika historia, matukio ya hivi karibuni, na hasa siku za usoni, inaweza kuwa kazi ngumu. Hata linaweza kuwa jambo la kutisha kidogo kwa baadhi.
Ellen White Alifundisha nini Kuhusu Matumizi ya Vyakula Vinavyotokana na Mimea?
Moja ya mambo ambayo unaweza kuwa umewahi kusikia kuhusu Waadventista wa Sabato ni msisitizo wao kwenye mtindo wa maisha wa kutumia vyakula vinavyotokana na mimea.








