Waadventista wa Sabato wanajulikana kwa kusisitiza maisha yenye afya bora. Na Ellen G. White alikuwa na ushawishi mkubwa katika maendeleo ya kipaumbele hiki na utekelezaji wake miongoni mwa Waadventista.
Alifundisha kwamba kujali miili yetu, akili, na roho ni jukumu la kila Mkristo kwa nafsi yake, kwa jamii, na kwa Mungu—muumba na mtunzaji wetu.
Katika makala haya, tutajadili jinsi maandiko ya Ellen White yalivyochangia sana katika kuelewa na utekelezaji wa ujumbe wa afya wa Waadventista. Tutachunguza:
Nafasi ya Ellen White katika kuendeleza ujumbe wa afya wa Kanisa la Waadventista wa Sabato

Courtesy of the Ellen G. White Estate, Inc.
Shauku ya Ellen White katika maswala ya afya ilianza mapema kwani alipata jeraha la utotoni lililoathiri ubora wa maisha yake. Pia alikuwa na uzoefu wa kutunza wagonjwa katika familia yake, hasa mumewe, James White.
Lakini zaidi ya safari yake binafsi katika maisha yenye afya, pia alihamasisha mtindo wa maisha wenye afya kati ya Wakristo wenzake. Ufahamu wake wa kanuni za afya uliongezeka kadri alivyopokea ufunuo kutoka kwa Mungu, na hatua kuu zikiwa:
- Disemba 1848 – Ushauri wa kuepuka tumbaku, chai, na kahawa
- Februari 1854 – Kuzingatia usafi binafsi na kuwa makini na hamu ya kula
- Juni 1863 – Mashauri ya maelezo ya kina kuhusu kuzuia magonjwa, na tabia za kila siku za kuishi kiafya
- Disemba 1865 – Ushauri kuhusu kuanzisha kituo cha afya kuhudumia wagonjwa na kutoa mafunzo kuhusu kuishi kiafya.
Aliandika kanuni hizi katika vipeperushi, kama makala katika magazeti ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato, na pia kuzitoa kama barua binafsi au ushauri kwa watu binafsi au kanisa kwa ujumla.
Kisha akaziweka pamoja katika vitabu kama vile Huduma ya Uponyaji. Na baadaye sana, watunzaji wa maandishi yake, Hazina ya Ellen G. White, walikusanya maandishi yake kuhusu afya katika vitabu vya mada kama vile Mashauri Kuhusu Lishe na Vyakula, Huduma ya Tiba, n.k.
Kanuni hizi zilikuwa mwanga kwa Waadventista zikiwaongoza katika kutumia na kuishi kile kilichojulikana kama Ujumbe wa Afya wa Kiadventista.
Lakini safari ya kujifunza mafundisho haya, au ya kuyafanya kuwa njia ya maisha, haikuwa rahisi. Ilichukua marekebisho makubwa na mabadiliko ya mtazamo kutoka kile kilichochukuliwa kuwa “kawaida” wakati huo.
Hapa kuna muhtasari wa jinsi ilivyotokea.
Waadventista wa mwanzo na ujumbe wa afya
Baada ya Kanisa la Waadventista Wasabato kuundwa katika misingi ya mafundisho yake na muundo wa kiutawala, Ellen White alielekeza umakini wake katika afya ya washiriki wa kanisa.
Na kwa sababu nzuri.
Kufikia mwanzoni mwa miaka ya 1860, viongozi wengi wa kanisa la Waadventista na wafanyakazi walikuwa wakipatwa na maradhi. Magonjwa mengi yalisababishwa na usafi duni binafsi, kufanya kazi kupita kiasi, mazingira mabaya ya kuishi, na sababu zingine zinazoweza kuepukika.
Katika karne ya 19, mazoea ya kiafya ambayo tunayoona kuwa ya kawaida leo hayakujulikana au yalipuuzwa.
Hivyo akaanza kushauri kuishi kwa usafi, lishe yenye afya, na kutumia njia za asili kutibu magonjwa.
Ushauri wa Ellen White kuhusu kuishi kwa afya

Photo by Sweet Life on Unsplash
Ellen White alianza kwa kuonyesha kwa nini kujali afya zetu ni njia ambayo kwayo tunaweza kuitikia upendo wa Mungu. Na pia inaweza kutusaidia kuwa na uwezo zaidi wa kumtumikia Yeye na kukua katika imani yetu.
Akiangazia 1 Wakorintho 6:19-20 katika Biblia, alionyesha kwamba ukuaji wetu kiroho na uzoefu unategemezwa na hali ya ustawi wetu kimwili. Kwa kuwa mwili ni “hekalu la Roho Mtakatifu,” ina maana tu kuutunza vizuri kama tendo endelevu la ibada (NKJV).1
Alijua wazi kwamba kufuata kanuni hizi za afya sio njia ya mtu kupata wokovu. Na kwamba ukomavu au kiroho wa mtu haupaswi kuhukumiwa na hali ya afya aliyonayo sasa.
Kwa kweli, ingawa watu wengi sasa wanaziita “sheria za afya,” hazipaswi kuchukuliwa kama maelekezo matakatifu au sheria kali.
Badala yake, zilipaswa kutazamwa kama kielelezo cha upendo wetu na shukrani kwa Mungu. Tunatunza afya yetu kama sehemu ya utayari wetu wa kufuata kile alichofunua kuwa njia bora kwetu kwa sababu Yeye anatupenda na anatutakia mema.2
Pia, Ellen White alionyesha kwamba afya yetu ya akili inahusiana na ustawi wetu kimwili. Tatizo katika afya ya mwili pia huathiri utendaji wa akili. Na hali ya kihisia na akili yenye msongo hupelekea afya duni kimwili.
Zaidi kuhusu hili inaweza kupatikana katika vitabu vyake Akili, Tabia na Utu Volumes 1 na 2.
Kwa kuelewa hii, kauli mbiu ya Mkristo katika eneo la afya ilikuwa kukuza na kudumisha maisha na afya njema.3
Basi hilo lilionekanaje?
Hapa kuna muhtasari wa kanuni za afya na mazoea aliyopendekeza kupitia maandishi yake:
Mungu ndiye chanzo cha afya na uponyaji
Ellen White alikuwa haraka sana kutambua kwamba Mungu ndiye mtoa uzima, na ni Yeye pekee anaweza kurejesha afya.
Kwamba katika jitihada zetu zote za kudumisha mwili wenye afya, akili na roho, ukweli ni kwamba tunashirikiana tu na Mungu, Mponyaji. Aliandika:
“Nguvu yote ya kutoa uhai inatoka kwake. Wakati mtu anapopona kutoka katika ugonjwa, ni Mungu pekee anayemrejesha.”4
Ni kama vile hata dawa za kisasa haziponyi mwili. Matibabu na taratibu husaidia mwili kupigana na magonjwa na majeraha, lakini bado ni mifumo ya asili ya mwili inayoponya. Kwa mfano, daktari anarekebisha mfupa baada ya kuvunjika, lakini mchakato wa uponyaji wa mwili ndio unaoponya mfupa.
Kula chakula bora zaidi5

Image from foodiesfeed
Ellen White alihamasisha mabadiliko ya endelevu kutoka katika lishe inayotegemea nyama kwa kiasi kikubwa hadi lishe inayotokana na mimea. Aliandika:
“Nafaka, matunda, karanga, na mboga ndicho chakula kilichochaguliwa kwa ajili yetu na Muumba wetu. Vyakula hivi, vikitayarishwa kwa njia rahisi na ya asili iwezekanavyo, ndivyo vyenye afya na lishe zaidi. Vinatoa nguvu, uwezo wa kustahimili, na nguvu ya akili, ambayo haipatikani kwa lishe yenye utata na inayosisimua zaidi.”6
Tafadhali kumbuka kwamba anasema chakula kinapaswa kutayarishwa “kwa njia rahisi na ya asili iwezekanavyo.” Kwa hivyo, alihamasisha matumizi ya vyakula vyenye asili badala ya bidhaa zilizosindikwa sana.
Pia anashughulikia maelezo mengi kuhusu jinsi ya kupika kwa njia yenye afya zaidi, jinsi ya kupanga milo yetu, mara ngapi tule, kuepuka sukari nyingi na mafuta yaliyoganda n.k.
Maelezo ya miongozo yote hii ya vitendo kuhusu lishe yenye afya yamekusanywa katika kitabu chake, Mashauri Kuhusu Lishe na Vyakula.
Kuepuka tabia ambazo zina athari mbaya kwa mwili na akili
Alihimiza watu kujiepusha kabisa na tabia na vitu vinavyoharibu, na kufanya kwa kiasi hata na vitu vilivyochukuliwa kuwa vya afya.
Aliita kanuni hii kuwa ni uwakili wa Kikristo.
Alihimiza kutokutumia tumbaku, pombe, na vichocheo. Na pia alizungumzia mada kama vile kula kupita kiasi, kufanya kazi kupita kiasi, kusoma machapisho ya kubuni na yenye kuchochea hisia mbaya n.k.7
Hata alishughulikia baadhi ya maswala yaliyosababishwa na jinsi watu walivyovaa kawaida katika karne ya 19.8 Kama vile mavazi ya wanawake yaliyokuwa marefu sana na kuvuta sakafuni, kiasi cha kuleta uchafu kutoka mitaani na kuuingiza ndani. Na tusisahau kuhusu korseti, ambazo zilikazwa sana kwenye viuno na tumbo la wanawake hivyo kuzuia kupumua vizuri na harakati sahihi. Mienendo ya wakati huo ilikuwa na athari hasi kubwa kwa afya zao.9
Ukusanyaji wa maandishi yake kuhusu kanuni hii sasa unapatikana katika kitabu kiitwacho Kiasi.
Pumziko Sahihi
Wanadventista wengi wa awali walikuwa wenye bidii na wafanyakazi hodari. Lakini sifa njema hii mara nyingi iliwapelekea kujifanya kazi kupita kiasi. Wengi wao, kama vile James White na J.N. Andrews, walikufa wakiwa na umri mdogo, sehemu kubwa kutokana na uchovu na kujifanya kazi kupita kiasi.
Ellen White mara nyingi aliwashauri kupumzika. Alihimiza umuhimu wa kupata usingizi wa kutosha, na kwamba usingizi wenye manufaa zaidi unatokana na kwenda kulala mapema.
Kwa mfano, katika moja ya barua zake nyingi kwa wafanyakazi wenzake, alisema:
“Najua kutokana na ushuhuda niliopewa mara kwa mara kwa wafanyakazi wanaotumia akili, kwamba usingizi una thamani zaidi kabla ya saa sita usiku. Usingizi wa masaa mawili kabla ya saa sita usiku una thamani zaidi kuliko saa nne baada ya saa sita usiku.”10
Umuhimu wa mazoezi ya mwili11

Photo by Lucas van Oort on Unsplash
Ellen White alisisitiza umuhimu wa shughuli za kimwili katika kudumisha afya, na katika mchakato wa kutibu magonjwa.
Wafanyakazi wengi katika Kanisa la Waadventista wa Sabato la awali walikuwa waandishi, wahariri, wachungaji, na wasomi. Na ilikuwa kawaida kwao kutumia siku zao ndani, wakisoma au wakifanya kazi za uchapishaji.
Maisha ya kutokuwa na shughuli nyingi, pamoja na usiku usio na usingizi na kufanya kazi kupita kiasi, mara nyingi yalisababisha afya mbaya sana miongoni mwa safu za waanzilishi wa Uadventista.
Hivyo Ellen White alisisitiza umuhimu wake kwa kusisitiza usawa kati ya kazi za kiakili na kimwili. Aliwaomba watumie muda nje kila siku, wakifanya mazoezi au kufanya kazi kwenye jua na hewa safi.
Pia alionyesha jinsi shughuli za kimwili zilivyokuwa muhimu katika kusaidia uponyaji kwa wagonjwa.
Ndio maana alipojitokeza kuunga mkono Waadventista kuanzisha vituo vyao vya afya vilivyoitwa Sanitarium, alihakikisha kwamba mazoezi ya kimwili yalikuwa sehemu ya ratiba ya kila siku ya wagonjwa. Na kwa wale ambao walikuwa dhaifu sana kufanya mazoezi, kupata msaada wa kupewa mazoezi ya kupumzika ingekuwa chaguo la kiafya.12
Pia, kama sehemu ya mtaala wa elimu ya Kiadventista, alisisitiza wanafunzi kusawazisha masomo na kazi za nje.
Na pamoja na hili, alisisitiza mazoea mengine kama ukaaji sahihi, na matumizi sahihi ya sauti katika kuzungumza na kuimba.
Matumizi ya mawakala asilia kukuza afya na uponyaji
Ellen White alipendelea tiba asilia badala ya dawa za wakati huo kwa ajili ya uponyaji.
Katika karne ya 19, viwanda vya dawa vilikuwa katika hatua za mwanzo. Na ingawa hawakukusudia madhara, baadhi ya dawa zilizopendekezwa na madaktari zilijumuisha vitu vya sumu kama strychnine na arsenic, na madawa ya kulevya yenye nguvu kama cocaine.13
Kutokana na mambo kama hayo katika tiba, Ellen White alihamasisha matumizi stadi ya tiba asilia zisizo na madhara kwa matibabu. Aliandika:
“Hewa safi, jua, kiasi katika kula, mapumziko, mazoezi, lishe sahihi, matumizi ya maji, imani katika nguvu za Mungu—hizi ndizo dawa za kweli. Kila mtu anapaswa kuwa na maarifa ya njia za uponyaji za asili na jinsi ya kuzitumia.”14
Alisisitiza sana matumizi ya tiba ya maji na dawa za mimea kama njia za matibabu zenye ufanisi bila madhara yoyote.15
Hii hakumaanisha kwamba alikataa dawa zote kiholela.
Hakuwa kinyume na baadhi ya taratibu za upasuaji, au dawa kama Quinine ambazo zikisimamiwa ipasavyo wakati zinapohitajika zingeweza kuokoa maisha.16
Waadventista walikubali kanuni hizi na kuzitumia katika nyumba zao. Na walipoanzisha vituo vya afya, vilikuwa vimeandaliwa kwa njia ambayo kanuni hizi pia zilitumika katika viwango vya taasisi kwa wagonjwa.
Kanuni hizi zimejadiliwa kwa kina katika kitabu Huduma ya Uponyaji.
Lakini unaweza kujiuliza jinsi Waadventista wanavyotumia kanuni hizi, zilizotolewa katika karne ya 19, leo katika karne ya 21.
Hebu tuangalie hilo.
Waadventista wanavyoelewa na kutumia ujumbe wa afya leo
Kwa miaka, Waadventista na mfumo wa afya wa Waadventista umebaki katika mstari wa mbele wa utafiti wa matibabu na ugunduzi.
Kumekuwa na maendeleo makubwa katika uga wa matibabu na afya ya umma katika karne iliyopita. Ugunduzi kuhusu vifaa salama na taratibu za kuzuia, kutambua, na kutibu magonjwa umefanywa. Na Waadventista wamepokea kwa uangalifu mazoea haya.
Hata hivyo, pamoja na maendeleo yote, kanuni za kuishi kiafya ambazo Ellen White alizitangaza zimeonekana kuwa zisizopitwa na wakati.
Bado wanazingatia na kuishi sheria za afya katika nyumba zao, hospitali, na vituo vya mtindo wa maisha.
Pia wamegundua njia za ubunifu za kufundisha kanuni hizi zilizotokana na maandishi ya Ellen White kwa njia rahisi kama programu za elimu ya mtindo wa maisha. Mifano ya programu hizo ni pamoja na:
- Afya ya UUMBAJI na Advent Health katika Hospitali ya Florida
- Programu ya maisha ya NEWSTART na Kituo cha Maisha cha Weimar
- CHIP Australia
Moja ya maarufu zaidi ni programu ya NEWSTART, ambayo ni ufupisho wa sheria mbalimbali za afya:
Hii ni mfano unaotumiwa katika vikao vingi vya elimu ya afya ya Waadventista leo.
Ujumbe wa afya umebaki kuwa sehemu muhimu ya kila mkutano wa injili wa Kiadventista.
Katika sehemu inayofuata, tutaangalia jinsi Ellen White alivyofundisha kuhusu ujumbe wa afya ukiwa sehemu ya mfano wa injili ya Kiadventista.
Mchango wa Ellen White katika huduma ya afya ya Waadventista na injili ya matibabu

Courtesy of the Ellen G. White Estate, Inc.
Kuanzia mwishoni mwa mwaka 1865, Ellen White alianza kuhamasisha Kanisa kuanzisha vituo vya afya ambavyo vingefuata kanuni hizi za afya katika kutunza wagonjwa. Pia wangewafundisha wagonjwa na familia zao kanuni hizo, ili waweze kwenda nyumbani wakiwa na taarifa ambazo zingewasaidia kudumisha afya bora.
Na katika huduma kwa wagonjwa, madaktari walikuwa wanafanya kile ambacho Yesu alifanya katika huduma yake ya uponyaji kwa kutoa mahitaji ya kimwili na kupunguza mateso.
Na kama vile mkono wa kulia daima unavyofanya kazi kurahisisha utendaji wa mwili, alirejelea ujumbe wa afya kama “mkono wa kulia” wa Injili.17
Huduma hii ya afya ilikuwa mara nyingi huitwa kazi ya umisionari wa kitabibu, au injili ya matibabu, kwani ilikuwa njia ya kuishi huduma ya uponyaji ya Yesu. Na ili kuhakikisha vituo hivi vya huduma ya afya vilikuwa na wafanyakazi waliofundishwa vizuri, Ellen White alipigania kuanzishwa kwa taasisi sahihi za mafunzo.
Maelezo ya jinsi ambavyo hili lingefanyika yanapatikana katika kitabu chake Huduma ya Matibabu.
Taasisi ya kwanza kati ya hizi ilikuwa Chuo cha Wainjilisti wa Matibabu huko California – kinacho julikana leo kama Chuo Kikuu cha Loma Linda.
Na Chuo Kikuu cha Loma Linda kimekuwa mstari wa mbele katika utafiti wa kisayansi wa hivi karibuni ambao umedhihirisha ushauri wa Ellen White kuhusu afya kuwa sahihi kisayansi.
Hebu tuangalie walichogundua.
Maandishi ya Ellen White na sayansi ya matibabu leo
Sayansi na utafiti wa kisasa unatuonyesha wazi faida za usafi binafsi,18 mazoezi,19 kunywa maji ya kutosha,20 kupata mapumziko ya kutosha,21 kupata mwanga wa kutosha wa jua,22 na hewa safi23 n.k.
Pia, madhara hatari ya tumbaku,24 pombe,25 na vitu vingine vinavyoharibu afya vinafahamika sana.
Na wakati habari hizi zimekuwa wazi kwetu leo, jamii kwa ujumla ilikuwa haina ufahamu kuhusu hayo wakati wa Ellen White.
Wale waliofuata ushauri wake walifurahia faida za afya ambazo wengine wangefaidika nazo miongo kadhaa baadaye. Alikuwa mbele ya wakati wake.
Hapa kuna utafiti wa kisasa unaoonyesha hivyo:
Tangu mwaka 1958, Chuo Kikuu cha Loma Linda kimefanya mfululizo wa utafiti wa matibabu wa muda mrefu uitwao Adventist Health Studies (AHS).
Tafiti hizi, zilizofanywa miongoni mwa Waadventista Wa Sabato, zimeonyesha jinsi mtindo wao wa maisha wenye afya ulivyopelekea matokeo mazuri. Waadventista wana kiwango cha chini sana cha vifo kutokana na kansa, magonjwa ya moyo, na kiharusi, ambacho kina uhusiano moja kwa moja na kufuata kwao kanuni za afya ambazo Ellen White aliandika.
Ili kujifunza zaidi kuhusu masomo haya, soma makala yetu kuhusu Tafiti za Kiadventista za Afya.
Utafiti mwingine wa hivi karibuni kuhusu Waadventista ni Blue Zones, uliofanywa na Dan Buettner na National Geographic.
Ilipata jamii 5 duniani zenye idadi kubwa ya watu waliokua na umri wa miaka 100 bila matatizo ya kiafya.
Moja ya maeneo haya ilikuwa Loma Linda, California.
Hili ni eneo lenye idadi kubwa zaidi ya Waadventista huko Amerika Kaskazini, na wanaishi hadi miaka 10 zaidi wenye afya kuliko Mmarekani wa kawaida.
Sababu ni ipi?
“Wanafuata lishe ya Kibiblia ya nafaka, matunda, karanga, na mboga.”26 Lishe ambayo Ellen White aliandika kuhusu miaka 200 iliyopita.
Lakini Ellen White hakuwa peke yake akipigania matengenezo ya afya. Walikuwepo wengine, baadhi yao ambao hata alishirikiana nao.
Wanamatengenzo ya afya wengine wakati wa Ellen White
Kwa ujumla, kulikuwa na harakati nyingi hasa zikipinga matumizi ya pombe, tumbaku, na dawa nyingine katika miaka ya 1800.27
Ellen White mara nyingi aliunga mkono harakati hizi, na hata alihutubia katika baadhi ya mikutano yake.
Lakini kulikuwa na wanamatengenezo wengine maarufu ambao walishiriki baadhi ya msimamo wake kuhusu afya.
Kwa kweli, kwanza alipata tiba ya maji kutoka katika sanitariam iliyoitwa “Our Home on the Hillside,” huko Dansville, New York, iliyokuwa ikiongozwa na Dk. James Caleb Jackson. Alitumia baadhi ya kanuni za afya ambazo Ellen White alipigania, kama vile tiba za maji. Lakini pia walipinga mazoezi mengine kama vile shughuli za kimwili kwa wagonjwa na maombi.28
Mwanzoni mwa karne ya 19, Sylvester Graham alikuwa mwana matengezo maarufu, hasa akisisitiza mageuzi ya lishe. Anakumbukwa zaidi kwa kitabu chake cha mwaka 1837 kinachoitwa “Treatise on Bread and Bread Making.” Alihamasisha matumizi ya unga wa ngano isiyokobolewa kutengeneza mkate. Unga huo ukawa unaitwa “unga wa Graham.”29 Na hata Ellen White alihamasisha matumizi yake.
Joseph Smith, mwanzilishi wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, alikuwa pia mwana matengenzo wa afya. Kama Ellen White, alifundisha kwamba kutunza miili yetu ni muhimu kwa kuwa miili yetu ni hekalu ya Mungu (1 Wakorintho 6:19). Pia alifundisha usafi binafsi, lishe bora, na kujiepusha na pombe, tumbaku, na kahawa.30
Hivyo, Ellen White alijiunga na wanamatengenezo hawa katika kukuza maisha yenye afya wakati wao.
Kile kinacho tofautisha mashauri yake ni mtazamo wake wa kina kuhusu afya. Alihimiza afya ya mwili, akili, na roho. Na zaidi ya yote, aliunganisha yote na uhusiano wa Mkristo na Mungu Anayetutakia afya na furaha.
Mashauri ya Ellen White kuhusu afya ni halisi, yenye busara, na yaliyoongozwa na Mungu
Ellen White alikuwa na jukumu kubwa katika kuhamasisha maisha ya kiafya kati ya waamini wenzake, pia kuwatia moyo kushiriki vidokezo hivi halisi, mara nyingine vinavyookoa maisha, kwa wote waliokuwa wakisumbuliwa.
Kupitia maandishi yake, Mungu alitumia kumwezesha kusaidia kutengeneza ujumbe wa afya unaoshughulikia mtu katika ukamilifu wake—sio tu dalili, au kugeuza watu kuwa mrundikano wa viungo vya mwili. Moja inayoonyesha jinsi Mungu anavyotaka tuishi maisha yetu bora, kimwili, kihisia, na kiroho. Pia inatusaidia kuwa bora katika kutumikia Mungu na wenzetu katika upendo wake (3 Yohana 1:2).
Na hii ndio imepelekea mfumo wa Afya wa Waadventista tunaojua leo. Kutoka katika ushauri wake, Waadventista waliendelea kuona huduma ya afya kama wito wa injili ya matibabu na elimu ya afya.
Na kadri sayansi inavyoendelea kuonyesha, kanuni hizi za afya ni za busara na muhimu kwetu, hata leo.
Je unataka kujua zaidi kuhusu Waadventista wanavyoamini kuhusu afya?
Kurasa zinazohusia
- White, Ellen G., Letter 85, 1888. [↵]
- White, Spiritual Gifts Vol. 4, (Seventh-day Adventist Publishing Association, 1864), pp. 148-149. [↵]
- White, Counsels on Diet and Foods, (Review and Herald Publishing Association, 1938), pp. 353,395. [↵]
- White, The Ministry of Healing, p. 112. [↵]
- White, Testimonies for the Church, Vol. 9, (Pacific Press Publishing Association, 1909), p. 163. [↵]
- White, The Ministry of Healing, (Pacific Press Publishing Association, 1905), p. 296. [↵]
- White, Testimonies for the Church Vol.1, (Pacific Press Publishing Association, 1865), p. 618. [↵]
- https://www.smithsonianmag.com/innovation/how-19th-century-activists-ditched-corsets-for-one-piece-long-underwear-180976774/ [↵]
- White, The Health Reformer, December 1, 1871. [↵]
- White, Letter 85, May 10, 1888. [↵]
- White, Mind Character, and Personality, Vol.1, (Southern Publishing Association, 1977), pp. 115-122. [↵]
- White, Testimonies for the Church, vol. 3, p. 76. [↵]
- Drugs And Their Manufacture In The Nineteenth Century: https://collections.countway.harvard.edu/onview/exhibits/show/apothecary-jars/nineteenth-century-drugs [↵]
- White, The Ministry of Healing, pp.127-128. [↵]
- White, Selected Messages Book 2, (Review and Herald Publishing Association, 1958), p. 288. [↵]
- Ibid., pp. 281-284. [↵]
- White, Testimonies for the Church, Vol. 6, (Pacific Press Publishing Association, 1901), pp. 288-291. [↵]
- https://www.medicalnewstoday.com/articles/personal-hygiene [↵]
- https://www.mayoclinic.org/healthy-lifestyle/fitness/in-depth/exercise/art-20048389 [↵]
- https://www.health.harvard.edu/staying-healthy/how-much-water-should-you-drink [↵]
- https://www.webmd.com/sleep-disorders/benefits-sleep-more [↵]
- https://www.healthline.com/health/depression/benefits-sunlight [↵]
- https://minnesota.cbslocal.com/2022/01/11/what-are-the-health-benefits-of-fresh-air/ [↵]
- https://my.clevelandclinic.org/health/articles/17488-smoking [↵]
- https://www.cdc.gov/alcohol/about-alcohol-use/ [↵]
- https://www.nationalgeographic.com/books/article/5-blue-zones-where-the-worlds-healthiest-people-live [↵]
- https://www.encyclopedia.com/social-sciences-and-law/sociology-and-social-reform/social-reform/temperance-movements [↵]
- Housel, Jemison, A Prophet Among You, (Pacific Press Publishing Association, 1955), p. 230. [↵]
- https://www.encyclopedia.com/people/social-sciences-and-law/social-reformers/sylvester-graham [↵]
- https://www.churchofjesuschrist.org/study/manual/gospel-topics/health?lang=eng [↵]
Majibu Zaidi
Hatua Kuelekea kwa Kristo: Mwongozo wa Uhusiano na Yesu
Iwe unanza safari yako na Yesu Kristo, unarejea baada ya muda fulani, au umekuwa na uhusiano na Yesu kwa miaka, kutumia kitabu
Wafahamu Watoto wa Ellen White
Ellen White, ambaye ni mmoja wa waanzilishi maarufu zaidi wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, alikuwa na watoto wanne na mumewe, James: Henry Nichols, James Edson, William Clarence, na John Herbert.
Jinsi Mafundisho ya Ellen White Yanavyoweza Kuboresha Afya Yako
Matibabu katika karne ya kumi na tisa yalisemekana kuacha “ugonjwa zaidi kuliko yalivyotibu” kwa matumizi yake ya kutoa damu na “dawa” kama zebaki na arseniki.
Ellen White anasema nini kuhusu Maombi?
Je, umewahi kuwa na mzigo ambao ulihitaji kumwambia mtu, lakini uliogopa kuhukumiwa ikiwa ungefanya hivyo?
Ellen G. White au Biblia—Kipi ni Muhimu Zaidi kwa Waadventista?
Biblia—bila shaka—ndiyo kitabu muhimu zaidi. Ni kipimo tunachotumia kupima maandishi mengine yote, ikiwa ni pamoja na yale ya Ellen White.
Ellen G. White Alisaidia Vipi Katika Kuanzisha Kanisa la Waadventista wa Sabato?
Ellen G. White, mwanamke mnyenyekevu kutoka Gorham, Maine, alikuwa mmoja wa waanzilishi wa Kanisa la Waadventista wa Sabato na kiongozi muhimu tangu mwanzo wake.
Ellen White na Kitabu cha Pambano Kuu
Pambano Kuu ni moja ya vitabu vya Ellen G. White vinavyo thaminiwa zaidi na Waadventista wa Sabato.
Roho ya Unabii Ni nini (Kitabu cha 1-4) na Ellen G. White?
Kutumia unabii wa Biblia katika historia, matukio ya hivi karibuni, na hasa siku za usoni, inaweza kuwa kazi ngumu. Hata linaweza kuwa jambo la kutisha kidogo kwa baadhi.
Ellen White Alifundisha nini Kuhusu Matumizi ya Vyakula Vinavyotokana na Mimea?
Moja ya mambo ambayo unaweza kuwa umewahi kusikia kuhusu Waadventista wa Sabato ni msisitizo wao kwenye mtindo wa maisha wa kutumia vyakula vinavyotokana na mimea.











