Matibabu katika karne ya kumi na tisa yalisemekana kuacha “ugonjwa zaidi kuliko yalivyotibu” kwa matumizi yake ya kutoa damu na “dawa” kama zebaki na arseniki.1 Watu walipoanza kuhoji njia hizi, njia mpya zilijitokeza. Lakini ni zipi zilikuwa za kuaminika?
Kati ya mchanganyiko huu wa mawazo, Kanisa la Waadventista Wa Sabato lilikuwa na sauti ya wazi kupitia ushauri uliovuviwa na Roho wa Unabii wa Ellen White. Mafundisho yake ya afya yenye upole yalikuwa ya kimapinduzi katika jinsi yalivyovuka maoni tofauti, na tangu hapo yamekuwa yakithibitishwa kupitia wakati na sayansi.
Mafundisho mengi haya yalitokana na maono aliyopokea kutoka kwa Roho Mtakatifu, yakifunua njia za kukuza jamii yenye afya na usawa. Ili kupata ufahamu bora wa maono aliyokuwa nayo na jinsi habari hio ilivyojaribiwa, tutajibu maswali yafuatayo:
Maono ya Ellen White kuhusu afya yalihusu nini?

Courtesy of the Ellen G. White Estate, Inc.
Ellen White alipata maono manne kuhusu afya—mnamo 1848, 1854, 1863, na 1865. Kupitia hayo, Roho Mtakatifu alimwonyesha athari ya afya ya kimwili kwa ustawi wa kiroho na kiakili. Maono hayo pia yalifunua kanuni muhimu (ingawa mara nyingi hupuuzwa) za mtindo wa maisha na kuwaita wafuasi wa Yesu kuakisi huduma yake ya uponyaji kupitia elimu ya afya na kazi ya matibabu.
Waadventista wanaita ushauri huu “ujumbe wa afya” au “sheria za afya.
Muktadha wa maono
Ellen White alipokea maono yake wakati jamii kwa ujumla ilikuwa imechanganyikiwa kuhusu afya na tiba. Ujumbe wake—wa kimapinduzi wakati huo—uliwasaidia Waadventista kushinda mchanganyiko huo.
Hapa kuna historia kidogo.
Katika miaka ya mwanzoni ya 1800, tiba haikuwa na msingi wa kisayansi na mara nyingi ilisababisha madhara zaidi kuliko manufaa. Madaktari wengi waliamini kwamba wangeweza kuponya ugonjwa kwa kuvunja mwili na kisha kuujenga upya. Kufanya hivyo, walitumia kutoa damu, kusafisha mwili, au kutibu magonjwa mbalimbali kwa zebaki, arseniki, opiumu, au kalomeli.2
Hata walidhani tumbaku ingeponya mapafu!3
Afya ilikuwa na changamoto katika Kanisa la Waadventista wa Sabato pia, hata miongoni mwa viongozi wake. Baadhi yao walikunywa pombe na kuvuta tumbaku.4 Kiongozi mmoja, J. N. Andrews, alielezea lishe yake: nyama ya nguruwe kwa namna mbalimbali, soseji, donati, biskuti, na jibini ya zamani.5
Katika muktadha huu, ushauri wa Ellen White ulionekana kuwa wa kipumbavu. Lakini baadaye iligundulika kuwa, ulikuwa tu mbele sana katika wakati wake.
Kusudi la maono6
Miongozo ya Ellen White hutoa mtazamo kamilifu wa afya na kuiweka ndani ya lengo la Kanisa la Waadventista Wa Sabato.
Yanaonyesha kwamba Mungu anataka kutuponya kimwili, kiroho na kiakili ili tuweze kuishi maisha bora na kumtumikia kwa ufanisi zaidi. Afya ni njia moja ambayo Kanisa la Waadventista Wa Sabato linaweza kutimiza lengo lake la “kumtukuza” Mungu (Ufunuo 14:7; 1 Wakorintho 10:31).
Na kupitia ujumbe wa afya, lengo letu ni kuakisi kazi ya Yesu ya kupunguza mateso na kushiriki ukweli wa kiroho.
Maono haya yalikuwaje?
Ellen White alipokea maono manne ambayo yalishughulikia mada za afya. Tutagusa mambo muhimu ya kila moja.
Maono ya kwanza ya afya (1848)7

Photo by Shaun Meintjes on Unsplash
Katika maono ya kwanza ya Ellen White kuhusu afya, Roho Mtakatifu alimwonyesha hatari za tumbaku, pamoja na athari mbaya ambazo kafeini inaweza kusababisha.
Alionya kuhusu athari mbaya za tumbaku kwa afya ya akili na kiroho, akizungumzia hasa tabia yake ya kuwa ya kuleta uraibu. Inaweza hata kuwa kitu kinachoweza kusimama katikati ya uhusiano wa mtu na Mungu.”
Maono ya pili ya afya(1854)
Maono ya pili yalihusu usafi wa msingi na kusafisha nyumba. Pia yalileta faida za chakula cha kawaida, tofauti na chakula “tajiri” (kama vile keki, pai, pastries, vyakula vyenye viungo vingi na viungo vya pilipili, jibini, siagi, na viungo).
Kumbukumbu ya maono ya Ellen White ilichapishwa katika hati.
Maono ya tatu ya afya (1863)
Courtesy of the Ellen G. White Estate, Inc.
Maono kuhusu matengenezo ya afya ya Ellen White yaliyokuwa kamili zaidi yalitokea Otsego, MI, na yalidumu kwa dakika 45. Yalihimiza uhusiano kati ya afya na maisha ya kiroho, huku pia yakijadili kanuni za kuishi kiafya.
Mungu alimpa ujumbe huu wakati mume wake James White alikuwa na msongo, mgonjwa, na ameishiwa nguvu kabisa.8 Takribani theluthi mbili ya ujumbe huo ulikuwa ushauri kwa wawili hao.
Ushauri kama vile:
“Niliona kwamba sasa tunapaswa kufanya huduma maalum ya afya ambayo Mungu ametupa, kwa sababu kazi yetu bado haijakamilika. Hasa tunapaswa kuelekeza tahadhari yetu kwa afya yetu, na kutumia muda kujitolea kwa afya yetu ili tuweze kwa kiwango fulani kupona kutokana na athari za kufanya kazi kupita kiasi na kuchosha akili”.9
Sehemu iliyobaki ya maono ilihusisha kanuni za afya kwa ujumla, ambazo aliziandika katika sura ya 39 ya Karama za Roho, kitabu cha 4a.
Hapa kuna muhtasari wake mfupi:
- Uhusiano wa afya na maisha ya kiroho
- Uhusiano kati ya mtindo wa maisha na magonjwa
- Madhara mabaya ya pombe, tumbaku, vinywaji vinavyochochea hisia, na chakula tajiri
- Kiasi (udhibiti wa nafsi) katika kila eneo la maisha – kula, kunywa, na kufanya kazi
- Lishe rahisi linalotokana na mimea
- Kuepuka nyama najisi, kama vile nguruwe, kulingana na Mambo ya Walawi 11
- Usafi na nadhifu
- Nguvu ya mazoezi inayoponya, maji safi, hewa safi, na jua
- Athari ya dawa za kulevya za burudani (hasa zile zilizotumiwa wakati wa Ellen White)
- Nguvu ya akili na umuhimu wa mtazamo mwema
- Jukumu la matengenezo ya afya katika utume wa Waadventista wa Sabato
Maono ya nne ya afya (1865)
Maono ya afya ya nne na ya mwisho ya Ellen White ilikuwa wito kutoka kwa Mungu kwa Waadventista kuanzisha kituo chao wenyewe cha kuendeleza kanuni za afya na kusaidia wagonjwa kupona.
Lakini kwa nini Waadventista walihitaji kituo chao cha afya?
James na Ellen White walitumia muda katika kituo cha afya huko Dansville, New York, baada ya James kupatwa na kiharusi. Kituo hiki kilikuza mawazo mengi ambayo Waadventista waliamini: lishe inayotokana na mimea, kujiepusha na pombe na tumbaku, na matumizi ya hidroterapia (matibabu kutumia maji).
Lakini Ellen White alikuwa na wasiwasi kuhusu baadhi ya vipengele vya programu hiyo, hasa kutokuwepo kwa uhusiano kati ya imani ya kidini na uponyaji.
Waadventista walihitaji mahali ambapo wangeweza kuwatunza wagonjwa na kufundisha matengenezo ya afya katika muktadha wa imani yao.10 Hii ilipelekea kuanzishwa kwa Taasisi ya Matengenezo ya Afya ya Magharibi (baadaye ilijulikana kama Sanitarium ya Battle Creek).
Vitabu gani vilitokana na maono ya Ellen White kuhusu afya?11
Kama Ellen White alipokea mwongozo kuhusu mada mbalimbali za afya, alianza kuziandika katika makala na vipeperushi ili ziweze kushirikishwa na wengine. Hatimaye, vipande hivyo vidogo viligeuka kuwa vitabu vikubwa. Hapa ni maandishi ya awali yaliyoandikwa kulingana na maono yake kuhusu afya:
Wito kwa Akinamama (1864)
- “Afya,” Karama za Roho, kitabu cha 4a (1864)
- “Ugonjwa na Sababu Zake” katika kitabu Afya, au Namna ya Kuishi (1865)
- Kiasi na Usafi wa Kibiblia (1890)
Mwaka wa 1905, alikusanya mafundisho yake kuhusu afya na ustawi katika kitabu kikubwa, Huduma ya Uponyaji.
Na mwaka wa 1897, daktari mmoja aliyeitwa David Paulson alikusanya muhtasari wa mafundisho yake kuhusu afya katika kitabu kiitwacho, Kuishi Kiafya.
Mjumuisho mwingine wa vitabu—ulioandaliwa na wadhamini wa Mali ya Ellen G. White baada ya kifo chake—ni:
Mashauri Kuhusu Afya (1923)
Huduma ya Matibabu (1932)
Mashauri Kuhusu Lishe na Vyakula (1938)
Kiasi(1949)
Tunaweza kujifunza nini kutoka maono ya Ellen White kuhusu afya?
Maono ya Ellen White hutoa kanuni za kivitendo kwa maisha yenye afya, ambazo Waadventista wanaziita ujumbe wa afya. Tunaendelea kufuata kanuni hizi kwa imani kuu zaidi kwa sababu ya jinsi sayansi inavyozithibitisha leo.
Hebu tuangalie baadhi ya kanuni muhimu:
Afya ya mtu katika ukamilifu

Photo by Nathan Dumlao on Unsplash
Katika maono yake, Ellen White aliona uhusiano kati ya afya ya kimwili, kiakili, na kiroho. Jinsi tunavyojali miili yetu inaathiri akili zetu na uhusiano wetu na Mungu.
“Uhusiano uliopo kati ya akili na mwili ni wa karibu sana. Wakati mmoja unaathiriwa, mwingine hujisikia hivyo hivyo. Hali ya akili inaathiri afya ya mfumo wa kimwili”.12
Chakula cha mimea na kuepuka nyama ya nguruwe
Linapokuja swala la chakula, “nafaka, matunda, karanga, na mboga zinaunda chakula kilichochaguliwa kwa ajili yetu na Muumba wetu. Vyakula hivi, vilivyo tayarishwa kwa njia rahisi na asilia iwezekanavyo, ndivyo vyenye afya na lishe zaidi.”13
Sayansi inathibitisha hili kwa kuonyesha jinsi lishe inayotegemea mimea inavyosaidia kuzuia magonjwa sugu – kansa, kisukari, na zaidi.14
Angalia jinsi daktari na mwandishi Dk. Greger alivyojibu alipoulizwa ni aina gani ya lishe linanalolinda dhidi ya magonjwa:
“Ni lishe linalopunguza ulaji wa nyama, mayai, maziwa, na taka na kuongeza ulaji wa matunda, mboga, nafaka nzima, maharage au maharagwe, njegere, dengu, choroko, karanga, mbegu, mimea, viungo, na uyoga – kimsingi chakula halisi kinachomea ardhini sio katika kiwanda. Hizo ndizo chaguzi zetu za kiafya zaidi.”
Inasikika kama kile ambacho Ellen White aliandika, sio?
Anasisitiza utafiti wa kisasa kuhusu hatari za nyama ya nguruwe pia:
“Kwa hivyo, nyama ya nguruwe nchini Marekani ina uchafu kiasi gani? Consumers Union ilipima karibu sampuli 200 za nyama ya nguruwe kutoka miji mbalimbali nchini, na kugundua zaidi ya theluthi mbili zilikuwa na Yersinia—90% ambavyo vilikuwa sugu kwa dawa moja au zaidi ya kuua viini hivyo”.
Na kufikiria kwamba Ellen White aliandika hili zaidi ya miaka 150 iliyopita:
“Nyama ya nguruwe, ingawa ni moja ya vitu vya kawaida sana kwenye chakula, ni moja ya vitu vya kudhuru zaidi. Mungu hakukataza…kula nyama ya nguruwe tu kwa ajili ya kuonyesha mamlaka Yake, bali kwa sababu haikuwa kitu sahihi cha chakula kwa mwanadamu.”15
Vitu na shughuli za kudhuru
Maonyo ya Ellen White dhidi ya vitu na shughuli zenye madhara bado ni muhimu leo.
Hizi ni pamoja na:
- Uvutaji wa sigara/Tumbaku: “Tumbaku ni sumu yenye hila na yenye kudhuru sana, ikiwa na athari ya kusisimua, kisha ya kulemaza, kwenye mishipa ya mwili. Ni hatari zaidi kwa sababu athari zake kwenye mfumo wa mwili ni za polepole sana, na mwanzoni sio rahisi kuziona.”16
- Pombe: “Athari za vinywaji vya kulevya ni kudhoofisha mwili, kuchanganyikiwa kwa akili, na kuharibu maadili.”17
- Kufanya kazi kupita kiasi: “Tunapaswa kuwa na kiasi katika kazi zetu. Sio jukumu letu kujiweka mahali ambapo tutafanya kazi kupita kiasi. Baadhi wanaweza wakati mwingine kuwekwa mahali ambapo hili ni lazima, lakini inapaswa kuwa kwa nadra, sio jambo la kawaida.”18
- Kula kupita kiasi: “Kuna ubaya katika kula kupita kiasi hata chakula chenye afya…. Ikiwa tunakula kupita kiasi, nguvu ya ubongo inaathiriwa kwa kushughulikia wingi wa chakula ambacho mfumo hauhitaji, akili inafifia, na uwezo wa kufikiri unadhoofika.”19
- Usafi duni: “Usafi unapaswa kuzingatiwa kwa uthabiti. Wengi, hali wakiwa na afya njema, hawajishughulishi kujiweka katika hali ya afya. Wanapuuza usafi binafsi, na hawatilii maanani kuweka nguo zao safi. Uchafu unapita kwa wingi na bila kugundulika kutoka mwilini, kupitia vinyweleo, na ikiwa sehemu ya juu ya ngozi haitunzwi katika hali ya afya, mfumo unachoshwa na mambo machafu.”20
Tiba za asili

Photo by Eric Prouzet on Unsplash
Ellen White aliandika, “Hewa safi, jua, kiasi katika kula na kunywa, kupumzika, mazoezi, lishe sahihi, matumizi ya maji, imani katika nguvu ya kiungu—hizi ndizo dawa halisi.”21
Ingawa hakupuuza matibabu maalum, alifundisha kwamba tunahitaji kufikia chanzo cha ugonjwa—mara nyingi ni mtindo wa maisha—badala ya kupigana tu na dalili. Leo, jamii ya kitabibu inatambua uhusiano huu kati ya mtindo wa maisha na magonjwa.
Daktari Josh Axe, daktari maarufu wa tiba asilia, mganga wa mifupa, na mtaalamu wa lishe kliniki, anasisitiza kanuni hii pia:
“Nadhani swali muhimu sana la kumwuliza daktari wako ni, ‘Nini chanzo cha hali yangu?'”
Ili kujifunza zaidi kuhusu dawa za asili hizi, angalia makala yetu kuhusu ufupisho wa NEWSTART kwa maisha yenye afya.
Mtazamo mwema
Kutokana na uhusiano mkubwa kati ya akili na mwili, mtazamo una jukumu muhimu katika uponyaji. Ndiyo maana Mungu alitoa ushauri ufuatao kwa James na Ellen White:
“Tunapaswa kuhamasisha mtazamo wa furaha, matumaini, na amani, kwa sababu afya yetu inategemea kufanya hivyo.”
Sasa tunajua kwamba mtazamo mwema husaidia uponyaji kutokana na majeraha au ugonjwa.
Huduma ya kushiriki ujumbe wa afya
Courtesy of the Ellen G. White Estate, Inc.
Huduma ya afya ina msisitizo muhimu katika Kanisa la Waadventista wa Sabato kutokana na mashauri ya Ellen White. Kwa kila namna, Waadventista wanataka “kuifanya dunia iwe bora kwa kuwa wameishi ndani yake.”22
Kivipi?
Moja ya njia ni kwa kuunganisha kanuni za Biblia na uponyaji, kama Yesu alivyofanya. Kila mshiriki anaweza kuwa mmishonari wa matibabu kwa kuuelewa mwili na kujifunza jinsi ya kutumia tiba za asili.23
Ellen White pia alihimiza kanisa kuanzisha:
- Maduka na wazalishaji wa chakula cha afya
- Mikahawa ya vyakula vya mimea
- Vituo vya afya
- Vitu vya mafunzo ya afya
- Kliniki
Kupitia hivi “vituo vya mvuto,” alitazamia madaktari, wachungaji, na washiriki wa kanisa kufanya kazi pamoja kutoa elimu ya afya na uponyaji.24
Je, kufuata ujumbe wa afya ni njia ya kupata wokovu?
Hapana, kufuata ujumbe wa afya hakuhusu kupata wokovu au kibali kwa Mungu. Badala yake, Waadventista wanachukulia kuishi kwa afya njema kama njia ya kumheshimu Mungu na kutimiza vyema wajibu wao katika ulimwengu huu.
Imani kuhusu afya ni imani binafsi. Hatupaswi kuhukumu tabia au uhusiano wa mtu na Mungu kulingana na afya yao.
Hata Ellen White mwenyewe hakujiweka kama kigezo kwa wengine. Aliwahimiza watu kwa sala kuchunguza kwa makini Neno la Mungu na ushauri wa afya ili kujua jinsi wanavyoweza kuwa mawakili bora wa miili yao.
Unataka kujaribu kanuni hizi za afya?
Mungu anajali sana hali yetu ya kiafya. Ndiyo maana alitumia mashauri ya Ellen White kuwaongoza watu kurudi kwenye falsafa rahisi, ya Kibiblia ya afya.
Na leo, sayansi inakubaliana, ikituwezesha kuwa na ujasiri mkubwa katika yale Mungu anayosema!
Waadventista wanathamini ujumbe huu wa afya kwa sababu sio tu unawanufaisha katika maisha yao binafsi bali pia kuwaleta karibu na Yesu na kuunda utume wetu wa kuwaambia watu kumhusu.
Na Mungu anaweza kutumia hii kubadilisha maisha yako pia! Kwa nini usijaribu mafundisho ya Ellen White na uone jinsi yanavyoweza kufaidisha afya yako mwenyewe.
Makala yanayohusiana
- Bigelow, Jacob, M.D., Brief Exposition of Rational Medicine (Philips, Samson, and Co., Boston, 1858), pp. 62–63. [↵]
- Robinson, Doris, The Story of Our Health Message (Southern Publishing Association, Nashville, TN, 1965), pp. 17–22. [↵]
- Douglass, Herbert, Messenger of the Lord (Nampa, Idaho, Pacific Press, 1998), p. 289. [↵]
- Robinson, pp. 63–64. [↵]
- Ibid., p. 26. [↵]
- “Health Reform,” Fortin and Moon, The Ellen G. White Encyclopedia (Review and Herald, Hagerstown, MD, 2014). [↵]
- Robinson, pp. 65–66. [↵]
- Ibid., p. 76. [↵]
- White, Ellen, Manuscript 1, 1863. [↵]
- Purpose and Objectives of Seventh-day Adventist Institutions, p. 64–69. [↵]
- Levterov, Theodore, “The Ministry of Healing,” Encyclopedia of Seventh-day Adventists, Jan. 29, 2020. [↵]
- Counsels on Health, p. 28 [↵]
- White, Ellen, The Ministry of Healing (Pacific Press, Mountain View, CA, 1905), p. 296. [↵]
- Miles et. al., “Plasma, Urine, and Adipose Tissue Biomarkers of Dietary Intake Differ Between Vegetarian and Non-Vegetarian Diet Groups in the Adventist Health Study-2,” The Journal of Nutrition, vol. 149(4), April 2019, pp. 667–675. [↵]
- White, Ellen, Counsels on Diet and Foods (Review and Herald Publishing Association, Washington, D.C., 1938), p. 392. [↵]
- White, Ellen, Spiritual Gifts, vol. 4a (Seventh-day Adventist Publishing Association, Battle Creek, MI, 1864), p. 128. [↵]
- White, Ellen, Temperance (Pacific Press, Mountain View, CA, 1949), p. 268. [↵]
- Ibid., p. 139. [↵]
- White, Ellen, Healthful Living (Medical Missionary Board, Battle Creek, MI, 1897), p. 88. [↵]
- Ibid., p. 143. [↵]
- White, The Ministry of Healing, p. 27. [↵]
- Ibid., p. 398. [↵]
- White, Ellen, Testimonies for the Church, vol. 7 (Pacific Press, Mountain View, CA, 1902), p. 62. [↵]
- White, Ellen, Counsels on Health (Pacific Press, Mountain View, CA, 1923), p. 493. [↵]
Majibu Zaidi
Hatua Kuelekea kwa Kristo: Mwongozo wa Uhusiano na Yesu
Iwe unanza safari yako na Yesu Kristo, unarejea baada ya muda fulani, au umekuwa na uhusiano na Yesu kwa miaka, kutumia kitabu
Wafahamu Watoto wa Ellen White
Ellen White, ambaye ni mmoja wa waanzilishi maarufu zaidi wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, alikuwa na watoto wanne na mumewe, James: Henry Nichols, James Edson, William Clarence, na John Herbert.
Jinsi Ellen White Alivyochangia Ujumbe wa Afya wa Waadventista
Jinsi Ellen White Alivyochangia Ujumbe wa Afya wa WaadventistaWaadventista wa Sabato wanajulikana kwa kusisitiza maisha yenye afya bora. Na Ellen G. White alikuwa na ushawishi mkubwa katika maendeleo ya kipaumbele hiki na utekelezaji wake miongoni mwa Waadventista....
Ellen White anasema nini kuhusu Maombi?
Je, umewahi kuwa na mzigo ambao ulihitaji kumwambia mtu, lakini uliogopa kuhukumiwa ikiwa ungefanya hivyo?
Ellen G. White au Biblia—Kipi ni Muhimu Zaidi kwa Waadventista?
Biblia—bila shaka—ndiyo kitabu muhimu zaidi. Ni kipimo tunachotumia kupima maandishi mengine yote, ikiwa ni pamoja na yale ya Ellen White.
Ellen G. White Alisaidia Vipi Katika Kuanzisha Kanisa la Waadventista wa Sabato?
Ellen G. White, mwanamke mnyenyekevu kutoka Gorham, Maine, alikuwa mmoja wa waanzilishi wa Kanisa la Waadventista wa Sabato na kiongozi muhimu tangu mwanzo wake.
Ellen White na Kitabu cha Pambano Kuu
Pambano Kuu ni moja ya vitabu vya Ellen G. White vinavyo thaminiwa zaidi na Waadventista wa Sabato.
Roho ya Unabii Ni nini (Kitabu cha 1-4) na Ellen G. White?
Kutumia unabii wa Biblia katika historia, matukio ya hivi karibuni, na hasa siku za usoni, inaweza kuwa kazi ngumu. Hata linaweza kuwa jambo la kutisha kidogo kwa baadhi.
Ellen White Alifundisha nini Kuhusu Matumizi ya Vyakula Vinavyotokana na Mimea?
Moja ya mambo ambayo unaweza kuwa umewahi kusikia kuhusu Waadventista wa Sabato ni msisitizo wao kwenye mtindo wa maisha wa kutumia vyakula vinavyotokana na mimea.











