Ikiwa Biblia haijawahi kutaja mabadiliko ya Sabato, kwa nini leo wengi wanaenda kanisani Jumapili?
Nani alibadilisha siku hiyo?
Lakini hilo sio swali sahihi la kuuliza. Sabato haijabadilika.
Kilichobadilika ni uamuzi wa Wakristo wa siku ya kuabudu. Na yote ilianza wakati wa karne ya kwanza na ya pili. Hebu tuangalie zaidi ya hadithi kwa kuchunguza:
- Sabato ya siku ya saba ilianzia wapi
- Jinsi Sabato ilivyotunzwa katika Biblia
- Jinsi Wakristo walivyohamia kutunza Jumapili
Bila kuchelewa, hapa kuna ukumbusho kidogo kuhusu Sabato mpaka wakati wa Agano Jipya. Kutoka hapo, tutagundua kilichotokea katika karne za mapema za Ukristo.
Sabato ya siku ya saba ilianzia wapi

Photo by Javier Miranda on Unsplash
Sabato ya saba ya siku saba imeunganishwa na ubinadamu tangu Mungu alipowapa wanadamu aliowaumba kama siku ya kupumzika. Watu wameendelea kutunza Sabato tangu wakati huo: Waisraeli walifanya hivyo, Yesu alifanya hivyo, mitume walifanya hivyo, na watu wengi waaminifu baada ya wakati huo walifanya hivyo.
Lakini yote hayo yalianza wakati ambapo hapakuwa na Wayahudi au makundi mbalimbali ya watu au makanisa. Kulikuwa na Mungu tu na wanadamu wa kwanza wawili: Adamu na Hawa.
Mungu alipomaliza kuumba ulimwengu katika siku sita, “Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa, kwa sababu katika siku hio Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya” (Mwanzo 2:3, NKJV).
Aliifanya Sabato kama wakati wa kutulia—kujielekeza upya kwake na kwa wenzetu. Tumeumbwa kwa ajili ya mzunguko huu.
Jinsi Sabato ilivyotunzwa katika Biblia
Kote katika Agano la Kale na Agano Jipya kuna mifano ya watu waliotunza Sabato ya siku ya saba.
Mungu aliwakumbusha watu wake kuhusu Sabato alipompa Musa Amri Kumi. Amri ya nne kuhusu Sabato ilianza kwa maneno maalum “Ikumbuke” (tofauti na amri nyingine yoyote).
Mungu alikuwa amewaleta Waisraeli kutoka Misri, walipokuwa watumwa. Baadhi yao bila shaka walikuwa wamesahau kanuni hizi, lakini kama watumwa, pia wasingeweza kufurahia siku ya mapumziko kila wiki. Kukumbushwa na Mungu kungetokea kama zawadi ya ukaribisho. Pia ingewalazimu kujifunza upya maana ya kuwa na mfumo wa kazi na mapumziko ya kila wiki.
Ndiyo maana kati ya maagizo ya kumpenda Yeye na kupendana sisi kwa sisi (Mathayo 22:38–40), alisema,
“Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote…. Maana kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; Kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa” (Kutoka 20:8–11, NKJV).
Watu wa Israeli waliendelea kutunza Sabato katika Agano la Kale.
Kisha, katika Agano Jipya, Yesu anaingia katika eneo hilo.
Yesu angeweza kubadilisha Sabato kama angependa. Hakika hakuogopa kuwaonyesha Mafarisayo kwamba walikuwa wamegeuza Sabato kuwa siku ya kazi ngumu na sheria badala ya huruma na ukarimu (Marko 2:4).
Bado, Yesu alithibitisha Sabato (Luka 4:16), hata akijitangaza mwenyewe kuwa “Bwana wa Sabato” (Marko 2:28, NKJV). Aliweka wazi kwamba hakuja kuharibu Sheria ya Mungu bali kuishi kwa mfano wake, kutuwekea sisi mfano (Mathayo 5:17–19).
Mitume katika karne ya kwanza, ikiwa ni pamoja na Paulo, walitunza Sabato pia. Na waliandika kuhusu umuhimu wa Amri Kumi na pumziko la Sabato lililosalia (Yakobo 2:10–11; Waebrania 4:4, 9).
Lakini kama ilivyo kawaida ya asili ya binadamu, baadhi ya Wakristo waligeuza Sabato kuwa mazoea ya kisheria badala ya sherehe ya furaha kama iliyokusudiwa iwe.
Uvurugaji huu wa Sabato ulichangia kupelekea watu kutunza Jumapili.
Jinsi Wakristo walivyohamia kutunza Jumapili
Baada ya Yesu kurudi mbinguni (31 BK), wanafunzi na kanisa la Kikristo la awali (Wayahudi na watu wa Mataifa) waliendelea kutunza Sabato. Walifanya hivyo wakati wote wa kitabu cha Matendo na karne ya kwanza.
Mwanahistoria Lyman Coleman katika kitabu chake cha Ancient Christianity Exemplified anasisitiza hili. Alichosema ni muhimu, ikizingatiwa kwamba yeye mwenyewe sio mtunza Sabato:
“Hakuna sheria au amri inayoonekana kutolewa na Kristo au mitume, ama ya kufuta Sabato ya Kiyahudi au kuanzisha siku ya Bwana, au kuchukua nafasi ya siku ya kwanza badala ya siku ya saba ya wiki.”1
Licha ya kutokuwa na maagizo yoyote kutoka kwa Kristo au mitume, baadhi ya mababa wa kanisa la awali (viongozi) wa karne ya pili walianza kubadilisha siku yao ya ibada kutoka Jumamosi kwenda Jumapili.
Tujaribu kugundua sababu halisi ya mabadiliko haya. Tutachunguza utafiti wa kihistoria ili kupata majibu.
Mababa wa Kanisa katika karne ya kwanza hadi ya tatu
Mabadiliko kutoka Sabato hadi Jumapili ilikuwa mchakato wa polepole uliodumu kwa mamia ya miaka kadhaa. Ilianza wakati Wakristo walipojumuisha falsafa za Kigiriki, Kirumi, na za kipagani katika Ukristo ili kujumuika na wale walio karibu nao na kujitenga na Uyahudi.
Angalia, Jumapili ilikuwa siku takatifu kwa dini nyingine nyingi kwa muda mrefu. Kwao, ilikuwa sherehe ya kuabudu jua—ambapo tunapata jina lake.2 Desturi hizi zinatoka nyuma sana na hata zinatajwa katika Agano la Kale (Ezekieli 8:15–17).
Wakristo kuabudu Jumapili “kunahusishwa na karne ya pili au ya tatu” na “kulihusishwa na Roma au Aleksandria.”3
Mmoja wa marejeo ya kwanza ni katika BK 155 na mmoja wa mababa wa kanisa, Justin Martyr, katika utetezi wa Ukristo kwa mfalme wa Kirumi:
“Lakini Jumapili ndiyo siku ambayo sote tunakusanyika pamoja, kwa sababu ni siku ya kwanza ambayo Mungu, baada ya kufanya mabadiliko katika giza na vitu, aliumba ulimwengu; na Yesu Kristo Mwokozi wetu siku hiyo hiyo alifufuka kutoka kwa wafu.”4
Inawezekana alitarajia kuwapa Wakristo upendeleo mbele ya mfalme na kupunguza mateso.
Justin Martyr, ambaye alitumia muda wake huko Rumi, alitoka katika asili ya kipagani na alikuwa amejifunza falsafa za Stoic, Platonic, na kipagani nyingine. Wakati wa uhai wake, Jumapili ilikuwa sherehe ya kipagani kumheshimu mungu wa jua, lakini Wakristo walikuwa wameanza kusherehekea Jumapili kama njia ya kuwaunganisha na dini hizi nyingine na kwa matumaini ya kuwabadilisha kuwa Wakristo.5
Lakini ikiwa Wakristo walifanikiwa katika jitihada zao ni swala linalotatiza, hasa tunaposoma maneno ya mwandishi Mkristo Tertullian kutoka miaka takriban 60 baada ya Justin Martyr.
Kwa kushangaza, Tertullian, baba mwingine wa kanisa, alionekana kujipinga aliposema kuhusu Sabato. Alisema Neno la Mungu halikutoa ushahidi wowote kwamba “Sabato ya Muumba” ilikuwa imebadilika, na aliamini ilikuwa kazi ya adui kupata njia za kuepuka kutunza Sabato.
Na bado, Tertullian pia alitetea ibada ya Jumapili aliposhutumiwa kwa kuabudu jua badala ya Mungu siku hiyo.6
Sabato na Jumapili kwa pamoja

Photo by Chandan Chaurasia on Unsplash
Wapagani katika Utawala wa Rumi walisherehekea ibada ya jua kila Jumapili. Kwa muda, Wakristo, wakivutwa na mtazamo wa Kirumi, walianza kuabudu siku ya Sabato pamoja na Jumapili.
Hata hivyo, Jumapili haikuonekana kama mbadala wa Sabato—kama “Sabato ya Kikristo.” Badala yake, ilionekana kama sherehe ya ziada. The Apostolic Constitutions, kipande cha fasihi ya Kikristo ya awali kutoka karne ya nne, kinaelekeza hivi:
“Lakini tunza Sabato, na sherehe ya siku ya Bwana; kwa sababu ya kwanza ni kumbukumbu ya uumbaji, na ya pili ya ufufuo.”7
Lakini katika mchakato huo, Sabato ilikuwa inapotoshwa. Kama ilivyotokea wakati wa Yesu, viongozi wa kidini walioitwa Mafarisayo walikuwa wameweka sheria nyingi sana na kanuni kuzunguka Sabato hivyo kuitunza ikawa ni jambo la kuchosha badala ya furaha kama ilivyokuwa inatarajiwa kuwa (Isaya 58:13). Yesu alikuwa amewaonyesha watu njia tofauti ya kuitunza Sabato, lakini kwa bahati mbaya, hili lilipotea katika karne zilizofuata.
Hivi ndivyo ilivyokuwa, kulingana na mwanahistoria wa kanisa Dkt. Charles Hase wa Ujerumani:
“Wakati makanisa ya mashariki yalibaki kutunza Sabato, sehemu ya makanisa ya magharibi, pamoja na kanisa la Rumi kama kiongozi wao, waliigeuza kuwa siku ya kufunga.”8
Na wakati Sabato iligeuka kuwa siku ya kufunga, Jumapili ilikuwa siku ya kusherehekea. Hivyo, ikawa siku ya furaha na sherehe ya kutarajia baada ya Sabato kuisha.
Na kushika siku zote mbili kulikuwa jambo la kawaida hadi karne ya tano.
Tazama alichosema mwandishi wa historia Coleman kuhusu hilo:
“Kutunza siku ya Bwana kama siku ya kwanza ya juma ilianzishwa kwanza kama taasisi tofauti… Sabato yao, siku ya mwisho ya juma, ilitunzwa kwa uangalifu kwa muda mrefu baada ya kuangushwa kwa hekalu na ibada yake [BK 70]. Hata hadi karne ya tano, kutunza Sabato ya Kiyahudi kulionekana katika kanisa la Kikristo, kwa ukali na utakatifu ukipungua polepole hadi ikaachwaa kabisa.”
Kwa muda, wengi wa Wakristo walipoteza hamu katika kazi ngumu na kufunga siku ya Sabato, hivyo kuwafanya waweze kukubali kilichofuata kwa urahisi.
Sheria ya Jumapili ya Constantine

Photo by John Nail
Wakristo walipokuwa wakifanya maamuzi ya kutunza Sabato pamoja na Jumapili, jambo lisilotarajiwa lilitokea ndani ya Utawala wa Kirumi. Mapema katika karne ya nne, Kaisari Constantine alikuwa katika Vita vya Daraja la Milvian, alipokuwa na maono ya msalaba unaowaka na maneno ya Kilatini, “Kwa ishara hii, shinda.”9
Kufuatia hilo, yeye akawa Mkristo—na vivyo hivyo Utawala wake. Mabadiliko haya yalimaanisha mwanzo wa kanisa kuwa chini ya mamlaka ya Kirumi.10
Mabadiliko hayo bila shaka yalikuwa faraja kwa Wakristo ambao walikuwa wamepitia mateso makali chini ya utawala wa Kaisari Diocletian.
Mpaka wakati huu, Constantine alikuwa mfuasi wa Mithraism, dini moja ya kipekee ambayo ilihusisha ibada ya mungu jua. Inaonekana kwamba Mithraism ilipungua wakati Ukristo ulipoenea zaidi. Lakini kwa kweli, ilikuwa tu imepakwa rangi mpya. Tunaweza kuona hili katika amri ya Constantine ya Machi 7, 321:
“Siku takatifu ya Jua, maafisa na watu wanaoishi mijini wapumzike, na maduka yote yafungwe.”11
Ilikuwa hatua ya kisiasa sana—njia ya Constantine kuunganisha makundi tofauti ya kidini ndani ya Utawala wake na kuleta utulivu wa kijamii.
Eusebius, mwanahistoria Mkristo wakati huo, alikuwa na uhusiano wa karibu na mfalme na bila shaka alikuwa akitafuta njia za kumpendeza. Katika Komentari yake ya Zaburi, anadai hivi:
“Na vitu vyote vyote ambavyo ilikuwa ni wajibu kufanywa siku ya Sabato, hivi sasa tumevihamishia siku ya Bwana, kama vinavyostahili zaidi kuwa navyo, kwa sababu ina kipaumbele na ni ya kwanza kwa cheo, na ni ya heshima zaidi kuliko Sabato ya Kiyahudi.”12
Hata hivyo, kama tulivyotaja awali, kushika Sabato haikusimamishwa wakati huo. Ingechukua miaka mingine mia kadhaa kwa kanisa la Kikristo kuiweka rasmi.
Mabaraza ya karne ya nne

Photo by Fabio Fistarol on Unsplash
Baadhi ya mabaraza muhimu ya karne ya nne ndani ya kanisa lililokuwa chini ya udhibiti wa Warumi yalichochea njia ambayo Wakristo walishika Sabato. Kutunza Jumapili badala ya siku ya saba ilikuwa njia kwao ya kuweka umbali kati yao na Wayahudi.
Wakati wa Baraza la Nikea katika BK 325, mjadala ulizuka kuhusu iwapo kushika Pasaka kama Wayahudi. Tunashuhudia mtazamo wa kibaguzi dhidi ya Wayahudi katika jibu la Constantine, kama ilivyoandikwa na Eusebius:
“Kunaonekana jambo lisilostahili kwamba katika maadhimisho ya sikukuu hii takatifu sana [Pasaka] tunapaswa kufuata desturi za Wayahudi…. Basi tusiwe na chochote kinachofanana na umati wa Kiyahudi wa kuchukiza.”
Ni wazi, Constantine alikuwa na ajenda dhidi ya desturi za Kiyahudi, na Wakristo wangelazimika kufuata ili waendelee kukubalika.
Kisha, Baraza la Laodikea katika BK 365 lilijadili moja kwa moja kuhusu utunzaji wa Sabato. Lilikataza Wakristo, hasa katika kanisa la magharibi, kuitunza:
“Wakristo wasijitahidi kuwa Wayahudi kwa kupumzika siku ya Sabato, bali wafanye kazi siku hiyo, badala yake kuheshimu Siku ya Bwana, na, ikiwezekana, kupumzika wakati huo kama Wakristo. Lakini ikiwa yeyote atapatikana kuwa Mwayahudi, na awe laana kutoka kwa Kristo.”13
Kuanzia karne ya sita kuendelea, amri na mabaraza mengine ya kanisa lililodhibitiwa na Warumi yalikataza Wakristo kufanya kazi Jumapili au kutunza Sabato.14 Polepole, wale wanaoshika Sabato walipungua.
Lakini hawakutoweka kabisa.
Ukweli uliendelea kuishi
Mabadiliko kutoka utunzaji wa Sabato hadi kutunza jumapili yanafunua tabia ya mwanadamu ya kutaka kufuata mkumbo na kumpendeza binadamu wenzake kuliko Mungu. Yawezekana hatukubaliani na uongo moja kwa moja, lakini kwa muda, tunaweza kufanya mabadiliko madogo ambayo yanatupeleka kwenye njia ya kuacha ukweli.
Licha ya ukweli kwamba Wakristo kwa ujumla walifuata mwongozo wa Kanisa la Kirumi, baadhi ya makundi madogo, kama Kanisa la Kelti na Waaldensia wa Kaskazini mwa Italia, walibaki waaminifu kwa mafundisho na mfano wa Yesu.15
Ingawa ilifichwa kwa muda mrefu, ukweli wa Mungu haukutoweka kabisa.
Na pia ulikuja wakati kundi la Waprotestanti Wakristo walipojitokeza na kurudi katika maandiko ili kuchunguza tena.
Jifunze zaidi kuhusu jinsi Waadventista walivyogundua ukweli wa Sabato na kwa nini tunaitunza leo.
Kurasa zinazohusiana
- Coleman, Lyman, Ancient Christianity Exemplified (Lippincott, Grambo & Co, 1853), p. 530. [↵]
- Andrews, John Nevins, The History of the Sabbath, p. 146. [↵]
- McIver, Robert, “When, Where, and Why Did the Change from Sabbath to Sunday Worship Take Place in the Early Church?” [↵]
- Justin Martyr, First Apology 67. [↵]
- Andrews, p. 148. [↵]
- Ibid., p. 155. [↵]
- Ibid., p. 163. [↵]
- Quoted in Andrews, p. 156. [↵]
- Cavendish, Richard, “The Battle of the Milvian Bridge,” History Today. [↵]
- “Constantine the Great – Paganism to Christianity,” Lineage. [↵]
- Codex Justinianus 3.12.3, trans. Philip Schaff, History of the Christian Church, 5th ed. (New York, 1902), 3:380, note 1. [↵]
- Andrews, p. 200. [↵]
- Canon XXIX. [↵]
- Andrews, Chapter 19. [↵]
- “Waldensians: People of the Valleys,” Lineage. [↵]
Majibu Zaidi
Kila kitu unachohitaji kujua kuhusu Shule ya Sabato
Kila kitu unachohitaji kujua kuhusu Shule ya SabatoShule ya Sabato ndio sehemu ya kujifunza Biblia ya programu za kanisa katika makanisa mengi ya Waadventista wa Sabato. Ni wakati wa kujifunza Biblia kuhusu mada au somo fulani. Badala ya kumsikiliza mhubiri, watu...
Ninawezaje Kuanza Kutunza Sabato?
Sabato, inayokuja kila siku ya saba ya juma, ni siku maalum inayoheshimu amri ya nne na uumbaji wa Mungu.






