Kitabu cha Nyimbo cha Waadventista Wa Sabato 

Kitabu cha nyimbo cha Waadventista wa Sabato ni kitabu cha nyimbo kinachotumiwa ulimwenguni kote na makanisa mengi ya Waadventista wakati wa ibada zao. Tangu kuchapishwa kwake mwaka 1985, kimekuwa msaada mkubwa katika kutoa sifa kwa Mungu huku kikiwakumbusha washiriki wa kanisa juu ya utume wetu na kuwavuta karibu na Yesu.

Unapoingia katika Kanisa la Waadventista, utagundua kuwa watu wanaimba nyimbo kutoka kwenye vitabu hivi vyenye jalada gumu wakati wa huduma ya nyimbo—wakati wa kusifu Mungu kwa nyimbo katika programu kuu ya kanisa. Maneno yanaweza kuwa kwenye skrini mbele ya kanisa pia.

Hata unapotembelea nyumba za Waadventista, unaweza kuona kitabu cha nyimbo kwenye kabati la vitabu au piano.

Kwa kuwa ni jambo la uhakika utakutana na kitabu hiki wakati fulani, sasa ni wakati mzuri wa kukifahamu.
Tutakupa muhtasari:

Sasa tuanze.

Mahali utakapopata kitabu cha nyimbo cha Kiadventista leo

Hymnals resting in the backs of pews at an Adventist Church

Photo by CHUTTERSNAP on Unsplash

Sio jambo gumu kupata vitabu vya nyimbo vya Kiadventista! Angalia tu kabati ndogo au kifurushi nyuma ya kiti katika Kanisa la Waadventista wa Sabato la eneo lako. Unaweza kuwa na uhakika kwamba unaweza kukipata, pamoja na Biblia kadhaa na labda vitabu vingine vya nyimbo pia.

Lakini kama sivyo, habari njema ni kwamba kuna programu nyingi za bure za vitabu vya nyimbo vya Kiadventista katika simu yako ya mkononi. Pakua mojawapo ya programu hizo na uendelee kufurahia.

Unaweza pia kupata nakala ya kitabu cha nyimbo katika Duka la vitabu la Waadventista wa Sabato lililoko karibu nawe au kwenye tovuti yao.

Ili kufurahia uimbaji wa nyimbo za Waadventista wa Sabato, tembelea kanisa katika eneo lako au angalia ibada yake inayotangazwa moja kwa moja mtandaoni.

Kitabu cha nyimbo cha Waadventista Wa Sabato ni nini

Kitabu cha nyimbo ni mkusanyiko wa nyimbo, au zaburi, zinazotumika katika ibada za kidini. Hivyo, Kitabu cha Nyimbo cha Waadventista wa Sabato kina nyimbo zinazotumika katika ibada za Waadventista.

Nyimbo ya kutukuza ni tofauti na nyimbo nyingine kwa kuwa hutumiwa katika muktadha wa ibada na mara nyingi hutoa sifa kwa Mungu. Leo, watu wanahusisha neno hilo na mtindo wa muziki wa jadi, ukisindikizwa na piano au ogani, au wakati mwingine gitaa.

(Tafadhali zingatia: Hii haimaanishi kwamba kuimba nyimbo za kutukuza ni utakatifu zaidi kwa namna fulani. Badala yake, ni uchaguzi tu katika mtindo wa muziki kati ya mitindo mingine inayomtukuza Mungu.)

Huenda ukagundua kwamba makanisa mengi ya Waadventista huchagua kuimba nyimbo za kutukuza kutokana na utajiri uliopo katika ujumbe, kicho, na maneno ya kishairi. Zinaweza:

  • Kutengeneza hali ya sifa na ibada
  • kutusaidia kuelekeza fikira zetu kwa Yesu
  • kutukumbusha imani zetu na kuimarisha imani yetu
  • kutuhamasisha katika utume wetu wa kushiriki wema wa Mungu, na kujiandaa kwa ujio wake

Hebu tujifunze zaidi kuhusu yaliyomo ndani ya kurasa za kitabu hiki.

Muhtasari wa kitabu cha Nyimbo cha Waadventista wa Sabato

Mkusanyiko huu wa nyimbo umepangwa kwa mada na una sehemu kuu mbili. Sehemu ya kwanza na kubwa zaidi ina jumla ya nyimbo —695! Sehemu ya pili ina Maandiko kwa ajili ya ibada.

Sehemu ya nyimbo imepangwa kwa makundi, ambayo yanatajwa kwenye Jedwali la Yaliyomo mwanzoni mwa kitabu cha nyimbo. Yafuatayo ni makundi hayo:

Nyuma ya kitabu cha nyimbo kuna zana muhimu pia. Zinazojumuisha

  • Orodha (Faharasa) ya nyimbo kulingana na mada
  • Orodha ya Maandiko, inayoonyesha aya za Biblia na nyimbo zinazotokana na aya hizo
  • Orodha ya nyimbo kwa ajili ya watoto
  • Orodha ya waandishi na watunzi wa nyimbo
  • Orodha ya ala za nyimbo
  • Orodha ya metriki, ambayo inayo orodhesha nyimbo kulingana na idadi ya silabi katika kila mstari wa muziki
  • Orodha ya jumla, ambayo inayo orodhesha nyimbo kwa majina yake au mistari ya kwanza

Hebu tuangazie kwenye ukurasa wa kitabu cha nyimbo.

Kutazama ukurasa wa kitabu cha nyimbo

Katika muundo wake, kitabu cha nyimbo cha Waadventista hakitofautiani sana na vitabu vya nyimbo vya madhehebu mengine ya Kikristo. Unapofungua ukurasa wa wimbo, utapata namba yake kwenye kona ya juu kulia. Watu hutumia namba hizi kuonyesha ni nyimbo zipi zitaimbwa, kwani ni fupi kuliko majina yake na hivyo msomaji anaweza kuupata wimbo kwa urahisi.

Kisha, utaona noti za muziki pamoja na maneno ya wimbo katikati (isipokuwa kitabu cha nyimbo maneno pekee). Hii inachukua sehemu kubwa ya ukurasa na ndio hutumiwa na waimbaji na wapigaji muziki.

Noti ya muziki sio maalum kwa wapigaji muziki, badala yake, imeandikwa kwa ajili ya kwaya kuimbia, ambapo watu huimba kwa sehemu nne—melodi na sehemu tatu za sauti kwa ajili ya upatanifu.

Lakini usijali—sio lazima ujue jinsi ya kufanya hivyo! Watu wengi huimba tu melodi au wimbo wenyewe, au kufuatisha maneno tu.

Kushoto, juu ya noti ya muziki, utaona jina. Huyo ndiye mwandishi wa wimbo.

Kulia, utaona majina machache—lile lililo juu ni jina la wimbo na lile lililo chini ni jina la mtunzi wa wimbo, kwani mara nyingine mtunzi ni tofauti na mtu aliyeandika maneno.

Nyimbo za Kikristo

Kitabu cha nyimbo cha Waadventista kina nyimbo mbalimbali kutoka kwa waandishi wa nyimbo wa Kanisa la Waadventista wa Sabato na wasio wa Waadventista. Nyimbo nyingi zinazopendwa sana katika kanisa la Waadventista pia zinathaminiwa katika madhehebu mengine. Fikiria “Neema ya Ajabu,” “Roho Yangu na Ikuimbie,” au “Alilipa Bei”.

Hapa kuna baadhi ya waandishi maarufu wa nyimbo na waimbaji ambao nyimbo zao zimo katika kitabu cha nyimbo cha Waadventista, na moja ya nyimbo zao maarufu:

  • Fanny Crosby (“Yesu Mwokozi kwa Hakika”)
  • Ira D. Sankey (“Chini ya Mbawa Zake”)
  • Isaac Watts (“Nasifu Shani ya Mungu”; “Msalaba wa yesu”)
  • Charles Wesley (“Malaika Wanaimba”)
  • Philip Bliss (aliandika muziki wa “Ni Salama Rohoni”)
  • Lowell Mason (“Furaha kwa Ulimwengu”)

Angalia kama unautambua wimbo wowote hapo pembeni.

Ni kitu gani kinacho fanya Nyimbo za Kiadventista ziwe tofauti?

Kitabu cha Nyimbo cha Kiadventista ni cha kipekee kwa sababu nyingi kati ya nyimbo zake zinaeleza ukweli wa Kibiblia ambao umekuwa muhimu katika Kanisa la Waadventista tangu mwanzo wake. Kweli kama vile ujio wa pili wa Yesu, hukumu, patakatifu, utume ulimwenguni, na Sabato.

Nyimbo mbili zinazo zingatia hukumu ni “Funika na Maisha Yake” na “Imeanzishwa Hukumu Mbinguni,” ambazo ziliandikwa na mwandishi na mtunzi wa Mwadventista, F. E. Belden.

Nyimbo Maarufu za Waadventista Maarufu:

Neema ya ajabu
Jinsi Ulivyo Mkuu
Ni Salama Rohoni Mwangu
Wewe Mwamunifu
Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu
Uwe Maono Yangu
Habari Njema
Alilipa Bei
Ngome Kuu
Uje Unisaidie
Yesu kwetu ni Rafiki
Pale Msalabani
Mtazame Mwokozi
Mungu Atukuzwe
Taji Mvikeni
Msifu Mungu Wa Neema

Nyimbo kuhusu Sabato ni pamoja na “Kilele cha Uumbaji” na “Ikumbuke Sabato.

Wimbo mmoja unaolenga urithi wetu wa unabii ni, “Tazama Alama Njiani.” Wimbo huu unafuata unabii wa Danieli 2, ambao unaonyesha sanamu ya madini tofauti tofauti, ikionyesha milki za ulimwengu zilizopita katika historia hadi kuja kwa Kristo. Wimbo huo unataja milki hizo na kutuita kuziangalia hizi “alama njiani” kama dalili za kurudi kwa Yesu hivi karibuni.

Nyimbo zinazokazia mafundisho yetu ziliwahamasisha Waadventista wa kwanza na bado zinatutia moyo leo katika kumfuata Yesu.

Kitabu cha Nyimbo cha Kiadventista kina historia gani?

Uimbaji umekuwa sehemu muhimu ya Uadventista tangu mwanzo wake. Hata kabla ya kanisa kuundwa rasmi, waanzilishi wake walichapisha vitabu vya nyimbo. Kitabu cha nyimbo cha sasa kiliandaliwa na kamati ya Konferensi Kuu kuanzia mwaka 1982 hadi 1984.

Hebu turudie kidogo.

Kitabu cha kwanza cha nyimbo za Kiadventista

James White, mmoja wa waanzilishi wa kanisa, alichapisha kitabu cha kwanza cha nyimbo kwa kanisa hilo mwaka 1849—zaidi ya miaka 10 kabla ya kanisa hata hilo kupata jina lake. Aliita kitabu chake Hymns for God’s Peculiar People That Keep the Commandments of God and the Faith of Jesus. (Ndio, vitabu wakati huo vilikuwa na majina marefu!)

Ni aina gani ya nyimbo zilikuwemo?

Kilikuwa na nyimbo kutoka madhehebu mengine mengi, ikiwa ni pamoja na Methodist na Baptist. Pia kilikuwa na nyimbo za Waadventista zilizoakisi utume wao katika kujiandaa kwa ujio wa Yesu.

Vitabu vinne zaidi vya nyimbo vya kanisa “rasmi” vilifuata kabla ya toleo la hivi karibuni.1

Kitabu cha Nyimbo za Waadventista wa Sabato cha Mwaka wa 1985

A Seventh-day Adventist songbook open on a music stand

Photo by Mick Haupt on Unsplash

Mwaka wa 1981, Mkutano Mkuu ulichagua watu 19 kwa ajili ya kamati ya maandalizi ya Kitabu cha nyimbo. Iliyoongozwa na Charles L. Brooks, kikundi hiki, pamoja na kamati kubwa ya ushauri ya watu 90 kutoka duniani kote, ingeandaa kitabu kipya cha nyimbo za kanisa.

Kamati ilifanya utafiti kwa kuwauliza wachungaji 3,000 kuhusu nyimbo za zamani ambazo wangependa kuziona katika kitabu kipya. Pia walifanya utafiti katika vitabu vya nyimbo 100 tofauti tofauti.

Waliishia kupata orodha ya nyimbo 3,600 ambazo zingehitaji kuchaguliwa!

Kisha kazi ikaanza. Kutoka 1982 hadi 1984, wajumbe walitumia muda mwingi nyumbani na kukutana mara tano kwa siku nne kila mara. Walilazimika kusikiliza kila wimbo, kuupitia, na kupiga kura juu yake.

Vigezo gani vilitumika?

Walijiuliza maswali yafuatayo:2

  • Je! Wimbo uliendana na Biblia na mafundisho yake?
  • Je! Ungefaa kwa kundi kubwa lenye umri na tamaduni mbalimbali ndani ya ulimwengu wa Kiingereza?
  • Je! Ilikuwa kitu ambacho watu wangeweza kujifunza kwa urahisi na kufurahia kuimba au kuucheza katika vyombo?

Wakusanyaji walitaka nyimbo ambazo zilithibitisha mafundisho ya pekee ya Kiadventista na kutuunganisha na Ukristo kwa ujumla. Ili kupata utofauti, walichagua baadhi ya nyimbo za mwanzo za Waadventista, nyimbo za Injili za kisasa, nyimbo za kiroho za Wamarekani Weusi, na nyimbo za kiroho za watu wengine.

Baada ya nyimbo kupigiwa kura na kuchaguliwa, Kitabu cha Nyimbo cha Kanisa la Waadventista Kilichapishwa mwaka 1985. Konferensi Kuu Ilisaidia kuhamasisha kitabu hicho.

Toleo hili tunalolizungumzia ni lile la kawaida linalotumiwa katika makanisa mengi ya Kikristo ya Kiadventista yanayo zungumza Kiingereza. Pia imetafsiriwa katika lugha nyingine. Mbali na kitabu hiki cha nyimbo, baadhi ya makanisa ya Kiadventista hutumia vitabu vingine vya nyimbo pia, ikiwa ni pamoja na vile vilivyotengenezwa kwa ajili ya watoto.

Wapi naweza kupata kitabu cha nyimbo cha Kiadventista leo

Sio ngumu kupata kitabu cha nyimbo cha Kiadventista! Angalia tu kabati ndogo ya vitabu au mfuko nyuma ya kiti cha Kanisa la Waadventista lililoko karibu nawe. Unaweza kupata kimoja hapo, Unaweza kupata pia Biblia na labda vitabu vingine vya nyimbo pia.

Lakini ikiwa sivyo, habari njema ni kwamba kuna programu nyingi za bure za nyimbo za Waadventista kwa simu yako. Pakua programu moja wapo na uendelee kufurahia.

Unaweza pia kupata nakala ya kitabu hicho katika duka la vitabu la Kiadventista lililoko karibu nawe au kwenye tovuti yao.

Ili kufurahia uzoefu wa kuimba nyimbo za Kiadventista, tembelea kanisa katika eneo lako au utazame ibada yake inayorushwa (mubashara) mtandaoni.

Nyimbo za Kiadventista zinaweza kuboresha ibada yetu kwa Mungu.

Katika maeneo mengi, Biblia inatuhimiza “kuimba kwa Bwana” au “kuinua sauti zetu” tukimsifu. Waefeso 5:19 hata inazungumza kuhusu “mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu” (NKJV). Lengo la kitabu cha nyimbo cha Waadventista ni kuwasaidia watu kufanya hivyo. Kinaturuhusu kutumia nguvu ya muziki kuunganisha mioyo yetu katika ibada kwa Mungu.

Kadri tunavyoimba, nyimbo zinainua roho zetu, kutukumbusha kuhusu utume wetu katika ulimwengu huu, na kutusaidia kupata uzoefu wa uwepo wa Yesu.

Ndio, kuimba ni sehemu moja tu ya ibada. Lakini ni sehemu yenye maana sana inayotuvuta kwa Mwokozi wetu kwa njia ambazo ibada nyingine haziwezi kufanya. Kuimba daima imekuwa njia ya kueleza dhana na hisia za kina, na mara nyingi nyimbo huwa na maana kubwa kwa watu wanaozitunga na wanaoimba.

Ungependa kujifunza zaidi kuhusu ibada za Kanisa la Waadventista wa Sabato?

Tafuta Kanisa

If you’re interested in finding a local Adventist church near you, you can use the Adventist Locator provided by the General Conference of Seventh-day Adventists.

  1. Seventh-day Adventist Hymnal (Hagerstown, MD, Review and Herald, 1985), p. 5. []
  2. Seventh-day Adventist Hymnal, p. 6; Hooper, Wayne, “The Making of the Seventh-day Adventist Hymnal.” []

Je, Una swali kuhusu Waadventista? Uliza hapa!

Pata majibu kwa maswali yako kuhusu Waadventista Wasabato

Majibu Zaidi