Kanisa la Waadventista wa Sabato lina mfumo wa uwakilishi unaounganisha makanisa yake zaidi ya 90,000 ulimwenguni na kuwapa washiriki wake nafasi katika kufanya maamuzi. Ingawa Kanisa lilisajiliwa mwaka 1863, mfumo huu ulianzishwa wakati wa kurekebisha upya wa kanisa kati ya 1901 na 1903. Unajumuisha ngazi nne za utawala.
Mfumo huu ni wa kipekee ikilinganishwa na muundo wa utawala katika madhehebu mengine.
Hakuna mtu anaye simama kama kichwa (mfumo wa kieklesi), au hata kundi la viongozi wanaofanya maamuzi kwa niaba ya mwili wote (mfumo wa kipresbiteri). Badala yake, mamlaka hutoka kwa washiriki wa kanisa, ambao wanachagua wajumbe wa kuhudumu katika ngazi ya kanisa ulimwenguni.
Kusudi la aina hii ya muundo ni nini?
Kanisa linalounganishwa na utume kwa ulimwengu linahitaji njia yenye ufanisi katika kuutekeleza. Muundo huu unahakikisha kuwa kila kanisa lina rasilimali kwa ajili ya kuwahudumia washiriki wake na kuongoza watu kwa Yesu.
Hivyo hebu tupate maelezo zaidi kwa kuangalia:
Ni ngazi zipi nne za utawala katika Muundo wa Kanisa la Waadventista wa Sabato?
Ngazi za utawala katika Kanisa la Waadventista wa Sabato ni kama mduara wa mzunguko. Kuanzia mduara mdogo zaidi katikati, ni:
1. Kanisa mahalia
2. Konferensi mahalia
3. Union Konferensi
4. Konferensi Kuu na divisheni zake
Ngazi hizi zinatengeneza mtandao wa kanisa duniani kote. Kila moja ipo ili kuhudumia ngazi iliyoko chini yake vizuri zaidi, hivyo kuwezesha uongozi mahalia kuhudumia washiriki wake binafsi vizuri zaidi. Kwa upande wao, washiriki wanaweza kujikita kwenye misheni yao—kushiriki habari za Yesu.
Uongozi wa kanisa mahalia
Kanisa la mahalia ni kikundi cha waamini wanaompenda Yesu na kuishi kulingana na mafundisho ya Neno lake. Wanapokea mwongozo wa kiroho kutoka kwa mchungaji na hukutana mara kwa mara kwa ibada. Pia wanapata fursa ya kushiriki katika mchakato wa maamuzi ya kanisa kupitia mikutano ya halmashauri, kama inavyohitajika.
Washiriki wote wa kanisa wanaweza kuhudhuria na kupiga kura katika mikutano ya halmashauri ya kanisa. Aina za maamuzi yanayofanywa wakati wa mikutano hiyo ni pamoja na:
- Ushiriki wa Kanisa
- Maamuzi ya Kifedha
- Nidhamu
- Uchaguzi wa Viongozi
- Shughuli za Uinjilisti
Wakati mwingine, baadhi ya mikutano hii hufanyika siku ya Sabato wakati wa ibada. Kwa mfano, baada ya ubatizo, mchungaji ataita kura ili kukubali mtu aliye batizwa kuwa mshiriki—ni njia rasmi tu ya kusherehekea kukubaliwa kwa mshiriki mpya katika kanisa, kuonyesha umoja.
Lakini maswala ya kifedha na halmashauri, au mambo yanayo hitaji mjadala mkubwa, hushughulikiwa wakati mwingine.
Katika mikutano ya halmashauri ya kanisa, washiriki wana fursa ya kuwapigia kura viongozi wao. Viongozi hawa huunda baraza la kanisa, ambalo linashughulikia maswala ya kiutawala kanisani. Ni kama baraza la wakurugenzi kwa kampuni.
Katika Makanisa ya Waadventista wa Sabato, kanisa halimwajiri moja kwa moja mchungaji wake. Badala yake, konferensi ya eneo mahalia hutoa majina kwa kanisa kuchagua kutoka kwao na kushughulikia mchakato wa ajira.
Ingawa mchungaji hutoa msaada wa kiroho na uongozi, mamlaka yake—na mamlaka ya baraza la kanisa—hayazidi mamlaka ya mkutano wa halmashauri. Mwishowe, kura za washiriki wa kanisa ndizo zenye mamlaka kuu.
Konferensi mahalia
Konferensi mahalia inajumuisha kundi la makanisa ndani ya eneo fulani, kama vile mkoa au eneo la mji mkuu. Viongozi wake huchaguliwa na ujumbe wa waumini wa kanisa wakati wa mkutano wa uwakilishi.
Mkutano wa uwakilishi nini? Tunaweza kulinganisha na mkutano wa halmashauri ya kanisa mahalia. Maamuzi muhimu kwa ajili ya konferensi hufanywa katika mkutano huu.
Makanisa mahalia huchagua wawakilishi, ambao wamepigiwa kura na washiriki (au wapiga kura), kuhudhuria mkutano wa uwakilishi. Kwa njia hii, kila kanisa linashiriki katika maamuzi ya konferensi.
Konferensi mahalia ina majukumu yafuatayo:
- Kuajiri wachungaji
- Kugawa pesa ya zaka kwa ajili ya kulipa wachungaji
- Kuidhinisha makanisa ya mtaa
- Umiliki wa mali ya kanisa
- Usimamizi wa shule za bweni za Waadventista
- Mipango ya Konferensi kwa ajili ya kufikia jamii nzima
Unioni Konferensi
Union Konferensi ni muunganiko wa konferensi mahalia kadhaa ndani ya eneo. Kawaida inashughulikia majimbo machache, mikoa, au maeneo.
Kwa mfano, Union Konferensi ya Kaskazini mwa Pasifiki nchini Marekani yenye konferensi sita: Alaska, Idaho, Montana, Oregon, Washington, na Upper Columbia (eneo la kaskazini-mashariki mwa jimbo la Washington).
Kama ilivyo kwa Konferensi mahalia, Union Konferensi hufanya mikutano ya wajumbe. Lakini safari hii, konferensi mahalia huchagua wajumbe kutoka kwa washiriki wa kanisa.
Ni nini jukumu la union konferensi?
Inashughulikia maswala ya utawala kwenye eneo lake. Pia inawawekea mikono (inaidhinisha) wachungaji na inaendesha taasisi za union, kama vile vyuo vikuu.
Na usisahau uinjilisti! Kila ngazi ya muundo wa kanisa imetengenezwa kutoa msaada katika kutimiza utume katika kusambaza habari njema kuhusu Yesu.
Konferensi Kuu na divisheni zake
Konferensi Kuu ya Waadventista wa Sabato, yenye makao makuu yake huko Silver Spring, Maryland, ina mamlaka juu ya makanisa yote ya Waadventista kote ulimwenguni—inayojulikana kama kanisa la ulimwengu. Ina divisheni 13 zenye ofisi kila kanda. Viongozi wa divisheni hizi husaidia kazi ya Konferensi Kuu katika kupanga na kutoa rasilimali kwa maeneo yao na kanda husika.

Zifuatazo ni Divisheni hizo:
- Divisheni ya Afrika ya Mashariki-Kati (ECD)
- Divisheni ya Ulaya-Mashariki ya Asia (ESD)
- Divisheni ya Amerika ya Kati (IAD)
- Divisheni ya Ulaya ya Kati (EUD)
- Divisheni ya Amerika Kaskazini (NAD)
- Divisheni ya Kaskazini-Mashariki ya Asia-Pasifiki (NSD)
- Divisheni ya Amerika Kusini (SAD)
- Divisheni ya Pasifiki Kusini (SPD)
- Divisheni ya Kusini mwa Afrika-Bahari ya Hindi (SID)
- Divisheni ya Kusini mwa Asia (SUD)
- Divisheni ya Kusini-Mashariki ya Asia-Pasifiki (SSD)
- Divisheni ya Ulaya ya Kati (TED)
- Divisheni ya Afrika ya Magharibi-Kati (WAD)
Labda unajiuliza ni nini jukumu la Konferensi Kuu.
Konferensi Kuu inashughulikia uanachama wa union Konferensi, sera za ulimwengu, na maswali yanayohusiana na imani za msingi. Wajumbe hupiga kura kuhusu maswala haya wakati wa mkutano mkuu wa Konferensi Kuu kila baada ya miaka mitano.
Mamlaka ya juu kabisa ya kufanya maamuzi katika Kanisa la Waadventista wa Sabato iko chini ya mikutano hii.
Basi, maamuzi haya hufanywa vipi hasa?
Jinsi maamuzi yanavyofanywa kwa ajili ya kanisa la ulimwengu?

Photo by Element5 Digital on Unsplash
Wajumbe kutoka sehemu mbalimbali duniani husaidia kufanya maamuzi makubwa kwa ajili ya kanisa la ulimwengu kulingana na Biblia. Wanakutana kila baada ya miaka mitano wakati wa mkutano mkuu wa Konferensi Kuu ambao hufanyika Marekani Kaskazini. Hii inamaanisha kwamba kila mshiriki wa kanisa anawakilishwa katika maamuzi.
Takriban wajumbe 2,500 hushiriki mikutano hii na kupiga kura, wakisafiri kutoka sehemu mbalimbali za dunia.
Kati ya wajumbe hawa, angalau nusu ni waumini wa kawaida wa kanisa, wachungaji, na walimu. Kila Union konferensi hupata kuchagua idadi fulani ya waumini kama wajumbe.
Kwa maneno mengine, karibu kila Mwadventista anaweza kuwa mjumbe!
Nusu nyingine ni viongozi wa kanisa wanaowakilisha taasisi na kamati za ulimwengu.
Wakati wa kikao, wajumbe hujadili ajenda iliyotayarishwa na kamati ya utendaji ya Konferensi Kuu na kupiga kura juu ya mambo hayo. Pia wanachagua viongozi wa Konferensi Kuu, rais wa Konferensi Kuu na maafisa wa kanisa la ulimwengu.
Lakini hapa ndipo sehemu muhimu zaidi:
Kila hatua ya mchakato wa kufanya maamuzi inahusisha maombi mengi na kusoma Biblia.
Viongozi wa kanisa na wajumbe wanatafuta mwongozo wa Roho Mtakatifu kwa sababu wanatambua kwamba Yesu ndiye kiongozi wao wa juu zaidi. Wanatamani kila uamuzi uthibitisho Biblia na kuendeleza utume wa kanisa.
Muundo wa kifedha wa Kanisa la Waadventista wa Sabato ukoje?

Photo by Steve Johnson on Unsplash
Kanisa la Waadventista wa Sabato linaendeshwa kama shirika rasmi lisilo la faida. Wafanyakazi wake wote na programu zinaungwa mkono na zaka na michango/ufadhili. Kanisa linakita muundo wake wa kifedha kwenye kanisa la Agano Jipya, ambalo lilikusanya pesa mahali pamoja na kuzigawa kwa makundi mahalia:
“Na wote walioamini walikuwa mahali pamoja, na kuwa na vitu vyote shirika, wakiuza mali zao…. na kuwagawia watu wote kama kila mtu alivyokuwa na haja” (Matendo 2:44-45, NKJV).
Kwa ufupi, kanisa la Agano Jipya lilitegemezwa kifedha na washiriki wake.
Kulingana na mfano wa Kibiblia, washiriki wa kanisa la Waadventista wa Sabato hurudisha zaka—neno katika Biblia linalomaanisha “fungu la kumi.” Kwa kuwa Mungu anamiliki kila kitu, sisi ni mawakili wa pesa zake na kwa furaha tunamrudishia asilimia kumi ya mapato yetu ambayo Yeye anataka (Kumbukumbu la Torati 14:22; Malaki 3:10–12).
Lakini zaka haitumiki kwa chochote. Ina kusudi maalum.
Zaka inawasaidia wale wanaohudumu kama wachungaji na wamisionari, kama ilivyo wasaidia makuhani katika Agano la Kale na viongozi wa kanisa katika Agano Jipya (Hesabu 18:21; 1 Wakorintho 9:13–14).
Uongozi wa kanisa hukusanya zaka na kuituma kwa konferensi mahalia. Kutoka hapo, inasambazwa kuwalipa wachungaji. Mpango huu unazuia changamoto ya makanisa yenye washiriki wengi kuweza kutoa mishahara mikubwa kuliko wale wenye washiriki wachache.
Ili kujifunza zaidi kuhusu imani za Waadventista kuhusiana na zaka, angalia ukurasa huu kuhusu uwakili.
Kisha, kuna sadaka.
Sadaka ni zawadi ya hiari ya pesa iliyotolewa kwa Mungu (Kutoka 35:29; 2 Wakorintho 8:2–4). Wakati mwingine, mtoaji hutoa sadaka kwa ajili ya mradi au hitaji fulani.
Lakini sadaka ambazo hazina maelezo hugawanywa kulingana na Mpango wa Pamoja wa utoaji. Hivi ndivyo inavyofanya kazi:
Takriban asilimia 50 ya matoleo yanasalia katika kanisa mahalia, asilimia 20 hadi 30 yanasaidia utume wa eneo husika, na asilimia 20 huenda kwenye Konferensi Kuu, ambayo huisambaza kwenye miradi ya utume duniani kote.
Kwa njia hii, kanisa la ulimwengu husaidia kila kusanyiko mahalia—bila kujali ukubwa au eneo—kukamilisha utume wake.
Muundo wa Kanisa la Waadventista unahusu utume wake.
Muundo wa dhehebu la Waadventista ni wa kipekee kwa namna ambayo hutimiza mahitaji ya mtandao wake wa kimataifa na humpa kila mshiriki sehemu katika maamuzi muhimu. Bila shaka, Roho Mtakatifu alituongoza kwenye mpango huu.
Muundo huu husaidia kanisa kufanya kazi na kutimiza kusudi lake: kuwawezesha washiriki wa kanisa kuishi utume wao kama watu wa Mungu.
Lakini licha ya kuwa na ngazi zote hizi za utawala, lazima tukumbuke jambo moja kuu:
Yesu ndiye kiongozi mkuu wa kanisa.
Muundo upo ili kutusaidia kutekeleza mipango yake kwa namna bora kadri inavyowezekana.
Ili kupata maelezo zaidi,
Tafuta Kanisa
If you’re interested in finding a local Adventist church near you, you can use the Adventist Locator provided by the General Conference of Seventh-day Adventists.
Kurasa Zinazohusiana:
Majibu Zaidi
Wasimamizi wa Waumini Wana Nafasi Gani Ikilinganshwa na Wachungaji?
Neno “Usimamizi wa kidini” linatokana na neno la Kigiriki laikos, ambalo maana yake ni “wa watu.”
Kitabu cha Nyimbo cha Waadventista Wa Sabato
Kitabu cha nyimbo cha Waadventista wa Sabato ni kitabu cha nyimbo kinachotumiwa ulimwenguni kote na makanisa mengi ya Waadventista wakati wa ibada zao.






