Ni Lini Yesu Atarudi Tena?
Hatujui saa halisi ya kurudi kwa Yesu Kristo.
Biblia inasema kwamba hakuna mtu anayeweza kujua, hata malaika (Mathayo 24:36)! Ndio maana Biblia inatushauri tusijaribu kuweka tarehe ya kurudi kwake. Kwa sasa, tunahimizwa kuwa tayari.
Hata hivyo, Biblia inatuambia mambo fulani ambayo yatatokea kabla ya ujio wake mara ya pili. Ishara hizi za Kibiblia hazionyeshi mfuatano wa matukio kulingana na wakati, lakini zinazonyesha mwelekeo wa dunia yetu.
Ni jambo la kawaida kujiuliza kinachotokea katika nyakati za mwisho na kile ambacho dalili hizi zinaashiria. Hebu tuangalie kwa karibu kile Biblia inachosema.
Hapa ndipo tutakapozungumzia:
- Kwa nini hatuwezi kujua wakati halisi wa kuja kwa Yesu?
- Tunajua nini kuhusu kurudi kwa Yesu?
- Nini maana ya yote haya
Hebu tuanze na sababu ya kuwa hatuwezi kujua.
Kwa nini hatuwezi kujua wakati kamili wa ujio wa Yesu?

Photo by Towfiqu barbhuiya on Unsplash
Yesu hatuambii ni lini Atarudi kwa sababu hio sio jambo kuu. Muda ni kitu ambacho hatuwezi kuelewa.
Mtazamo wa Mungu ni mkubwa sana kuliko wetu. Anaona taswira kubwa ya mahali ambapo dunia inaelekea, na anaweza kujua wakati Yesu anahitaji kurudi.
Hili inaonyeshwa katika 2 Petro 3:8. Kwa Mungu, “siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja” (NKJV).
Hatuna uwezo wa kuona taswira yote—hatujui hata kitakachotokea katika saa moja linalokuja! Ndiyo maana haina maana kwetu kujua lini Yesu atakuja.
Na ndiyo maana Yesu anawaambia wanafunzi wake juu ya Mlima wa Mizeituni, katika mazungumzo kuhusu kurudi kwake,
“Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake” (Mathayo 24:36, NKJV; angalia pia Mathayo 24:42, 44; Marko 13:32).
Yesu anataka tuweke mkazo katika ukweli kwamba Anarudi (Yohana 14:2-3)! Hili ni tumaini ambalo binadamu amekuwa nalo tangu Yesu alipopaa mbinguni karne ya kwanza, na ni jambo la kulitazamia kwa mioyo yetu yote.
Kusumbukia sana siku ya kuja kwake kunaweza kututoa kwenye lengo halisi: kujazwa na upendo wa Kristo na kuushirikisha kwa wengine, jambo ambalo hutuandaa kwa ujio wake wa mara ya pili. Ujio wa Yesu uko karibu (Ufunuo 22:12) – unaweza kuwa muda wowote kutoka sasa. Kwa wakati huu, tunahitaji kumwamini, kumpokea, na kushikamana naye, hata wakati ulimwengu unapoporomoka katika machafuko ya siku za mwisho.
Kwa sababu hilo litatokea. Maandiko yanatuambia kwamba dhambi ilifanya Dunia iwe na machafuko kama ilivyo (Isaya 59:2, Warumi 5:12). Na kama dhambi haitazuiliwa, Dunia itajiangamiza wakati fulani.
Kuja kwa Yesu kutakomesha dhambi (Ufunuo 21:4; 1 Wakorintho 15:24), ndio maana Wakristo wanatazamia sana ujio wake.
Yesu anatupa dalili katika Biblia tunazoweza kuzitazamia, ili kutuhakikishia kuwa ni sehemu ya mwelekeo wa dunia. Ikiwa tunatambua dalili hizo, hatutalazimika kuwa na hofu au wasiwasi zinapotokea. Badala yake, tunaweza kumshikilia Yeye, tukijua kuwa kurudi kwake kunakaribia.1
Kutabiri wakati au tarehe kunaweza kusababisha kusahau jambo hili, na hatutakuwa sahihi kamwe kwa sababu hakuna njia ya kujua. Watu wamejiwekea tarehe katika historia, lakini wameishia kukatishwa tamaa.
Kwa mfano, Wafuasi wa Miller walidhani ujio wa Kristo ungekuwa Oktoba 22, 1844.2
Na Howard Camping alitabiri ufalme wa Mungu ungekuja katika tarehe tofauti tofauti katika miaka ya 1990 na, kwa kiasi kikubwa, Mei 21, 2011.3
Wengine walidhani mwisho wa kalenda ya Mayan mnamo Desemba 21, 2012 ilimaanisha mwisho wa dunia.4
Tarehe hizi (na kupita kwake) zimewakengeusha watu kutoka kwenye ujumbe halisi: Yesu anakuja, na tunapaswa kuwa tayari!
Ni wazi kuna mengi tusiyoyajua kuhusu ujio wa Yesu, hivyo hebu tuangalie baadhi ya mambo tunayoyajua.
Nini tunachojua kuhusu kurudi kwa Yesu?

Photo by Doruk Aksel Anıl
Agano jipya linatupa ufahamu mwingi kuhusu mambo yatakayotokea ulimwenguni kabla ya ujio wa pili wa Kristo.
Katika Injili, hasa Mathayo 24, Marko 13, na Luka 21, Yesu anawaambia wanafunzi wake matukio yatakayotokea wakati ulimwengu unapoelekea mwisho wake. Matukio hayo hayatuambii moja kwa moja jinsi ujio wa Yesu ulivyokaribia; badala yake, yanaonyesha ulimwengu wetu unaokufa ulipofikia.
Dhambi ina tabia ya kuharibu (Warumi 6:23), na mchakato wa kuharibu unaoruhusiwa kuendelea kwa muda usiojulikana kiasili huishia katika uangamivu.
Yesu alipowaambia wanafunzi kuhusu matukio haya, aliwakumbusha,
“Hayo hayana budi kutukia, lakini ule mwisho bado. … Haya yote ni mwanzo wa uchungu” (Mathayo 24:6, 8, NKJV, msisitizo umeongezwa).
Matukio haya humaanisha kuwa tunakaribia wakati, sio kwamba Yesu anakuja kesho. Mambo yatazidi kuwa mabaya tunapoendelea kwenye njia ya uharibifu.
Biblia inalinganisha maendeleo ya matukio na uchungu wa kuzaa. Mathayo 24:8 katika NKJV inasema, “Hayo yote ni mwanzo wa utungu.”
Na Paulo anarejelea hili katika moja ya barua zake: “Wakati wasemapo, Kuna amani na usalama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafla, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa” (1 Wathesalonike 5:3, NKJV).
Kama vile utungu unavyozidi kuongezeka kadiri muda wa kujifungua mtoto anavyo karibia, vivyo hivyo dalili hizi zitaongezeka kwa idadi ya kujirudia kwake na nguvu kadiri tunavyokaribia kurudi kwa Yesu.
Na jambo lingine la kukumbuka ni kwamba kunapokuwa na utungu, unajua jambo fulani litatokea hivi karibuni, lakini bado hujui ni lini mpaka litakapoanza kutokea. Tunajua Yesu atarudi, lakini hatujui ni lini hasa – dalili hizi tu zinatuambia ujio wake utakuwa hivi karibuni.
Kwa kuzingatia hili, hapa kuna baadhi ya matukio ambayo Yesu aliyataja alipokuja mara ya kwanza, kuwa tumekaribia ujio wake wa mara ya pili:
- Watu watajidai kuwa Yesu na manabii wa uongo (Mathayo 24:5, 11, 24; Marko 13:6, 22; Luka 21:8)
- Vita na uvumi wa vita (Mathayo 24:6; Marko 13:7; Luka 21:9)
- Majanga kama njaa, milipuko ya magonjwa, na matetemeko ya ardhi (Mathayo 24:7; Marko 13:8; Luka 21:11)
- Ghasia za kijamii (Mathayo 24:9-10; Marko 13:8-9, 11-13; Luka 21:12, 16)
- Majanga ya asili (Mathayo 24:29-30; Marko 13:24-25; Luka 21:25)
Mtume Petro pia anazungumza kuhusu watu ambao hawataamini kwamba Yesu anakuja, wakisahau kuhusu Uumbaji na Nuhu na Gharika (2 Petro 3:3-6).
Na mtume Paulo anamwonya Timotheo (2 Timotheo 3:1-5) kwamba watu watakuwa
- Wachoyo
- Walafi na wapenda starehe
- Wenye kujivuna
- Wenye kiburi na majivuno
- Wenye kukufuru na wenye mfano wa utaua
- Wasiotii na wasio na sheria
- Wasio na shukrani
- Wasio safi
- Wasiopenda
- Wasiosamehe
- Wasiojidhibiti
- Waovu
“Maelezo ya Petro na Paulo yanaonyeesha tabia za watu ambao wamekuwepo na zaidi siku hizi. Dunia haiongezeki bora—itaendelea tu kuzidi kuwa mbaya.
Kitabu cha Ufunuo kinaandika maono yaliyotolewa kwa mtume Yohana kuhusu matukio kuelekea mwisho ya Dunia. Kinaelezea mnyama na alama ya mnyama (Ufunuo 13), ambayo inawakilisha uamuzi wa ndani watu watachagua kufuata nguvu ya kidini-kisiasa badala ya Mungu.
Unabii wa Biblia pia unazungumza kuhusu mpinga-Kristo (1 Yohana 2:18, 22, 4:3). Hii ni nguvu ya kidini inayojaribu kuchukua mahali pa Yesu, ikidai kuwa kama Yeye (2 Wathesalonike 2:3-4).5
Baadhi ya watu pia wanaamini kwamba unyakuo wa siri utatokea kabla ya ujio wa pili wa Kristo, lakini hatuoni chochote katika Biblia kinachozungumzia hili.
Kuna dalili nyingi ambazo Biblia inazungumzia. Tunawezaje kutumia kila kitu tulichojifunza kwa ajili ya wakati tulionao hivi sasa?
Nini maana ya yote haya
Ujumbe muhimu kutoka kwenye mjadala huu ni kwamba Yesu anakuja—hivi karibuni! Na dalili alizotupa ni ukumbusho kwamba tunaelekea kwenye mwelekeo sahihi.
Tunaweza kuona ishara ziko kila mahali. Hatuhitaji kuendelea kutazama habari na kuogopa kukosa moja. Jambo kuu ni kuwa makini nazo, ili tunapoziona, tusiwe na hofu au wasiwasi.
Kuja kwa Bwana ni habari njema tunayoweza kutarajia wakati ulimwengu unapozidi kuingia kwenye machafuko.
Hatuna haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu siku halisi ya kuja kwa Yesu.
Tunahitaji kuwa na wasiwasi kuhusu utayari wetu.
“Basi tusilale usingizi kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi” (1 Wathesalonike 5:6, NKJV).
“Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari, kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja” (Mathayo 24:44, NKJV).
Hii haimaanishi kwamba tunapaswa kuhifadhi chakula au kuwa na msimamo mkali. Inamaanisha tunahitaji kutafakari mahali mioyo yetu ipo.6 Je! Imani yetu iko kwa Yesu? Je! Uaminifu wetu uko kwake badala ya ulimwengu? Je tutamtegemea atutunze wakati ulimwengu unapoporomoka? Je! Tunavutwa na upendo wake usio na masharti? Je! Tunaushirikisha waziwazi wengine?
Hiki ndicho Yesu anachotaka tukizingatie: kuweka imani yetu kwake, ili tuweze kumtegemea wakati mambo yatakuwa magumu sana duniani. Ikiwa tumemkubali Yeye, basi wakati halisi hauna umuhimu.
Kama vile mfano wa wanawali kumi katika Mathayo 25, tunapaswa kuwa waangalifu na kuzingatia. Au, kwa maneno ya Mark Finley, mchungaji na mhubiri: “Njia pekee ya kuwa tayari ni kujiandaa, na kubaki tayari.” 7
Weka imani yako na uaminifu kwa Yesu sasa.
Kwa wakati huu, tunaweza kuendelea na maisha kama kawaida (Luka 19:13), bila kuzingatia kila dalili tunazoweza kuona, tukiamini kuwa Roho Mtakatifu atatuongoza. Tunaweza kufanya kazi ya kujenga uhusiano wetu na Yesu ili tuwe tayari atakaporudi kwa utukufu mkuu. Na tunaweza kuishi uhusiano wetu naye na kuonyesha upendo wake kwa wengine, ili nao wawe tayari pia.
Nini kitatokea baada ya Ujio wa Pili wa Yesu?
- Mukuka, Christopher Kabwe, MA. “Discerning signs of the times in the context of Matthew 16:2-3,” Ministry Magazine, February 2024. [↵]
- “United for Mission: One Hundred and Fifty Years,” General Conference of Seventh-day Adventists. [↵]
- “Harold Camping, radio host who predicted world’s end, dead at 92,” CBS News, December 17, 2013. [↵]
- Vance, Erik. “Neither the Maya Calendar—nor the World—Ends on December 21, 2012,” Scientific American, July 6, 2012. [↵]
- “An Introduction to End-Time Prophecies in the Bible,” General Conference of Seventh-day Adventists. [↵]
- Nichol, F. D. The Seventh-day Adventist Bible Commentary, notes to 1 Thessalonians 5:6. [↵]
- Finley, Mark. “End Time Events Before the Second Coming of Christ,” HopeLives365. [↵]
More Answers
Je, Tunaweza Kumpata Yesu Kristo Katika Agano la Kale?
Je, Tunaweza Kumpata Yesu Kristo Katika Agano la Kale?Ndio, unaweza kushangaa kujua kwamba kuna mamia ya aya katika Agano la Kale kuhusu Yesu. Ingawa hazimtaji Yesu kwa jina, zinataja majina mengine tunayoyahusisha naye kama Masihi, Mwana wa Mungu, na Mwana wa Adamu....
Baada ya Yesu kupaa: Alichofanya katika Agano Jipya
Tunapata kumjua Yesu, Mwana wa Mungu na Masihi wetu, kwanza kwa kusoma habari za Injili kuhusu huduma yake duniani.


