Kanuni za Kibiblia kwa Mahusiano Yenye Afya

Mahusiano ya maisha yetu yanaweza kutofautiana kutoka furaha hadi matatizo, rahisi hadi ngumu, furaha hadi kuchosha…

Wakati mwingine inaweza kuwa changamoto kusimamia kila moja ya mahusiano haya yanapoonekana kuwa tofauti sana. Lakini habari njema ni kwamba, Mungu wa mahusiano ambaye alituumba ametupatia kanuni za msingi za kutuongoza katika aina yoyote ya uhusiano.

Tunaweza kupata kanuni hizi za mahusiano yenye afya katika Biblia.

Mungu anataka tuwe na amani na kuishi kwa upatanifu na wale wanaotuzunguka. Ingawa dhambi ilivunja uhusiano kamili wa mwanadamu na Mungu, mpango wake unaendelea kurejesha uhusiano huo. Alienda mbali hata kufanyika mwanadamu kupitia Yesu ili aweze kutembea kati yetu na kutuonesha jinsi ya kupendana.

Kwa kujifunza mfano huo, tunaweza kuutumia katika maisha yetu wenyewe. Tutachunguza maswali yafuatayo:

Tuingie katika Neno la Mungu na tuone tunachokipata.

Mahusiano yanazungumziwaje katika Biblia?

Mwanzoni, Mungu alituumba kwa mfano wake kama viumbe wa kimahusiano. Tangu wakati huo, hadithi nzima ya Biblia inahusu jinsi Anavyotafuta uhusiano na sisi hata baada ya dhambi kututenganisha naye. Anatamani kuziba pengo hilo.

Yesu Kristo ni kielelezo cha shauku hiyo ya Mungu. Alikuja duniani hapa kurejesha uhusiano wa mwanadamu na Mungu na kutuonyesha jinsi mahusiano yetu na Yeye na kati yetu yanavyopaswa kuwa.

Basi tuanze kwa kuelewa tabia ya Mungu ya kimahusiano.

Mungu ni wa kimahusiano

A pair of glasses and the Scrabble letters l-o-v-e sit on an open Bible.

Photo by Emmanuel Phaeton on Unsplash

Kila kitu kuhusu Mungu ni mahusiano, hata hadi kwa asili yake.

Yeye yupo ndani ya “umoja wa familia” ya Utatu Unaoitwa Mungu (Mathayo 28:19). Kila mshirika wa uungu huwahudumia wengine (Yohana 5:30; 16:13–14).

Zaidi ya hayo, Biblia inatuambia kwamba Yeye ni upendo (1 Yohana 4:8).

Tazama haijasema kwamba Yeye anatupenda, au kwamba Yeye tu ana upendo.

Hapana—Yeye ni upendo katika kiini chake kabisa.

Lakini upendo huu ni nini? Dunia yetu inaonyesha upendo kama hisia yenye nguvu lakini yenye migogoro na kasoro. Tunapendana na kutopendana. Tunatumia neno hilo kwa urahisi, kama tunavyopenda unga wa chokoleti, barafu, na gari la hivi karibuni.

Lakini Mungu ni aina ya upendo ulioelezwa katika 1 Wakorintho 13:4–7:

“Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote” (SUV).

Mungu alimwumba mwanadamu kwa sababu anatamani kuwa na uhusiano nasi (Yeremia 31:3). Na ametuumba tukiwa na shauku hiyo hiyo kwake.

Pia alitupa Amri Kumi—ambazo ni mwongozo wa mahusiano yenye afya kati yetu na Yeye na wengine (Mathayo 22:37–40).

Ingawa inavunja moyo wa Mungu kwamba wanadamu walichagua kuasi upendo wake, hajakata tamaa.

Badala yake, ametuonyesha mfano mkubwa zaidi wa maana ya kuwapenda watu wenye changamoto—sisi.

Simulizi ya Biblia imejaa mahusiano

Kisa cha Biblia kinaeleza mwingiliano wa watu na Mungu na wao kwa wao. Kinaonyesha mahusiano ya aina zote, hivyo ni lazima tupate uhusiano ambao tunaweza kuhusiana nao.

Na Biblia haitupatii tu upande mzuri wa mambo. Inaonyesha mema, mabaya, na machafu. Mahusiano ya kibinadamu yanaweza kuwa mabovu sana!

Dhamira tunayoiona ni matumizi ya Mungu ya mifano ya uhusiano anapowafikia watu wake walioasi.

Anatumia maneno agano na ndoa kuelezea ahadi yake kwa mwanadamu. Agano linatokea mara 316 katika Biblia na mara nyingi sana katika muktadha wa uaminifu wa Mungu.1

Pia anatumia ndoa kama ishara ya uhusiano wake na watu wake:

“Kwa sababu Muumba wako ni mume wako” (Isaya 54:5, SUV).2

Kitabu cha Hosea kinaeleza kisa cha Mungu alivyomwagiza Hosea kuoa kahaba na kuendelea kumtafuta kwa upendo hata atakapomwacha mara kwa mara. Vivyo hivyo, Mungu anawatafuta watu wake Akitaka kuwarejesha hata wanapomgeuka.

Aidha, Mungu hutumia lugha ya uzazi kuonyesha upendo wake kwetu:3

“Je! Mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye, hata asimhurumie mwana wa tumbo lake? Naam, hawa waweza kusahau, lakini mimi sitakusahau wewe” (Isaya 49:15, SUV).

Yesu ni kielelezo chetu katika mahusiano

A man bending down, talking to a homeless person on the ground, and holding his cat, just like Jesus would

Photo by Zac Durant on Unsplash

Yesu alikuja ulimwenguni kufunua upendo wa Mungu kwa watu wagumu. Wakati huo huo, alitupa mfano wa jinsi ya kuhusiana na wenzetu (1 Petro 2:21), akiunganisha huruma na kweli.

Ilikuwa kama…

  • Kuwalea wanaume kumi na wawili (Marko 3:14).
  • Kumfikia mwanamke Msamaria aliye hitaji tumaini (Yohana 4) hata ingawa Wasamaria walikuwa maadui wa Wayahudi na kuzungumza na mwanamke ilikuwa marufuku.
  • Kukubali mialiko ya chakula kutoka kwa watu wa jamii waliotengwa (Mathayo 9:10) na viongozi (Luka 7:36).
  • Kuwaalika watoto waje kwake (Marko 10:13–14).
  • Kuzungumza na kiongozi wa kidini Nikodemo na kumwonyesha mahitaji ya moyo wake (Yohana 3).
  • Kuwaombea msamaha wale waliomuua msalabani (Luka 23:34).

Katika kila njia, Yesu alionyesha sifa muhimu kwa ajili ya mahusiano yenye afya.

Upi ni mfano wa Kibiblia kwa mahusiano?

Haijalishi aina ya mahusiano unayotaka kuyaboresha— iwe na rafiki, mzazi, ndugu, mshiriki wa kanisa, mke/mume, au mfanyakazi— Biblia inatoa kanuni zinazofanya kazi katika mahusiano yote. Mara nyingi ni mambo yanayo fanikisha au kuvunja ukaribu.

Hizi ni:

Soma kwa ukaribu kila moja ya mambo haya.

Ubinafsi dhidi ya kujitoa kwa wengine

A young man helping an elderly man get out of the car and use his walker

Photo by RDNE Stock project

Ubinafsi – kujali mahitaji yako kuliko ya mtu mwingine – ndio anguko la mahusiano mengi. Kwa bahati mbaya, sisi sote tuna mwelekeo wa ubinafsi kutokana na asili yetu ya dhambi.

Lakini Yesu alikuja kutuonyesha namna tofauti—ile ya kujitoa. Aliwahudumia wengine, hata kufikia hatua ya kutoa maisha yake. Na kutoka hapo tunashuhudia onyesho kuu la upendo usio na masharti:

“Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake” (Yohana 15:13, SUV).

Tunashuhudia vipande vya ahadi hii katika kisa cha Ruth. Baada ya kupoteza mumewe, alipata nafasi ya kurudi kwa familia yake ambapo angehudumiwa. Badala yake, aliamua kwenda na mkwe wake mjane kwenda nchi ya kigeni na kumhudumia (Ruthu 1:14–17).

Katika Waefeso 5:25, mtume Paulo analinganisha uhusiano wa Yesu na watu wake na kujitoa kafara ambayo mume anapaswa kuwa nayo katika ndoa:

“Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake” (SUV).

Kujitoa kwa hiari kwa pande zote husababisha mahusiano kukua.

Kiburi dhidi ya unyenyekevu

Tunajua jinsi ilivyo kukunja mikono yetu wakati wa mabishano, bila kutaka kukiri kwamba tunakosea. Tunaweza hata kuwa na orodha ya sababu za kwanini tunapaswa “kushinda” mabishano.

Lakini ili kuwa na mahusiano yenye afya tunahitaji kuachilia kiburi hicho. Waefeso 5:21 inatuita “hali mnanyenyekeana katika kicho cha Kristo.” (SUV).

Yonathani alikuwa mrithi wa kiti cha enzi cha Israeli. Na hata hivyo, aliweka kando kiburi cha cheo ili kuwa rafiki na kumlinda Daudi, yule ambaye Mungu alikuwa amemchagua kuhudumu kama mfalme wa Israeli baadaye (1 Samweli 18; 20; 2 Samweli 9:1–7).

Unyenyekevu wetu unaweza kuonekana pia katika jinsi tunavyowatendea watu wanaopambana—maskini, wafungwa, wagonjwa, waliotengwa, wasiopendwa (Yakobo 2:1–13; Mathayo 25). Je, tuko tayari kuungana na watu wanaodharauliwa na wengine?

Ugumu wa moyo dhidi ya huruma

Tunaweza kuitikia makosa ya wengine kwa namna mbili: kwa ugumu wa moyo na hukumu au kwa huruma na unyenyekevu (Warumi 15:1–2).

Paulo na Barnaba walionyesha tabia hizi tofauti (Matendo 15:36–41):

Wakati wa safari ya utume, Paulo alikataa kumchukua Yohana Marko pamoja nao kwa sababu hapo awali kijana huyo alikuwa amekata tamaa kwa sababu ya hofu. Barnaba, kwa upande mwingine, alikuwa na huruma kwa Yohana Marko na aliona uwezo ndani yake. Alikuwa amechagua kumchukua na kumwelekeza.

Hii inaweza kuwa sawa na wazo la kuwa na shauku badala ya kuwa na hukumu. Badala ya kuwahukumu watu, tunauliza maswali na kuona kama kuna zaidi katika hadithi zao.

Jinsi tunavyoshughulikia makosa ya watu inaweza kuathiri mahusiano yetu nao.

Lakini vipi wanapotuumiza?

Hasira au msamaha

A couple hugging each other in forgiveness

Photo by Gus Moretta on Unsplash

Kurekebisha uhusiano inaweza kuwa ngumu sana tunapokuwa tumekosewa. Chaguo kati ya hasira na msamaha ni gumu.

Hii haimaanishi kuwa ni kosa kuwa na hasira. Ikiwa mtu anakudhuru, ni kawaida kuhisi hasira. Lakini tunapoiacha hasira hiyo ikomae na kuwa uchungu, mwishowe inatutafuna—na katika mahusiano.

Mfano mmoja wa chuki ya aina hii ni kati ya Esau na Yakobo. Ilichukua miaka mingi kwa ndugu hawa kusuluhisha ugomvi kati yao baada ya Yakobo kuiba baraka ya Esau kama mzaliwa wa kwanza (Mwanzo 27:34–35, 41–43).

Na bado Yesu anatuita kusamehe badala ya kushikilia uchungu:

lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,” (Mathayo 5:44, SUV).

(Tafadhali kumbuka: Kusamehe mara zote haimaanishi upatanisho. Wakati mwingine, hata baada ya kusamehe, inaweza isiwe salama au sahihi kuendeleza mahusiano—hasa wakati unyanyasaji umetokea.)

Kutokuheshimiana dhidi ya kuheshimu

“….. kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu;” ni mwito wa juu (Warumi 12:10, SUV).

Huenda ukawa na mtu mwenye mamlaka maishani mwako—labda mwajiri, mwana familia, au hata kiongozi wa serikali—ambaye huwezi kumvumilia. Daima kuna majaribu ya kutoa maoni ya pembeni kumhusu nyuma yake, na mara kwa mara kuwageuza watu wengine dhidi yake pia.

Na bado aya hii ya Biblia inatuhimiza tuwaheshimu wazazi wetu (Waefeso 6:1–3), mabosi wetu (mistari 5–8), na viongozi wetu (Warumi 13:1–7).

Maana ya “heshima” ni nini?

Inamaanisha kuwathamini watu, kutambua ubinadamu wao kwa sababu wameumbwa kwa mfano wa Mungu (Mwanzo 1:28). Inamaanisha kuchukua muda kuwasikiliza, badala ya kuwa na mwitikio wa hasira (Yakobo 1:19).

Daudi katika Agano la Kale alionyesha heshima hii alipokuwa akitafutwa na Mfalme Sauli. Ingawa alijua Mungu alikuwa amempa kiti cha enzi, Daudi alikataa kukomesha maisha ya Sauli kwa sababu aliheshimu nafasi ambayo Sauli alipewa na Mungu (1 Samweli 24).

Udanganyifu dhidi ya uwazi

Udanganyifu ni moja ya njia za haraka za kuvunja imani katika uhusiano. Uwazi husaidia kujenga imani hiyo.

Angalia uhusiano wa Yakobo na mkwewe, Labani (Mwanzo 29–31). Badala ya kumruhusu Yakobo kuoa binti yake Raheli kama alivyokuwa ameahidi, Labani alimdanganya Yakobo na kumpa Lea kama mke. Labani pia alimtendea Yakobo kwa udhalimu na kubadilisha mshahara wake mara nyingi (Mwanzo 31:41–42). Kama unavyoweza kufikiria, udanganyifu huo uliweka msuguano mkubwa katika uhusiano wao.

Biblia inapinga hili:

“Msiambiane uongo, kwa kuwa mmevua kabisa utu wa kale, pamoja na matendo yake” (Wakolosai 3:9, SUV).

Uwazi ni muhimu pia wakati mtu mmoja katika mahusiano anaamini amekosewa.

Inaweza kuwa ngumu kuzungumza wakati ambapo umeumizwa. Lakini Mathayo 18 hutoa kanuni za njia nzuri za kumkaribia mtu ambaye ametuumiza. Ingawa kanuni hizo ni maalum kwa mahusiano na washiriki wa kanisa, zinaweza kutumika pia kwa wengine.

Tukiangalia vipengele hivi vinavyoweza kufanya au kuvunja mahusiano, tunajiuliza: Tunawezaje kutumia mambo haya katika maisha yetu wenyewe?

Wakristo wanawezaje kufuata mfano wa Kibiblia”?

A man kneeling in church with his head in his hands, asking God to help him in his relationships

Photo by Samuel Martins on Unsplash

Yesu ametuwekea mfano wa jinsi ya kujenga mahusiano yenye afya. Kufuata mfano wa kibiblia wa mahusiano huanza kwa kuwa na urafiki Naye. Kisha, tunapoyatazama maisha yake, yanaturuhusu kutafakari juu ya mwingiliano wetu na wengine na kuomba Roho Mtakatifu Atubadilishe maisha yetu.

Tunapojisalimisha kwake, Yeye hutupa nguvu ya kuishi upendo wake.

Tunaelewa—inaonekana rahisi wakati mahusiano yanapoonekana kuwa magumu. Kama Wakristo, mara nyingi tunajua tunachopaswa kufanya lakini tunapambana kufanya hivyo (Warumi 7:15-20).

Unajua unapaswa kumheshimu mwenzako kazini ambaye ni mkorofi lakini unajikuta unataka kumjibu kwa ukali. Unajua hauitaji kuthibitisha hoja yako, lakini huwezi kujizuia unapogombana na mwenzi wako.

Hapa kuna jambo kuhusu upendo. Sio hisia tu. Upendo wa Kibiblia—ule ambao Mungu anawakilisha—ni tendo (1 Yohana 3:18). Wakati Roho Mtakatifu anapofanya kazi maishani mwetu, Yeye hutupa nguvu ya kuishi hata wakati ambapo hatujisikii.

Hebu tuangalie hatua zitakazotusaidia kupata uzoefu huu:

Tafuta urafiki na Mungu

Kabla hatujaweza kuwa na mahusiano yenye afya na watu wengine, tunahitaji urafiki na chanzo cha upendo Mwenyewe. Tunapomjua Yeye ni nani na jinsi anavyo husiana na watu, upendo Wake utatujaza (1 Yohana 4:12).

Chukua muda wa kumjua Mungu. Zungumza naye kwa maombi na soma ujumbe wake kwako katika Maandiko. Tumia muda kujifunza kuhusu maisha ya Yesu na jinsi alivyo watendea watu.

Jitathmini

Kadri unavyosoma kuhusu upendo wa Mungu na kusudi lake kwa mahusiano mazuri, mwombe akutafute moyoni mwako (Zaburi 139:23–24) na kukufunulia maeneo ambayo unaweza kukua.

Mawazo na hisia huweka msingi wa matendo yetu (Methali 23:7; 4:23), hivyo jiulize: Ni mawazo gani yanayo chochea matendo yangu?

Kusoma Maandiko kutakusaidia katika mchakato huu. Yanazungumza na mioyo yetu na kufichua nia zetu (Waebrania 4:12).

Omba kwa ajili ya Roho Mtakatifu

Kuona maeneo ya ukuaji katika maisha yetu kunaweza kuwa jambo chungu na la kukatisha tamaa. Tunaweza kujiuliza ikiwa tunaweza kufikia kiwango cha Mungu.

Vizuri, sio kwa nguvu zetu wenyewe! Lakini tunaweza kuomba Roho Mtakatifu atubadilishe—kutoka ndani kwenda nje. Na Yeye yuko tayari zaidi.

Wakati anapoingia mioyoni mwetu, yeye huiweka sheria yake ya upendo huko (Waebrania 8:10) na kutupa tunda la Roho (Wagalatia 5:22–23):

  • Upendo
  • Furaha
  • Amani
  • Subira
  • Upole
  • Wema
  • Imani
  • Upole
  • Kiasi

Ndio maana ni muhimu sana kwamba tuombe uwepo wa Roho Mtakatifu kila siku.

Jisalimishe kwa Mungu

Kufuata kanuni za Kibiblia kuhusu mahusiano haimaanishi hatutakutana na changamoto. Lakini tunapokutana nazo, tunaweza kuziona kama fursa ya kujisalimisha kwa Mungu.

Kujisalimisha ni mchakato endelevu wa kujitoa kwetu Kwake. Tunapopitia mawazo hasi na majaribu, tunaweza kujisalimisha kwake wakati huo (2 Wakorintho 10:3–5). Yeye, kwa upande wake, hutupa nguvu Zake.

Kujisalimisha kunaweza kuwa jambo gumu. Inamaanisha kukubali kile ambacho Mungu anasema ni sahihi – hata kama hatujisikii kusema au kufanya hivyo wakati huo.

Lakini hapa ndipo ahadi ilipo: Tunapomtii na kumpinga ibilisi, tutapata ushindi (Yakobo 4:7).

Chukua hatua ya kwanza ya upendo

Kama tulivyosisitiza tayari, upendo ni uamuzi wa kuchukua hatua—bila kujali unavyojisikia kuhusu mtu huyo. Na kuna wakati tunapaswa kuchukua hatua hiyo.

Fikiria jinsi Yesu alivyochukua hatua alipokusanyika na wanafunzi wake kwa Karamu ya Mwisho katika Yohana 11. Kawaida, mtumishi angeosha miguu ya wageni, lakini hapakuwa na mtumishi.

Wanafunzi walikataa kusogeza hata kidole kusafisha miguu ya wenzao. Hawakutaka kujinyenyekeza hadi kiwango hicho! Hasa kwa kuwa mara nyingi walikuwa wakigombana kuhusu ni nani aliye mkuu kati yao (Luka 22:24–27).

Lakini Yesu alichukua hatua.

Alichukua taulo na beseni la kutawadhia ili kufuta miguu yenye vumbi ya wanafunzi wake. Yote kwa sababu ya upendo.

Halikuwa jambo la kifahari kwa namna yoyote. Lakini linatuonyesha upendo ni nini kwa uhalisia – kufanya kinachotakiwa kufanywa ili kuwahudumia wale tunaohusiana nao. Upendo unachukua hatua.

Unaweza kuwa na mahusiano yenye afya

Ukifikiria kuhusu mahusiano yako, jipe moyo kwamba Mungu amekupa njia ya kufanya mahusiano hayo kustawi. Kanuni za Biblia na nguvu ya Mungu pamoja vitakusaidia kuingiliana na watu kwa njia yenye afya.

Changamoto itakuwa tofauti kwa kila mtu.

Mwenzi baridi.
Uhusiano wa ndugu wenye msuguano.
Mfanyakazi mwenza anayekusengenya.
Mfanyakazi mwenye mabadiliko ya tabia katika ofisi yako ya posta.

Lakini mwishowe, Yesu anatuita tuishi upendo Wake usio na masharti na kumkubali kila mtu tunayekutana naye. Mambo mazuri yanaweza kutokea.

Kwa zana zaidi za mahusiano ya Kibiblia,

Chagua Masomo ya Biblia Mtandaoni

Unataka kuendelea kujifunza? Pata habari zaidi kuhusu Yesu, mwanadamu, mpango wa wokovu, na jinsi Mungu anavyokupenda kiasi cha kutosha kujitolea kila kitu, ili tu kukupatia nafasi ya kumchagua.

Wakati mwingine inaweza kuwa ngumu kujua pa kuanzia, ndio maana tunatoa chaguo za masomo ya Biblia mtandaoni bure, rahisi kutumia, unaweza kufanya wakati wowote, mahali popote, na kwa kasi yako mwenyewe.

Shule hii ya Biblia mtandaoni itakuelekeza kupitia mada kuu za Maandiko, ikivunja dhana ngumu za Biblia katika vipande vidogo, ambavyo vinaweza kukusaidia kupata majibu ya maswali magumu zaidi ya maisha.

Kurasa Zinazohusiana

  1. Genesis 6:18; 15:1; Exodus 19:5; Leviticus 26:45; Deuteronomy 7:9; Judges 2:1; 2 Chronicles 15:12; Nehemiah 1:5; Psalm 25:14; 89:28; Isaiah 54:10; 55:3; Jer. 31:33; 32:40; Ezekiel 16:8. []
  2. See also Hosea 2:16, 19; 2 Corinthians 11:2 []
  3. Psalm 103:13; 2 Samuel 7:14–15; Luke 15:11–32; Hebrews 12:7 []

Je, Una swali kuhusu Waadventista? Uliza hapa!

Pata majibu kwa maswali yako kuhusu Waadventista Wasabato

Majibu Zaidi

Jinsi Biblia Inavyotafsiri Upendo

Jinsi Biblia Inavyotafsiri Upendo

Neno “upendo” linatumika katika namna ya kihisia sana, ya muda mfupi, na isiyo na maana. Hapa tunaangalia maelezo yote ya Biblia kuhusu upendo wa kweli, ambao ni mkubwa na wa kina zaidi.

Je, Ni Kawaida Wakristo Kuwa na Mashaka?

Je, Ni Kawaida Wakristo Kuwa na Mashaka?

Ndio, ni kawaida kabisa kwa Wakristo kupitia vipindi vya mashaka katika maisha yao ya kiroho. Kila mtu ameshawahi kuwa na mashaka wakati mmoja au mwingine, hata wachungaji, wanatheolojia, na watu muhimu katika Biblia.

Kile Mfano wa Yesu Kinatufundisha Kuhusu Maombi na Kufunga

Kile Mfano wa Yesu Kinatufundisha Kuhusu Maombi na Kufunga

Kufunga na kuomba vilikuwa sehemu muhimu ya huduma ya Yesu Duniani. Hebu tujifunze jinsi mfano wa Yesu unavyoweza kutufundisha jinsi ya kuwa na uhusiano wa karibu zaidi na Mungu. Kufunga na kuomba vilichukua sehemu kubwa ya huduma ya Yesu Duniani.