White, mmoja wa waanzilishi wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, aliamini kwamba elimu haikuwa kamili isipokuwa ilipojengwa juu ya kanuni za Biblia.
Ni muhimu katikEllen a kuwapatia wanafunzi mfumo wa kuelewa kila sehemu nyingine ya maisha.
Lakini Biblia inahusianaje na hesabu au sayansi? Je, ni muhimu kuunganisha Biblia na kazi ya shule?
Tutajibu maswali haya kwa kutazama:
- Kwa nini Ellen White alijali elimu
- Mawaidha yake kuhusu elimu inayotegemea Biblia
- Ushauri wake kuhusu elimu ulitoka wapi
- Jinsi ya kutumia Biblia darasani
Kwanza tupate historia kidogo kuhusu msisitizo wa Ellen White kuhusu elimu.
Kwa nini Ellen White alijali elimu

Photo by Max Fischer
Ellen White alijikita sana katika elimu kwa sababu alitambua athari yake inayozagaa katika sehemu nyingine zote za maisha. Kama vile Mithali 22:6 inavyosema, mwelekeo wa maisha ya mtu unajengwa wakati wa mafunzo yanayopokelewa katika miaka ya awali. Elimu inayowaongoza watoto kumjua Mungu ni muhimu kwa sababu itawaathiri kwa maisha yao yote—na labda hata milele.
Ellen White alipigania elimu inayogusa maisha yote ya mtu—ambayo aliiita elimu ya kweli.
Aina hii ya elimu ilikwenda zaidi ya mambo matatu ya msingi. Aliasisitiza kwamba “ni maendeleo yenye upatanifu ya nguvu za kimwili, kiakili, na kiroho.”1
Pia inajumuisha huduma, kanuni kuu ya Ukristo: “Inamwandaa mwanafunzi furaha ya huduma katika ulimwengu huu na kwa furaha kuu ya huduma kuu zaidi katika ulimwengu ujao.”2
Akichukua hatua moja zaidi, aliandika kwamba elimu, katika maana yake ya juu kabisa, inahusiana na kazi ya ukombozi. Zote zina msingi wao katika Yesu Kristo.3
Na ikiwa elimu inahusiana sana na ukombozi, inaleta maana ikiwa Biblia ina nafasi muhimu katika vyote viwili.
Mafundisho ya Ellen White kuhusu elimu inayotegemea Biblia
Ellen White aliamini katika kuwa na Biblia kama msingi wa elimu. Aliandika, “Biblia ni mwalimu mkuu; kwani haiwezekani kusoma kurasa zake takatifu kwa maombi bila akili kufundishwa, kuinuliwa, kusafishwa, na kutakaswa.”4
Ingawa Neno la Mungu sio kitabu kamili cha kila somo, linatoa mtazamo wa ulimwengu ambao unaweza kuunda jinsi mwanafunzi anavyofikiria kuhusu maisha.
Na inafanyaje hili?
Kwanza kabisa, Biblia inatuonyesha asili yetu na kusudi letu kuu.
Inatuonyesha kwamba Mungu aliwaumba wanadamu ili waakisi sura yake. Lakini kwa kiasi kikubwa, tulipoteza mfano wa Mungu wakati Adamu na Hawa walipochagua kumuasi (Mwanzo 3). Elimu inayotegemea Biblia inachangia katika kuturejesha ili tuweze kuakisi tena tabia ya Mungu.5
Urejeshwaji huu unahusisha elimu na mada ya Pambano Kuu katika Biblia.6 Pambano Kuu ni vita visivyoweza kuonekana kati ya mema na mabaya—Mungu na Shetani—vinavyoendelea wakati huu. Shetani amefanya kazi kwa bidii kukengeusha ufahamu wetu kuhusu Mungu na kumgeuza kuwa kitu ambacho yeye siyo.
Kuelimisha watoto ndani ya mfumo wa Kibiblia kunaweza kuwasaidia kuona tabia halisi ya Mungu na jinsi upendo wa Mungu unavyoweza kubadilisha maisha yao.
Linapokuja swala la matumizi ya Biblia darasani, Ellen White alitoa mwongozo ulio sawa. Neno la Mungu lisingeweza kuwekwa tu kwenye mtaala ili “kutia ladha” masomo mengine.7
Aliandika,
“Biblia isiletwe katika shule zetu ili iwekwe kati ya ukafiri. Biblia lazima iwe msingi na somo kuu la elimu.”8
Kwa maneno mengine, walimu na wanafunzi wasichukulie Biblia kama kitabu kingine chochote ambacho kinaweza au kisichoweza kulingana na mafundisho ya Kikristo. Badala yake, Biblia ndiyo mamlaka ya kutathmini kila kitabu kingine.
Lakini Biblia haitawezi kuwa kitabu pekee cha kufundishia. 9Sio kila somo lipo katika Biblia.
Kilichopendekezwa na Ellen White ni elimu kupitia lenzi ya mtazamo wa Kibiblia. Hii inamaanisha kwamba somo linakuza viwango vya Biblia na kuwaelekeza wanafunzi kwa Yesu. Wanafunzi wanajifunza kutathmini kila kitu kulingana na kanuni za Biblia.
Lakini lengo la mfumo wa Kibiblia ni lipi baada ya mtoto kumaliza shule?
Mithali 22:6 inatuambia,
“Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee” (SUV).

Photo by Stormseeker on Unsplash
Hii ndio lengo la elimu ya Kibiblia—kuwafundisha wanafunzi kutumia Biblia kufikiri na kufikiria wenyewe maisha yao yote. Ellen White alisema,
“Kazi ya elimu ya kweli ni kukuza uwezo huu, kuwafunza vijana kuwa wafikiriaji, na si tu wapokeaji wa mawazo ya watu wengine.”10
Kama matokeo yake, wanafunzi watakuwa na uwezo wa kutambua ukweli kwa msaada wa Roho Mtakatifu na kushiriki ukweli huo kwa ufanisi na wengine.
Aina hii ya elimu inatuandaa kuwa raia wema na mashahidi kwa Kristo.
Hivi ndivyo Ellen White alivyoelezea falsafa hii:
“Maandiko Matakatifu ni kiwango kamili cha ukweli, na kwa hivyo yanapaswa kupewa mahali pa juu katika elimu. Ili kupata elimu inayostahili jina, lazima tupate maarifa ya Mungu, Muumba, na ya Kristo, Mkombozi, kama wanavyofunuliwa katika Neno takatifu.”
Sasa tumeona mashauri yake kuhusu elimu inayotegemea Biblia, hebu tuone mashauri haya yalitoka wapi.
Ushauri wa Ellen White kuhusu elimu ulitoka wapi
Kila kitu ambacho Ellen White alifundisha kuhusu elimu kimejikita kabisa katika Biblia na kweli ambazo Roho wa Mungu alimwagiza.
Muktadha ambao alikuwa anaishi ulichangia pia katika shauku yake ya kuboresha mazoea ya elimu. Basi elimu ilikuwaje katika siku zake?
Elimu katika wakati wa Ellen White

Photo by Austrian National Library on Unsplash
Katika miaka ya 1800, elimu katika nchi zilizostawi kiuchumi ilikuwa tofauti kabisa na ilivyo leo. Nchini Marekani, shule nyingi zilikuwa za chumba kimoja za vijijini ambapo wanafunzi walifundishwa “k tatu” yaani kusoma, kuandika, na kuhesabu. Ingawa sehemu kubwa ya masomo ilikuwa ya maadili na vitendo, njia kuu ya kujifunza ilikuwa kwa kukariri. Wanafunzi hawakulazimika kufikiri kwa kina kuhusu walichokuwa wakijifunza.11
Nyumba za shule zilikuwa giza, na harakati kidogo za kimwili ziliruhusiwa nje ya mapumziko. “Kuleta mchezo” kulipelekea adhabu kali.
Kama matokeo yake, elimu ilikuwa upande mmoja, ikilenga katika kuendeleza uwezo wa kiakili zaidi ya ule wa kimwili.
Shule chache zenye kiwango cha juu mara nyingi zilifundisha mtaala wa kizamani.12 Wanafunzi, kwa kiasi kikubwa wanaume vijana, walijifunza sanaa na kusoma maandishi ya wafikiriaji wa kale, kama vile Cicero, Plato, na Homer. Waandishi hawa walikuwa wamejawa na falsafa ya Kigiriki na Kirumi, ambayo mara nyingi ilipingana na kanuni za Kibiblia.
Wakati huo nchini Marekani, kipindi cha Transcendentalism kilikuwa kinaendelea kwa kasi, na mawazo yake kuhusu wema wa asili wa binadamu yalipingana na mafundisho ya Biblia kwamba mwanadamu ni mwenye dhambi na anahitaji Mwokozi.
Elimu ilihitaji msaada, na Ellen White alijitokeza kufanya awezalo kwa ajili ya kizazi kijacho. Ingawa alikuwa pia alivutiwa na mapendekezo ya wanamatengenezo katika elimu, Biblia ilikuwa mwongozo wake mkuu.
Biblia na ushauri wa Mungu
Biblia ilikuwa na mvuto katika kila sehemu ya ushauri wa kielimu wa Ellen White. Mara nyingi alinukuu aya za Maandiko na kutumia kanuni zake wakati wa kueleza njia za kufundishia.
Kwa mfano, katika kitabu chake cha Elimu, yeye anaelezea elimu kutoka wakati wa Adamu na Hawa hadi Waisraeli na kuchota kanuni za leo.
Kama vile Waisraeli walivyofundishwa kuwaelimisha watoto wao katika maarifa ya kweli ya Mungu, aliwahimiza walimu kufanya sheria ya Mungu sehemu ya vitendo vya kila siku:
“Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako; nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo” (Kumbukumbu la Torati 6:6-7, SUV).
Ellen White alipokuwa akiandika mawazo haya, Mungu alikuwa akimwongoza. Ingawa hakurekodi maono maalum kuhusu mada hiyo, aliandika kwamba “mada ya elimu imeonyeshwa kwangu kwa njia tofauti, katika mitazamo mbalimbali, kwa vielelezo vingi, na kwa maelezo moja kwa moja, sasa kwenye sehemu moja, na tena kwenye nyingine.”13
Hebu tuangalie jinsi tunavyoweza kufanya ushauri wake katika matumizi maishani.
Jinsi ya kutumia Biblia darasani
Kama tulivyosema awali, wanafunzi wanaweza kufundishwa kutathmini kila somo kupitia mtazamo wa Kibiblia. Hapa kuna njia za kufanya hivyo:
Tumia mada za Biblia kwa ajili ya mada ya insha
Wakati wa kufundisha wanafunzi jinsi ya kuandika, walimu wanaweza kuwapa mada za insha ambazo zinawahimiza kutafuta majibu katika Biblia. Wanafunzi pia wanaweza kusoma kuhusu tabia au mada katika Biblia, kama vile imani au shauku, na kuandika kuhusu ugunduzi wao.
Toa mazoezi ya kusoma kutokana na maisha ya watu katika Biblia
Biblia ni mkusanyiko wa visa vya kipekee ambavyo vinaweza kutumika kujifunza wahusika wake wakuu.
Ellen White alisema kwamba kwa sababu Mungu ndiye mwandishi wa mwisho wa Biblia, wasifu wa wahusika wake hauna upendeleo wa kibinadamu unaopatikana kwa kawaida katika visa vingine:
“Hakuna sehemu yoyote ya Biblia yenye thamani kubwa kuliko maisha ya watu. Wasifu wake ni tofauti mwingine wote kwa kuwa ni za kweli kabisa. Ni vigumu kwa akili yoyote ya kibinadamu kufasiri kwa usahihi, katika mambo yote, jinsi mtu mwingine anavyofanya kazi. Hakuna mwingine ila [Mungu]…[anaweza] kuchora tabia, au kutoa kwa uaminifu picha ya maisha ya mwanadamu.”14
Kupitia kusoma hadithi za Biblia, wanafunzi pia watapata kujifunza kanuni ya sababu na matokeo: matendo huwa na matokeo. Ellen White anasema hivi:
“Hakuna ukweli ambao Biblia inafundisha wazi zaidi kuliko kwamba tunachofanya ni matokeo ya jinsi tulivyo. Kwa kiwango kikubwa uzoefu wa maisha ni matokeo ya mawazo na matendo yetu wenyewe.”15
Fundisha sayansi kutoka mtazamo wa Kibiblia, ukitumia kisa cha Uumbaji

Image by Gnattyone from Pixabay
Walimu wanaweza kutumia mtaala wa uumbaji, pamoja na kujifunza kisa cha Uumbaji, ili kuwaweka wanafunzi katika mtazamo wa Kibiblia kuhusu asili yetu.
Jifunze mbinu za utawala katika nyakati za Biblia
Wakati wanafunzi wanajifunza kuhusu aina za serikali za kisasa, wanaweza pia kujifunza jinsi serikali zilivyokuwa katika vipindi tofauti vya historia ya Biblia. Kwa mfano, aina maalum ya serikali ambayo Mungu aliunda kwa Waisraeli ikilinganishwa na zile za mataifa mengine yaliyotajwa katika Biblia, kama vile Wababeli, Waajemi, na Warumi.
Jumuisha visa vya Biblia katika kujifunza historia
Mara nyingi tunaitazama Biblia kama kitabu cha kiroho, lakini pia ni hazina tajiri ya historia ya kale. Kwa kweli, Taasisi ya Utafiti wa Uumbaji inasema,
“Biblia imeonyesha kuwa sahihi kihistoria na kiajemi zaidi kuliko kitabu kingine chochote cha zamani. Imewekwa chini ya uchambuzi wa kisayansi wa maandishi kwa undani kabisa unaowezekana kwa binadamu na imeonyeshwa kuwa halisi kwa kila njia.”
Kwa nini usiitumie kama chanzo katika mtaala wako wa historia ya ulimwengu?
Elimu inayotegemea Biblia inakuza watu wenye uwezo wa kufikiri.
Ellen White alihitimisha mawazo yake katika matumizi ya Biblia kwa kauli moja:
“Katika kurasa zake zimepatikana historia ya kale zaidi; wasifu wa kweli kabisa; kanuni za serikali kwa udhibiti wa nchi, kwa udhibiti wa familia – kanuni ambazo hekima ya kibinadamu haijawahi kufikia.”16
Hata kama wanafunzi hawashiriki moja kwa moja katika kujifunza Biblia, walimu wao wanaweza kufuma kanuni hizo katika sehemu nyingi za darasani. Biblia inaweza kuwa kigezo cha kufanyia majaribio mada na shughuli zote nyingine.
Kwa namna hii, watoto wanabeba msingi imara wanapokuwa watu wazima—uwezo wa kufikiri kwa ajili yao wenyewe na kutathmini maisha kulingana na Biblia.
- White, Ellen G., Education, p. 13 [↵]
- Ibid. [↵]
- Ibid., p. 30 [↵]
- White, Ellen, Christian Education (International Tract Society, 1894), p. 103 [↵]
- Douglass, Herbert E., Messenger of the Lord, p. 346 [↵]
- Ibid. [↵]
- bid., p. 347 [↵]
- White, Ellen G., Fundamentals of Christian Education, p. 474 [↵]
- Messenger of the Lord, p. 347 [↵]
- Education, p. 17 [↵]
- Knight, George, “The Transformation of Education” in Land, Gary, The World of Ellen White, pp. 162-163 [↵]
- Ibid. [↵]
- Fundamentals of Christian Education, p. 310 [↵]
- Education, p. 146 [↵]
- Ibid. [↵]
- Ibid., p. 125 [↵]
Majibu Zaidi
Ushauri wa Kiroho wa Ellen White kuhusu Ndoa
Kama mmoja wa waasisi wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato, Ellen G. White aliheshimiwa sana.
Mafundisho ya Ellen G. White kuhusu Elimu ya Chuo
Ellen G. (Harmon) White, mwanzilishi muhimu wa Waadventista wa Sabato, mara nyingi anajulikana kwa mwongozo wake wa vitendo na kiroho kuhusu elimu sahihi kwa watoto.
Maono na Unabii wa Ellen White
Agano Jipya linathibitisha unabii kama karama ya Roho ambayo itaendelea hadi mwisho wa wakati (Waefeso 4:11–14).
Vidokezo 8 vya Ushauri kwa Familia kutoka kwa Ellen White
Familia—inaweza kuwa chanzo cha sehemu yenye kufurahisha na yenye kuleta changamoto katika maisha.
Ellen G. White Alitoa Ushauri Gani kuhusu muziki?
Ellen G. White Alitoa Ushauri Gani kuhusu muziki?Katika kiini chake, muziki ni mkusanyiko wa sauti, muinuko wa sauti na mapigo ambayo huleta wimbo. Pia ni zaidi ya hayo. Kama aina yoyote ya sanaa, inaweza kuwa nzuri sana au mbaya sana, yenye kusisimua au yenye...
Mwongozo wa Ellen G. White kuhusu Elimu ya Kikristo
Ellen White, mwanzilishi wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, aliona kuwa mfumo wa elimu nchini Marekani wakati wake ulikuwa haukidhi mahitaji.
Hazina ya Ellen G. White Ni nini ?
Mchango wa Ellen G. White katika uundaji na ukuaji wa Kanisa la Waadventista wa Sabato ni sehemu muhimu ya historia yake.
Kuelewa Maisha na Huduma ya Ellen G. White
Jifunze Ellen G. White ni nani hasa na jukumu alilokuwa nalo katika kuongoza Kanisa la Waadventista Wa Sabato mapema kupitia huduma yake na maandishi yaliyoongozwa na Roho Mtakatifu.
Sabato katika Maisha na Mafundisho ya Ellen White
Sabato katika Maisha na Mafundisho ya Ellen WhiteSabato ni mada muhimu katika Kanisa la Waadventista wa Sabato. Sio jambo la kushangaza, basi, kwamba Ellen G. White, mwanzilishi mwenza wa kanisa, alisoma mafundisho ya Biblia kuhusu Sabato na akaandika kiasi kikubwa...
Urithi wa Kudumu wa Ellen G. White
Urithi wa Kudumu wa Ellen G. WhiteEllen G. White ni jina linalojulikana sana miongoni mwa Waadventista wa Sabato, lakini pia aliathiri sehemu nyingi za historia, mbali na kuwa mwanzilishi wa Kanisa la Waadventista wa Sabato. Ndiyo maana Jarida la Smithsonian...
Hatua Kuelekea kwa Kristo: Mwongozo wa Uhusiano na Yesu
Iwe unanza safari yako na Yesu Kristo, unarejea baada ya muda fulani, au umekuwa na uhusiano na Yesu kwa miaka, kutumia kitabu
Wafahamu Watoto wa Ellen White
Ellen White, ambaye ni mmoja wa waanzilishi maarufu zaidi wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, alikuwa na watoto wanne na mumewe, James: Henry Nichols, James Edson, William Clarence, na John Herbert.
Jinsi Mafundisho ya Ellen White Yanavyoweza Kuboresha Afya Yako
Matibabu katika karne ya kumi na tisa yalisemekana kuacha “ugonjwa zaidi kuliko yalivyotibu” kwa matumizi yake ya kutoa damu na “dawa” kama zebaki na arseniki.
Jinsi Ellen White Alivyochangia Ujumbe wa Afya wa Waadventista
Jinsi Ellen White Alivyochangia Ujumbe wa Afya wa WaadventistaWaadventista wa Sabato wanajulikana kwa kusisitiza maisha yenye afya bora. Na Ellen G. White alikuwa na ushawishi mkubwa katika maendeleo ya kipaumbele hiki na utekelezaji wake miongoni mwa Waadventista....
Ellen White anasema nini kuhusu Maombi?
Je, umewahi kuwa na mzigo ambao ulihitaji kumwambia mtu, lakini uliogopa kuhukumiwa ikiwa ungefanya hivyo?
Ellen G. White au Biblia—Kipi ni Muhimu Zaidi kwa Waadventista?
Biblia—bila shaka—ndiyo kitabu muhimu zaidi. Ni kipimo tunachotumia kupima maandishi mengine yote, ikiwa ni pamoja na yale ya Ellen White.
Ellen G. White Alisaidia Vipi Katika Kuanzisha Kanisa la Waadventista wa Sabato?
Ellen G. White, mwanamke mnyenyekevu kutoka Gorham, Maine, alikuwa mmoja wa waanzilishi wa Kanisa la Waadventista wa Sabato na kiongozi muhimu tangu mwanzo wake.
Ellen White na Kitabu cha Pambano Kuu
Pambano Kuu ni moja ya vitabu vya Ellen G. White vinavyo thaminiwa zaidi na Waadventista wa Sabato.
Roho ya Unabii Ni nini (Kitabu cha 1-4) na Ellen G. White?
Kutumia unabii wa Biblia katika historia, matukio ya hivi karibuni, na hasa siku za usoni, inaweza kuwa kazi ngumu. Hata linaweza kuwa jambo la kutisha kidogo kwa baadhi.
Ellen White Alifundisha nini Kuhusu Matumizi ya Vyakula Vinavyotokana na Mimea?
Moja ya mambo ambayo unaweza kuwa umewahi kusikia kuhusu Waadventista wa Sabato ni msisitizo wao kwenye mtindo wa maisha wa kutumia vyakula vinavyotokana na mimea.



















