Ellen G. White ni jina linalojulikana sana miongoni mwa Waadventista wa Sabato, lakini pia aliathiri sehemu nyingi za historia, mbali na kuwa mwanzilishi wa Kanisa la Waadventista wa Sabato. Ndiyo maana Jarida la Smithsonian lilimtambua kama mmoja wa Wamarekani 100 wenye ushawishi mkubwa wakati wote.
Kwa hiyo, ni nini kuhusu maisha ya Ellen White kilicholeta aina hii ya ushawishi na mvuto wa kudumu? Sio tu kwamba alisaidia kuongoza Kanisa la Waadventista wa Sabato katika maeneo ya elimu na afya, pia aliandika zaidi ya vitabu 40 (na nakala kama 5,000 ya jarida) ili kuwaongoza watu kuelekea kuwa karibu zaidi na Yesu.1
Na japo huduma yake ilifanyika zaidi ya karne moja iliyopita, ushauri wake ulio-ongozwa na Roho unaendelea kubariki na kuongoza watu hata katika karne ya 21.
Hebu tuangalie sehemu tofauti za maisha yake zilizo changia urithi aliouacha. Tutajadili:
- Maisha yake binafsi na ya familia
- Uwanja wa elimu
- Mafundisho ya Waadventista
- Uwanja wa afya
- Maandishi yake
Na katika kila jambo alilofanya, daima alimpatia Mungu utukufu.
Hebu tuanze kwa kuangalia jinsi urithi wake unavyoendelea kuishi kupitia familia yake.
Urithi binafsi na wa Familia

“Courtesy of the Ellen G. White Estate, Inc.”
Ellen White alikuwa na watoto wanne wa kiume, lakini ni wawili pekee waliobaki hai hadi kuwa watu wazima.
Wavulana hawa wawili, Edson na Willie, walikua na kufuata nyayo za mama yao katika kuhudumu kwenye kazi ya Mungu.
Shauku yake kuu kwa watoto wake ilikuwa kila mmoja ampokee Mungu kama mwokozi wao binafsi.2
Alijitahidi sana kuweka mfano mwema kwao, kuwakumbusha kujenga tabia zao kuwa kama Yesu—wenye huruma, wenye kuelewa, wenye kusudi, na muhimu zaidi, wakielekeza macho yao kwa Baba yao wa mbinguni.
Ingawa alikuwa na shughuli nyingi za kutunza nyumba yake, kuandika vitabu, na kusafiri huku akitumika katika majukumu mbalimbali ya huduma, alihakikisha watoto wake wanajua wanathaminiwa na kupendwa. Mara nyingi aliandika barua binafsi kwa kila mmoja wao alipokuwa mbali.
Ilikuwa katika barua hizi ambapo tunaweza kupata mtazamo wa aina ya mama ambaye Ellen White alikuwa. Aliandika mara kwa mara wanapokuwa mbali, kuwaeleza kuhusu safari yake.3 Na alikuwa makini kuonyesha maslahi binafsi katika maisha ya watoto wake, akiuliza kuhusu walichokuwa wanafanya na changamoto za hivi karibuni walizokuwa wakikabiliana nazo.4
Kama mama mzuri yeyote, alisaidia kutoa ushauri na kuwaongoza. Na katika barua zake angejumuisha himizo maalum la kumpenda na kumfuata Yesu.5
Kutoka katika maandishi yake na hadithi zilizoandikwa kumhusu, tunaweza kujifunza mengi kuhusu tabia tofauti tofauti za watoto wake, Willie na Edson. Willie kwa ujumla alikuwa mtiifu zaidi na mwenye kufuata maagizo kwa urahisi, wakati Edson alionekana kuwa mkaidi zaidi, akielekea kufanya mambo kwa njia yake mwenyewe.6 Na alijua Mungu alikuwa na mipango ya kipekee kwa kila mmoja wao.

James Edson
Mara nyingi Edson na baba yake, James White, walikuwa wakigombana kuhusu maamuzi mabaya ambayo Edson angefanya—hasa jinsi alivyoshughulikia pesa.7 Lakini mara nyingi Ellen White alisimama kidete kwa ajili ya Edson, akiuona uwezo wake na kujua kwamba Mungu kamwe hangekata tamaa naye, na wala yeye kamwe hangekata tamaa juu yake.8
Lakini wakati mmoja katika maisha yake, Edson alikata tamaa sana kiasi kwamba aliamua kuacha kabisa imani yake kwa Mungu.9
Ellen White alihuzunika sana kwa uamuzi wake. Na ingawa aliheshimu haki yake ya kuchagua, alimsihi katika barua zake amrudie Mungu.10
Ilipofika wakati huo, Mungu alimpa ndoto ya ishara ya Edson akizama kwenye mawimbi.11 Hii iliwakilisha hali yake ya kiroho iliyokuwa mbaya, na jinsi alivyohitaji mkono wa msaada kumsaidia kubaki juu ya maji wakati wa mapambano yake ya kiroho yaliyokuwa na changamoto nyingi.12
Alimsimulia Edson ndoto hii, sio kwa lengo la kumtishia, bali kumwonyesha ukweli wa maamuzi yake ya kukataa Mungu ungekuwa na maana gani.
Kwa kutafakari juhudi na uaminifu wa mama yake kwa ustawi wake wa kiroho, uzoefu huu hatimaye ulimshawishi Edson kwamba alihitaji mabadiliko ya mwelekeo katika maisha yake. Alikubali tena kumkaribisha Mungu moyoni mwake.13
Mabadiliko yake yalitokana kwa sehemu na juhudi za mama yake zisizochoka. Pamoja, walifurahia uhuru mpya ambao alifanikiwa kupata katika uhusiano wake na Mungu. Edson alihisi uongozi wake mtakatifu alipotimiza hatimaye shauku yake ya kuwa baharia.
Kwa kushuhudia uaminifu wa Ellen White kwa Mungu, na kwa ulimwengu na watoto ambao Anawapenda, wanawe walihamasishwa pia kutumia vipaji vyao kwa ajili ya Mungu.
Kwa mashua yake ya mvuke, Edson alianzisha huduma ya elimu kwenye Mto Mississippi kwa Wamarekani Weusi.14 Zamani alikuwa amefanya kazi kama mchapishaji, mtengenezaji wa vitabu vya nyimbo, mwandishi, na pia alisaidia na Chama cha Shule ya Sabato cha Konferensi Kuu.15
Kwa wakati huo, Willie alikuwa msaidizi wake na mwandamizi wa safari alipokuwa akisafiri nje ya nchi kusaidia kuanzisha na kuhamasisha juhudi za huduma za ziada za kusaidia kusambaza Injili.16 Katika maisha yake yote, Willie alikuwa mhariri na msimamizi, pamoja na majukumu mengine kama kutumika Bodi ya Chuo cha Battle Creek na kusaidiana na Chama cha Shule ya Sabato.17 Baadhi ya nafasi nyingine muhimu ni pamoja na jukumu lake kama mmoja wa wakurugenzi wa Taasisi ya Mageuzi ya Afya na makamu wa rais wa Chama cha Uchapishaji cha Waadventista wa Sabato.18 Hata alikuwa rais wa Union Konferensi Mkutano wa Muungano wa Australia.19
Ellen White alijivunia taaluma za utumishi za wanawe wote wawili. Aliwaombea mara kwa mara na alitamani kuwepo daima kwa ajili yao katika changamoto zao, kuwatia moyo waendelee kufanya kazi ya Mungu.
Kwa ujumla, alifurahi kuona kizazi kijacho kikichukua kazi yake kwa Bwana. Alijua kwamba kazi hiyo haimtegemei yeye. Alikuwa tu chombo tayari kwa Roho Mtakatifu kufanya kazi yake.
Ellen White alifariki mwaka 1915. Lakini aliacha watoto wake na kumbukumbu za huduma yake ya kipekee na njia za ajabu ambazo Mungu alimtumia. Huu ulikuwa ni uzoefu wa thamani kubwa uliokuwa nyongeza ya upendo wake wa kweli kwa wanawe, na shauku yake ya kusaidia kila mtu kujifunza kuhusu Yesu.
Urithi wake katika uwanja wa elimu

Marienhohe Adventist College, Darmstadt, Germany
Kutokana na shauku hiyo ya kusaidia watu ulimwenguni kujifunza kuhusu Yesu Kristo ni nani kwa kweli, Ellen White alitoa mchango katika uga wa elimu kwa kuhamasisha Waadventista kuanzisha shule zenye ubora wa hali ya juu zilizo jumuisha elimu kamili ya mtu na mafundisho ya kiroho—kitu ambacho kilikuwa nadra sana katika zama zake.
Kupitia kujifunza Biblia kwa bidii na uongozi wa Roho Mtakatifu, alisaidia kujenga mfumo wa Elimu wa Waadventista wa Sabato uliojikita katika kanuni kuu za Kibiblia ambazo huleta tofauti katika uwezo wa kila mtoto kujifunza na kukua.
Miongoni mwa waanzilishi wa awali wa dhehebu, Ellen White alikuwa mmoja wa wafadhili imara wa shule za Waadventista. Aliiona haja ya juhudi za elimu zilizokuza maisha yanayomcha Mungu na uhusiano wa karibu na Kristo, badala ya kujifunza vitabu vya msingi ambavyo vilizingatia mahitaji ya msingi tu.
Alikuwa na maono ya shule ambazo zingewasaidia wanafunzi kukua kifikra, kimwili, na kiroho.
“Elimu ya kweli inamaanisha zaidi ya kusoma kozi fulani. Inamaanisha zaidi ya maandalizi kwa maisha ya sasa. Inahusiana na kila kitu kwa mtu, na kwa kipindi chote cha maisha kinachowezekana kwa mwanadamu. Ni maendeleo yanayolingana ya nguvu za kimwili, kifikra, na kiroho. Inamwezesha mwanafunzi kufurahia huduma katika ulimwengu huu na furaha kuu ya huduma pana katika ulimwengu ujao.”20
Alizisaidia shule za Waadventista wa Sabato kutafuta malengo haya kwa kushiriki maelekezo ambayo Mungu alimpa kupitia karama ya roho ya unabii.
Aliandika kanuni hizi katika kitabu chake kinachoitwa, Elimu.
Baadhi ya kanuni hizi ni pamoja na:
- Masomo yote yanapaswa kufundishwa ndani ya mfumo wa Kibiblia.21
- Wanafunzi hujifunza stadi za vitendo na kushiriki katika kazi ya mikono.22
- Walimu wanapaswa kuhamasisha wanafunzi kufikiri kwa kina.23
- Wanafunzi wanapaswa kutumia muda zaidi nje katika asili.24
- Wanafunzi wanapaswa kujifunza jinsi ya kuwahudumia wengine, na mara kwa mara kupewa nafasi za kufanya hivyo.25
Ellen White, kwa mwongozo wa Roho Mtakatifu, pia alisaidia Kanisa la Waadventista wa Sabato kuamua mahali pa kuanzisha shule kadhaa za Waadventista, baadhi yake ni pamoja na:
- Chuo Kikuu cha Andrews (1874)26
- Chuo Kikuu cha Pacific Union (1882)27
- Chuo Kikuu cha Avondale (1897)28
- Chuo Kikuu cha Loma Linda (1905)29
Nyingi kati ya taasisi za elimu alizosaidia kuanzisha bado zinaendelea kufanya kazi leo. Na shule nyingine nyingi zaidi zimeanzishwa ulimwenguni kote.
Leo kuna shule zaidi ya 9,000 za Waadventista ulimwenguni kote.30 Hii ni pamoja na vyuo vikuu 118, shule za msingi 6,621, na shule za sekondari 2,731.31
Kwa ujumla, mfumo wa shule wa Waadventista ndio mfumo mkubwa zaidi wa shule za Kiprotestanti ulimwenguni kote.32
Hii ni kwa sababu ya Roho Mtakatifu anayefanya kazi kupitia Ellen White, pamoja na juhudi za bidii za walimu na wasimamizi Waadventista, ndio ndoto hii ya elimu inaendelea kustawi. Watoto hawawezi tu kujifunza zaidi kuhusu miujiza ya uumbaji wa Mungu, wanaweza pia kujifunza jinsi ya kumfahamu Muumba wao vizuri zaidi na jinsi ya kufuata uongozi wake katika maisha yao yote.
Urithi wake unathibitisha umuhimu wa kusoma na kufuata ukweli wa Biblia

Photo by Priscilla Du Preez 🇨🇦 on Unsplash
Na shauku yake ya kuelimisha haikukomea kwa watoto wadogo tu. Alijua kwamba kila mtu, kutoka kwa wasioamini hadi waamini wapya hadi wafuasi wa muda mrefu wa Kristo, ana mengi zaidi ya kujifunza kuhusu Mungu Muumba wetu na jinsi Anavyofanya kazi na jamii ya wanadamu.
Wakati Kanisa la Waadventista Wa Sabato lilipokuwa katika miaka yake ya mwanzo, Ellen White alihusika sana katika juhudi za kujifunza Biblia na baadaye kuanzishwa kwa imani za msingi. Kikundi kidogo lakini kinachoongezeka haraka cha waamini kilihitaji kuhakikisha kwamba imani zao pamoja zilikuwa zimejengwa imara katika Maandiko. Hawakutaka kutegemea sana tamaduni au falsafa maarufu za wakati huo.
Kupitia utafiti huu, Waadventista wa awali walikuja kuelewa dhana za msingi kama vile Sabato, Kuja kwa Kristo Mara ya Pili, na Hukumu ya Upelelezi. Na kwa sababu dhana hizi ni ngumu na zinategemea ufahamu wa sehemu nyingine za Biblia, mara nyingine juhudi za utafiti huu zilikwama kwa muda wanapokutana na kifungu ambacho hawakuwa na makubaliano ya pamoja juu ya jinsi ya kukielewa au kukitumia.33
Pia kulikuwa na nyakati katika historia ya Waadventista wa awali ambapo viongozi wa kanisa hawakukubaliana kuhusu baadhi ya dhana kuu za mafundisho ya Kiadventista. Mojawapo ya mijadala ya kitheolojia yenye utata zaidi ilikuwa juu ya mada ya wokovu kwa imani.
Ellen White alikuwa na mengi ya kusema katika moja ya mikutano ya Konferensi Kuu wakati mada hii ilipokuwa ikijadiliwa sana.34
Baadhi ya wajumbe walikuwa wenye bidii mno kuhusu kutii sheria ya Mungu hivyo wakapunguza umuhimu wa neema ya Mungu katika mchakato wa wokovu, ingawa inasisitizwa katika Maandiko kote.35
Ellen White alikubaliana kwamba watu wanapaswa kutii sheria. Mungu anawaomba wafuasi wake katika Biblia, na binadamu wanahitaji mfumo unaoeleweka wa maisha wanayopaswa kuishi. Lakini yeye, pamoja na waumini wenzake E.J. Waggoner, na A.T. Jones, walisisitiza kwamba hatupaswi kupunguza umuhimu wa neema ya Mungu na upendo wake usioelezeka uliodhihirishwa kwa kumtoa Mwana wake, Yesu Kristo, kufa msalabani.
Walizidi kutoa habari za msingi za Biblia kuhusu haki kwa imani, pamoja na ukweli kwamba imani yetu inadhihirishwa kupitia matendo yetu kwa uongozi wa Roho Mtakatifu (Yakobo 2:14-26).
Ellen White alijifunza Biblia kwa bidii na daima alikuwa akisikiliza mwongozo wa Roho Mtakatifu. Aliendelea kuchukua njia ya vitendo katika kujifunza mada hii ngumu. Na kama matokeo, aliwaomba waamini kukubali wokovu kwa imani, na mara walipofanya hivyo, kuishi maisha ya imani na huduma kwa Bwana kama mwitikio kwa upendo wake, sio kama njia ya “kujipatia” wokovu.
Mbali na kukabiliana na utii wa sheria uliokithiri, pia alikuwa na jukumu muhimu katika kuzuia Kanisa la Waadventista wa Sabato lisichafuliwe na mafundisho ya uongo au ya kupotosha ya falsafa maarufu au mifumo ya imani.
Moja ya falsafa hizi ilikuwa pantheism, wazo kwamba Mungu ni nguvu isiyo na utu badala ya nafsi Anayejali mahusiano, na kwamba hii “nguvu” ilikuwemo kila mahali, hasa ilionyeshwa kupitia asili. Ingawa Mungu bila shaka aliumba kila kitu na tunaweza kuona utukufu Wake ulioonyeshwa kupitia asili, tatizo kubwa la falsafa hii ilikuwa kwamba wale waliokuwa wakiifuata kwa kawaida mwishowe waliishia kuiabudu asili yenyewe, pamoja na watu wengine, kana kwamba kila kitu kilikuwa kimungu kikamilifu wakati wote. Hii ilipunguza umakini kutoka kwenye kuwa na uhusiano binafsi na Mungu mwenye upendo, ambaye aliumba kila kitu katika asili kwa ajili yetu kuheshimu, kufurahia, na kutunza—sio kwa ajili ya kukiabudu.36
Ellen White alionyesha mara kwa mara kwamba njia pekee ya kujenga mafundisho sahihi ni kupitia kusoma kwa makini Biblia chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu.
Pia alifuata uongozi wa Roho Mtakatifu ili kuwasaidia watu kutumia kanuni za Kibiblia katika maisha yao ya kila siku.
Ujumbe wa afya

“Courtesy of the Ellen G. White Estate, Inc.”
Ellen White aliacha urithi mkubwa katika uga wa afya na tiba. Alifanya hivi kwa kusisitiza uhusiano kati ya afya ya mwili, na afya ya akili na kiroho. Pia aliwafundisha watu jinsi tunavyoweza kutunza vema miili ambayo Mungu alitupatia, na hata alisaidia kuanzisha taasisi za afya ambazo bado zipo leo.
Roho Mtakatifu alimwongoza Ellen White kuhamasisha kuanzishwa kwa sanitarium (hospitali za nje ya miji zinazotibu magonjwa maalum au ya muda mrefu). Hata alipewa mwongozo kuhusu wanavyopaswa kutoa na wapi zinapaswa kujengwa. (Baadhi ya hizi ni pamoja na zile za Glendale, Paradise Valley, na Loma Linda).37
Sanitarium ni tofauti na hospitali za kawaida kwa sababu hufundisha wagonjwa kuhusu utunzaji wa kinga na zinapendelea matibabu ya asili yanayotegemea mtindo wa maisha.
Yaani, haziwatibu tu wagonjwa wao na kuwaacha. Wazo ni kuwasaidia kupona na kuwaonyesha wanavyopaswa kufanya ili kuhakikisha wanabaki wakiwa na afya njema baadaye.
Baadhi ya sanitarium hizi baadaye zilikuwa hospitali kamili, ingawa baadhi ya sanitarium bado zipo leo. Sasa tuna zaidi ya hospitali na sanitarium 230 za Waadventista duniani kote.38
Aina hizi za kliniki za afya zilikuwa na manufaa hasa wakati wa Ellen White. Aliishi wakati wa Mapinduzi ya Viwanda ya Marekani, ambayo ilikuwa pia wakati ambapo afya ya jumla iliharibiwa kutokana na mazoea mabaya katika usafi, kuwepo kwa sumu, mazingira hatari ya kufanyia kazi, na ufahamu mdogo kuhusu lishe sahihi. Akiongozwa na Roho Mtakatifu, alitambua haja ya kuboresha afya ya kimwili ya watu, ili waweze kufurahia maisha ambayo Mungu aliwapa na waweze kuwatumikia wengine vizuri zaidi.39

Photo by Juliane Liebermann on Unsplash
Aliandika pia vitabu kadhaa na barua nyingi ili kuwasaidia watu kuishi maisha yenye afya zaidi, yaliyojengwa kwa msingi wa habari ambazo Mungu alimpatia. Aliwahimiza watu kuacha kuharibu miili yao na akili zao kwa tumbaku na pombe, na kutumia muda nje kwenye mwanga wa jua na hewa safi, wakifurahia vitu ambavyo asili inatoa.
Ingawa hii inaweza isionekane kama ushauri wa mapinduzi kwetu leo, kulikuwa na wakati ambapo tumbaku ilikuwa inatumika kama tiba ya kawaida kwa takribani hali 65 tofauti za kiafya.40 Na watu hawakuzingatia njia za usafi au umuhimu wa kujumuisha matunda na mboga kwenye lishe yao ya kawaida.
Miongozo yake thabiti kuhusu jinsi ya kutunza miili yetu kwa njia za vitendo inaweza kufupishwa na pointi muhimu hizi, ambazo sasa inajulikana kama mfumo NEWSTART:41
N= Lishe
E= Mazoezi
W= Maji
S= Mwanga wa Jua
T= Kiasi
A= Hewa
R= Mapumziko
T= Kuamini katika nguvu ya Mungu
Wafanyakazi wa Sanitarium walihimizwa kuwafundisha wagonjwa wao kuhusu kanuni hizi za afya. Na ilichukuliwa kuwa mapinduzi wakati huo kufuata lishe ya mimea, ambayo alisisitiza ingesababisha mwili na akili yenye afya.
Kanuni hii, inayoakisi kanuni kutoka Danieli 1, imeonekana tangu wakati huo katika utafiti wa afya ya Mwadventista, kusaidia watu kuepuka kupata kisukari, kansa, kiharusi, na magonjwa mbalimbali ya moyo.
Kwa kuwafundisha watu kuhusu Yesu na kuanzisha mfumo wa shule za Kikristo, urithi wa Ellen White umewasaidia watu kuishi maisha marefu na yenye furaha. Ndiyo maana vitabu vingi vya White vinasisitiza umuhimu wa afya kamilifu na jinsi inavyoweza kusaidia maisha ya utumishi kwa Mungu na wengine.
Kwa ujumla, hata hivyo, maandishi yake yanajumuisha aina mbalimbali za mada za kitaaluma na za vitendo. Ingawa alipata elimu rasmi ambayo ilikoma akiwa na umri wa miaka tisa tu, alikuwa mwandishi wa kike aliyetafsiriwa zaidi katika vitabu vya kisasa visivyo vya hadithi za kufikirika.42
Urithi wa Ellen G. White katika uchapishaji

Photo by Emmanuel Phaeton on Unsplash
Kati ya mafanikio yote ya Ellen White, maandishi aliyochapisha ndiyo urithi wa kudumu zaidi wa huduma yake.
Wakati ambapo vuguvugu la Kikristo lililokuwa changa lilipohitaji uongozi na mwelekeo wa kimungu, maandishi yake yalitumika kurejea kanuni za Kibiblia ambazo mara nyingi zilisahauliwa, kueleweka vibaya, au kutumiwa vibaya katika siku zake. Hii ilijumuisha mada muhimu kama afya, tabia ya Kikristo, uongozi wa utumishi, mafundisho, injili, na vipawa vya roho.
Kulingana na Tim Poirier, Makamu Mkurugenzi wa Hazina ya Ellen G. White, jambo muhimu zaidi kuhusu maandishi yake ni kwamba:
“Yanatoa mafundisho ya kiroho na vitendo kwa ajili ya kuishi katika ulimwengu huu na kujiandaa kwa ulimwengu ujao.”
Na kwa sababu mambo haya yameandikwa, hatuhitaji kuwa na wasiwasi kuhusu kusahau aliyotufundisha. Maneno haya yenye manufaa yameandikwa kwa faida na ukuaji wa Kanisa la Waadventista wa Sabato (hasa vitabu kama Shuhuda kwa Kanisa) na kwa wale wanaotaka kukuza uhusiano wa kibinafsi na Mwokozi wao, Yesu Kristo (kwa vitabu kama Hatua Kuelekea kwa Kristo).
Ingawa maandishi yake yalikuwa yameandikwa kwa ajili ya waamini, na mara nyingine yakiwalenga Waadventista moja kwa moja, kila mtu anaweza kupata mambo muhimu ya kivitendo katika maandishi yake. Hata ingawa aliandika vitabu hivi zaidi ya karne moja iliyopita, kanuni za msingi zinaweza kutumika nyakati zote.
Taasisi ya Ellen G. White inamiliki maandishi yote binafsi na yaliyochapishwa ya Ellen White. Wana jukumu la kuhifadhi kwa uaminifu na kushiriki maandishi yake ili ulimwengu uweze kusoma.
Ikiwa unatamani kusoma maandishi yake wewe mwenyewe, unaweza kuyapata kwenye egwwritings.org.
(Na kwa wale wanaopendelea kusikiliza badala ya kusoma, wana matoleo ya sauti ya kidijitali ya maandishi yake.)
Aliandika zaidi ya kurasa 100,000 kwa ujumla katika maisha yake.43

“Ellen White”
Baadhi ya kazi zake maarufu ni Tumaini la Vizazi Vyote na Njia Salama, zote zilizochapishwa na Pacific Press na zinaweza kupatikana katika kila Duka la Vitabu la Waadventista, miongoni mwa maeneo mengine.44
Leo, urithi wake unaendelea kuishi hasa kupitia maandishi yake, ambayo ndiyo jinsi Mungu alivyomkirimia kushiriki upendo Wake na ujumbe wa Injili kwa ulimwengu. Kupitia hayo tunaweza kuona kina na upana wa kazi yake.
Matokeo ya Kazi ya Ellen G. White
Ellen White alikuwa mke mwaminifu, mama, rafiki, mjumbe, mzungumzaji, mwalimu, mwana matengenezo ya afya, na mwanaharakati wa ubinadamu.
Mahali popote alipokwenda, watu kwa ujumla walitoa maoni mema kumhusu. Kwa kweli, kila Mungu alipomwita kutembelea mji kuzungumza au kukutana na watu, wengi wa wenyeji walijikuta wakitamani angebaki.45
Na hakuwa anatambuliwa tu kwa kiwango binafsi. Magazeti makubwa haraka yakagundua mvuto aliokuwa nao ulimwenguni.
Kwa kweli, muda mfupi baada ya kufariki kwake, New York Independent, jarida la kila mwezi, liliandika:
“Alikuwa mwaminifu kabisa katika imani yake kuhusu maono yake. Maisha yake yalikuwa na maadili hayo. Hakuonyesha kiburi cha kiroho wala kutafuta faida chafu. Aliishi maisha na kufanya kazi ya nabii anayestahili.”46
Hii ni sehemu kubwa ya sababu kwa nini alitambuliwa na Jarida la Smithsonian. Aliwasaidia watu wasio hesabika kutafuta majibu katika Biblia, na alisaidia katika kuboresha afya ya jumla ya Wamarekani. Kwa kuwa chombo tayari kwa ajili ya Roho Mtakatifu kufanya kazi kupitia kwake, alifanikisha mambo ya kustaajabisha.
Unataka kujifunza zaidi kuhusu moja ya vitabu maarufu vya Ellen White? Angalia,
Kurasa zinazohusiana
- “How many books and articles did Ellen White write?” [↵]
- White, Ellen G., “I’d Like to Ask Sister White,” Ellen G. White Estate, p. 87. [↵]
- Ibid, p. 85-87. [↵]
- Ibid, p. 91. [↵]
- Ibid, p. 90. [↵]
- “Edson White: His Conversion and Work,” [↵]
- Ibid. [↵]
- Ibid. [↵]
- Ibid. [↵]
- Ibid. [↵]
- Ibid. [↵]
- Ibid. [↵]
- Ibid. [↵]
- “Edson White: His Conversion and Work,” [↵]
- Norman, Steve III, “James Edson White: A ‘No Limit’ Man,” [↵]
- Ibid. [↵]
- William Clarence ‘Willie’ White,” [↵]
- Ibid. [↵]
- Ibid. [↵]
- White, Ellen G., Education, p. 13. [↵]
- Ibid., p. 17. [↵]
- Ibid., p. 219. [↵]
- Ibid, p. 231. [↵]
- Ibid., p. 101. [↵]
- Ibid., p. 215. [↵]
- “Andrews Facts,” [↵]
- “About PUC,” [↵]
- “About Us,” [↵]
- “About the University,” [↵]
- “Seventh-day Adventist Education Statistics,” [↵]
- Ibid. [↵]
- “Now more than ever! Adventist Education,” [↵]
- White, Ellen Gould, Selected Messages Book 1, pp. 206-207. [↵]
- Douglass, E. Herbert, Messenger of the Lord, p. 195. [↵]
- Ibid. [↵]
- Ibid, pp. 200-201; White, Ellen G., Testimonies for the Church vol. 8. [↵]
- Douglass, p. 163. [↵]
- “Quick Statistics on the Seventh-day Adventist Church,” [↵]
- Ellen G. White, Counsels on Health, p. 6. [↵]
- anchez-Ramos, R. Juan, “The rise and fall of tobacco as a botanical medicine, ”[↵]
- “The NEWSTART Program,” [↵]
- White, Arthur L., Ellen G. White: A Brief Biography. [↵]
- “How many books and articles did Ellen White write?” [↵]
- “What is Ellen White’s Most Popular Book?” [↵]
- Skrzypaszek, John, “Ellen G. White’s Ministry in the South Pacific,” [↵]
- The Test Results Pt.4,” [↵]
Majibu Zaidi
Sabato katika Maisha na Mafundisho ya Ellen White
Sabato katika Maisha na Mafundisho ya Ellen WhiteSabato ni mada muhimu katika Kanisa la Waadventista wa Sabato. Sio jambo la kushangaza, basi, kwamba Ellen G. White, mwanzilishi mwenza wa kanisa, alisoma mafundisho ya Biblia kuhusu Sabato na akaandika kiasi kikubwa...
Hatua Kuelekea kwa Kristo: Mwongozo wa Uhusiano na Yesu
Iwe unanza safari yako na Yesu Kristo, unarejea baada ya muda fulani, au umekuwa na uhusiano na Yesu kwa miaka, kutumia kitabu
Wafahamu Watoto wa Ellen White
Ellen White, ambaye ni mmoja wa waanzilishi maarufu zaidi wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, alikuwa na watoto wanne na mumewe, James: Henry Nichols, James Edson, William Clarence, na John Herbert.
Jinsi Mafundisho ya Ellen White Yanavyoweza Kuboresha Afya Yako
Matibabu katika karne ya kumi na tisa yalisemekana kuacha “ugonjwa zaidi kuliko yalivyotibu” kwa matumizi yake ya kutoa damu na “dawa” kama zebaki na arseniki.
Jinsi Ellen White Alivyochangia Ujumbe wa Afya wa Waadventista
Jinsi Ellen White Alivyochangia Ujumbe wa Afya wa WaadventistaWaadventista wa Sabato wanajulikana kwa kusisitiza maisha yenye afya bora. Na Ellen G. White alikuwa na ushawishi mkubwa katika maendeleo ya kipaumbele hiki na utekelezaji wake miongoni mwa Waadventista....
Ellen White anasema nini kuhusu Maombi?
Je, umewahi kuwa na mzigo ambao ulihitaji kumwambia mtu, lakini uliogopa kuhukumiwa ikiwa ungefanya hivyo?
Ellen G. White au Biblia—Kipi ni Muhimu Zaidi kwa Waadventista?
Biblia—bila shaka—ndiyo kitabu muhimu zaidi. Ni kipimo tunachotumia kupima maandishi mengine yote, ikiwa ni pamoja na yale ya Ellen White.
Ellen G. White Alisaidia Vipi Katika Kuanzisha Kanisa la Waadventista wa Sabato?
Ellen G. White, mwanamke mnyenyekevu kutoka Gorham, Maine, alikuwa mmoja wa waanzilishi wa Kanisa la Waadventista wa Sabato na kiongozi muhimu tangu mwanzo wake.
Ellen White na Kitabu cha Pambano Kuu
Pambano Kuu ni moja ya vitabu vya Ellen G. White vinavyo thaminiwa zaidi na Waadventista wa Sabato.
Roho ya Unabii Ni nini (Kitabu cha 1-4) na Ellen G. White?
Kutumia unabii wa Biblia katika historia, matukio ya hivi karibuni, na hasa siku za usoni, inaweza kuwa kazi ngumu. Hata linaweza kuwa jambo la kutisha kidogo kwa baadhi.
Ellen White Alifundisha nini Kuhusu Matumizi ya Vyakula Vinavyotokana na Mimea?
Moja ya mambo ambayo unaweza kuwa umewahi kusikia kuhusu Waadventista wa Sabato ni msisitizo wao kwenye mtindo wa maisha wa kutumia vyakula vinavyotokana na mimea.












